Showing posts with label Relationship and Marriage. Show all posts
Showing posts with label Relationship and Marriage. Show all posts

Wednesday, December 7, 2016

KANUNI ZA KIROHO ZA KUMPATA MWENZI

NA MCHUNGAJI JOEL HAMULI

Mwanzo 24

1.  Kupata mwenzi miongoni mwa WAAMINI. Mwanzo 24:1-4
-  Abrahimu alimtaka mtumishi wake kumtwalia Isaka mke kutoka kwa "jamii yake"
-  1Wakorintho 15:15-16 huwezi kujiunganisha na "makahaba" au kufanyika mwili mmoja na wasioamini

2.  Chochote ukitakacho kwa Bwana unakipata kwa IMANI.

-  Mwanzo 24:6-7 Mungu alimuapia Ibrahimu kumpa uzao wake nchi hiyo. Hivyo alimwamini Mungu na akamwambia mtumishi wake kwa imani kwamba Mungu angemtuma malaika wake kumwongoza kupata mke.
-  Filemoni 6:4 msisumbuke kwa neno lolote bali ktk kila jambo kwa kuomba na kushukuru. Badala ya kujishughulisha na kujisumbua sana kutafuta mke/mume, mwambie Mungu kasha endelea kuamini.

3.  Lazima kuwe na MAANDALIZI. Mwanzo 24:10-11

-  Maandalizi stahiki kadri ya taratibu zinazokubalika ni muhimu.
-  Luka 14:28 Kabla ya kujenga, kaa chini hesabu gharama
-  Jiandae kiroho, kimwili, kisaikolojia, nk
-  Ikiwa wamtaka kutoka kwa Mungu, timiza mapenzi yote ya Mungu. Matendo 20:27

4.  Fanya MAOMBI. Mwanzo 24:12-14

-  Ombea jambo hili na ujue mapenzi ya Mungu kulihusu.
-  Usiwe mgumu kubadilika na kulazimisha mapenzi yako, unaweza kuwa na vigezo vyako, lakini si lazima Mungu ajibu hivyo. Ila waweza kuomba ili kupata uthibitisho wa ki-Mungu

5.  Chukua HATUA

-  Kwa tamaduni nyingi mwanaume ndiye huanzisha mchakato kwa kwenda kuomba uchumba. Mwanamke anaweza pia Biblia haijakataza, lakini zingatia matokeo yake. Kwa kuwa upendo unaoshikilia ndoa ni wa mwanaume, inabidi yeye ndio ashawishike zaidi juu ya msichana. Ndiyo maana yeye anaagizwa kupenda na mwanamke kutii.

6.  Kuhusisha watu WENGINE. Mwanzo 24:28-31, 50

-  Yafaa kueleza familia. Zamani familia zilibeba jukumu la kijamii na kiroho
-  Kwa sasa majukumu ya kiroho yapo kwa kanisa, kwa hiyo waambie viongozi wako wa kiroho wakuongoze, hata kabla ya kwenda kwa wazazi

7.  Msichana KUKUBALI. Mwanzo 24:57-58

-  Msichana inabidi kwa utashi wake mwenyewe aamue kumkubali na kuolewa na mwanamume husika.
1Wakorinthi 7:39 inaongelea juu ya mwanamke kuolewa na mwanamme “amtakaye”. Kuingia kwenye ndoa kwa kulazimishwa si mapenzi ya Mungu.

Makala hii ni sehemu ya semina ya Mahusiano na Ndoa iliyofundishwa kanisani City Harvest na ni sehemu ya kitabu kilicho njiani.

Wednesday, November 23, 2016

MWENENDO WAKATI WA UCHUMBA

Mambo ya kufanya na yasiyofaa kufanya kabla na wakati wa uchumba

Mhandisi Lucas & Happiness Mgalula (TAG City Harvest Church)


Kila mtengenezaji huweka kitabu cha maelekezo ili kuelezea namna ya utumizi wa kitu husika.

Mungu ametupa nguvu na twaenda kwake kujifunza kuhusu udhibiti wa nguvu hizo, Power & Control

Mara nyingi huwa tunaangalia uchumba lakini kuna mahali umeanzia, mahusiano ya urafiki. Tunaangalia namna vijana waliookoka wanavyopaswa kuenenda katika mahusiano kuelekea ndoa.

Umri huu ni kipindi muhimu ambacho hakirudi tena, ni cha muhimu kwako, kwa familia, wazazi, kanisa, jamii nzima na Mungu. Wote wanakutegemea upite salama na kufanikisha kusudi la Mungu.

Kabla ya Uchumba

Kipindi unachojiuliza ikiwa utapata mtu sahihi na ikiwa moyo wako utamkubali. Hata usipoijua njia, hautapotea

I.      Mahusiano na wenzako

-  Fanya ni utaratibu wako kuomba juu ya mahusiano uliyonayo na wenzako ili ule utakaopelekea ndoa ushamiri zaidi na yale yatakayoleta vurugu yafe! Mwanzo 24:12-14 aliyetumwa kumtafutia Yakobo mke alikuwa makini kuomba hivyo
-  Mwambie Mungu akusaidie ili ule uhusiano ulio makini uuone.
-  Anaweza kutokuwa na vigezo vyote unavyovidhania lakini akawa ndiye hasa. Isaya 30:21 Hii ndiyo njia, ifuate

II.  Tafuta ushauri wa wenye hekima wa Mungu

-  Unapoona kama uhusiano mmoja unashamiri na unaweza kupelekea kwenye uchumba, tafuta ushauri wa wenye hekima waliookoka hasa wanandoa.
-  Kuna mambo mengi njiani ambayo utahitaji maombi na msaada wao.
-  Mungu hukupa mwanamke/mwanaume, kazi kwako kumjenga awe mke/mume
-  Hakuna anayekuwa amekamilika, maana hakuna aliyekuwa mume au mke kabla hamjatangazwa hivyo na kuanza kuishi pamoja. Hakuna anayenunuliwa sokoni akiwa kamili
-  Hekima huja kwa kusikia au kupitia, hakuna aliyekuwa amepitia ndoa kabla, hivyo ni vema kupata wanandoa wenye hekima wakusaidie
-  Usiufiche uhusiano wako unaoelekea kwenye uchumba, ni hatari

III.    Kuwachukulia wote kuwa ndugu zako

-  Watu wote unaohusiana nao kanisani na kwingineko, wachukulie kama dada au kaka. Mvulana usiwadharau wadada na msichana usiwachukulie wakaka kama watu waonevu
-  Kuna aina hii ya heshima ambayo kaka na dada wanakuwa nayo kwa kila mmoja. 1Timotheo 5:1-2 Kwa usafi wote, nia, kimawazo, maneno na matendo
-  Sote tu wa damu moja, tumenunuliwa kwa damu ya Kristo
-  Kwa kuhusika katika shughuli nyingi za kanisa zinazoweza kuwaleta pamoja na mkafahamiana, ndipo waweza kujua namna ya kuamua ikiwa tabia zenu zitaendana na mtachukuliana. "Birds of feathers flock together"
-  Baada ya kumfahamu, heshima iendelee, hapa ni kabla ya kuwa “Mr. Special” au “Ms. Special”
-  1Wakorintho 13:4-8 (Sifa za Upendo)
-  Linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
-  Kama kuna kitu "special" baina yenu ni bora ukiseme na siyo kuficha ficha. Acheni kung'ang'aniana kama kumbikumbi kila uendako naye yupo halafu mnasema hakuna kinachoendelea baina yenu. Hiyo ni mbaya na hatari na unaweza kukosa "opportunity" na hata kumkosea Mungu.

NOTE: Don't treat anyone special! Don't single her out! Avoid over-clinging to one person when there is nothing-marital material!

Kabla ya Ndoa

-  Usimtembelee mtu wa jinsia tofauti (mchumba) kwake mkiwa peke yenu.
-  Usimfulie, kumpikia au kumsafishia nyumba. Kwa nini upate privileges za ndoa kabla? Una haraka gani?
-  Inaweza kuanza vizuri na kwa nia njema lakini mkaangukia kwenye "premarital sex and pregnancies" ambayo italeta majuto, uchungu na chuki

Wakati wa mahusiano/uchumba

-  Usichochee mapenzi kabla ya wakati wake. Ni mchumba wako lakini haimaanishi unao uhuru wa kufanya lolote utakalo. Huwezi kuwa Rais kabla ya kuapishwa
-  Mwili wako unatambua tayari kwamba huyu ni mtu maalumu, nao unajiandaa na kuitikia hivyo. Kuwa makini.
-  Avoid physical touches, as they will result into premarital sex and unplanned pregnancies
-  Uchumba unaweza kuvunjika. Mungu atakupa amani ndani yako kuendelea mbele, isiwe mzigo kwako ukatumia nguvu nyingi kumridhisha au kumweka kwako halafu mwitikio ukiwa mdogo unaanza kujiuliza kwa nini. Usijilazimishe au kukubali kwa kumhurumia. Ikiwa haiwezekani sema kwa upendo na upole. Ikiwa ana shida, ndiyo maana Mungu akakufunulia wewe ili uchukue hatua za Kikristo kumsaidia

Swali: Vipi kuhusu kutoa zawadi kwa mtu uliye kwenye mahusiano naye/mchumba?
-  Zawadi inaweza kuwa aina fulani ya rushwa, inaufunga moyo wa mtu. Anaweza kukukubali kwa hizo kwa kuwa umeuteka moyo wake na utalazimika kuwa unafanya vitu kwa ajili yake ili aendelee kukukubali

-  Ni bora ukilazimika au kujisikia kutoa zawadi, utoe ambayo haitaumiza moyo wako mambo yakienda kombo. Usianze kununua naye vitu vya thamani, kuwekeza pamoja, kujenga, viwanja na kadhalika.


-  Ni vema upendo ukaja kawaida, zawadi zitafuata kwa nafasi yake

Wednesday, November 16, 2016

KUJAMIIANA, UASHERATI NA USAFI - MCHUNGAJI YARED DONDO, TAG CITY HARVEST CHURCH


Pastor Architect Yared Dondo - TAG City Harvest Church
 Upendo wa Kweli Hungoja – Waebrania. 13:4

Mpango wa Mungu kuhusu kujamiiana unahusisha mwanaume mmoja na mwanamke mmoja walio ndani ya uhusiano wa ndoa. Serikali na dunia kwa ujumla hutumia mamilioni ya fedha kwa kinaitwa “ngono salama”. Hakuna ngono salama zaidi ya iliyo ndani ya mpango wa Mungu!
Tafsiri ya kidunia kuhusu ngono salama haijaegemea kwenye maadili hata kidogo. Mawazo yao ni kuwa: “ikiwa hauwezi kuenenda vyema, basi kuwa mwangalifu”.
Tafsiri ya Mungu wa ngono salama ni kungoja mpaka ndoa.
1 Petro 2:11 “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho”

Maadili ya Kibiblia huchekwa, hudharauliwa husemwa ni ya kale na yamepitwa na wakati.
Ninashukuru kwa ajili ya viajana matineja wachache ambao leo wanasema, kuanzia leo na kuendelea, nitangojea mpaka wakati wa ndoa….. nitaishi sawa na mpango wa Mungu….. na watu wazima wanaojitoa tena kuwa wasafi na waaminifu. Tumeliruhusu neno ngono/kujamiiana kuwa neno chafu. Kilichopaswa kuwa taswira njema ya upendo, ndoa na maskani, kwa sasa kinahusishwa na upotovu/ukimwi/ukahaba/usagaji/ngono ya jinsia moja.
Jamii inajifunza kwamba kuna adhabu ya uasherati na uzinzi. Lakini badala ya kurejea kwenye viwango vya Mungu na kutii sheria za Mungu, jamii husema “wacha tuone tunachoweza kufanya kukwepa matokeo ya matendo yetu”
Hapa ndipo hatari iko: ikiwa utaingia kwenye uhusiano wa kimwili kabla ya ndoa:

Hatari 5 za ngono kabla ya ndoa:

1.             Pendo bandia
Mahusiano yaliyojengwa juu ya ngono hayadumu! Mkianza na mambo ya kimwili mtajikuta hata hamvutiani. Hamtakua pamoja kiakili, kihisia au kiroho!
Upo hapo ukiwa hauna kitu isipokuwa malai/krimu iliyochapika na inazeekana ambayo utaitupa pia! Lakini…ikiwa kujamiiana kutaanza baada ya ndoa, sehemu nyingine tatu zitaendelea kukua pia! Hivyo unakuwa na siyo tu mshirika wa kujamiiana, bali pia rafiki bora zaidi anayekupenda.
Upendo wa kweli huvumilia, ni halisi na hauna ubinafsi.
Wasichana, pale mwanaume anaposema “Siwezi kusubiri”, utajua kwamba hakupendi. Pale anaposema “Ikiwa wanipenda kweli, nithibitishie”, chukulia hilo kuwa tusi na umchape kibao cha nguvu kiasi cha ubongo wake kupiga kelele kama kengele za kanisa wakati wa asubuhi yenye baridi!

Hatari za upendo wa bandia..

2.             Madhara kihisia

Mabinti wadogo:
Tafiti zinaonyesha uhusiano wa moja kwa moja baina ya ngono kabla ya ndoa na matatizo binafsi ya kihisia… Kujihisi mkosaji/wasiwasi/kupoteza kujiheshimu
Kujihisi una hatia ndiyo hisia inayoweza kutuharibu zaidi.
Hukukosesha usingizi, amani, furaha, kujithamini na uhusiano wako na Mungu.
Hukuacha umevunjika vunjika, ukiwa hauna uhakika na kutoweza kuzalisha matunda.
Na kisha hupoteza ule “mng’ao” unaoambatana na usafi.
Sikieni haya mabinti, na nitawaambia namna wanaume hufikiri…
…..kuna fumbo fulani kuhusu yasiyojulikana. Kuna kitu fulani cha kuvutia sana kuhusu yasiyojulikana.
Mara tisa kati ya kumi, pale unapojifunua kwa mwanaume, baada ya fumbo kuondoka, naye pia huondoka….atakudondosha kama jiwe la moto! Na haitakuwa kama kuachana kwingine kokote, itakuwa kama kupewa talaka.

3.             Madhara ya Kimwili

Bado mshahara wa dhambi ni mauti!
Kuwa mchafu – uko katika hatari ya magonjwa yasiyo na tiba. Kuna magonjwa saba, nje na ukimwi ambayo hayana tiba na yote yamebeba madhara ya muda mrefu, na yote huenea na huhusiana na kundi la watu walio tayari kufanya ngono nje ya usalama wa ndoa!
Utasema yuko tayari kuwa nami pekee. Usijihakikishie hivyo! Ikiwa wako tayari kufanya ngono nawe, basi wako tayari pia kufanya na wengine, na huenda wamekwisha kufanya hivyo tayari.
Unapolala na mtu, unalala na historia nzima ya ngono ya mtu huyo na KILA MTU ambaye amepata kuwa naye.
Mshahara wa dhambi bado ni mauti.

Hatari ya upendo bandia, madhara ya kimwili na kihisia…

4.             Madhara katika ndoa

Nimewashauri watu ambao wamekuwa wakisema “ni swa kwetu kufanya ngono kwani tunajua tutaoana”. Hapana, si sawa…. Kwa nini?
Kwa kuwa Mungu amesema si sawa…. Nani atakaye kubadili sheria yake? Inawezekana usionane naye!
Kwa wastani, kijana tineja hupenda takribani mara 10 kabla ya kuingia katika ndoa
Hivyo, hata ikiwa umeonana naye, umepunguza nafasi za kuwa na ndoa yenye furaha kwa kuwa umemegua msingi wa uaminifu. Kwenye akili yako, siku zote kutakuwa na lile wazo kuwa mtu uliyeoana naye anauwezo wa kuwa mdanganyifu. Waliweza kufanya dhambi nawe kabla ya ndoa, wanaweza kufanya dhambi dhidi yako sasa baada ya kuoana.

Kisha kuna…

5.             Madhara ya kiroho

Lakini Mchungaji, hauamini kuwa Mungu husamehe? NDIYO, NINAAMINI!
Lakini msamaha na madhara ni mambo mawili tofauti. Huwa tunadhani mambo yote mawili yanaishi kwenye mstari mmoja, kuwa tunapousogolea zaidi msamaha ndivyo tunakuwa mbali na madhara… siyo hivyo!
Daudi alifanya dhambi na Bathsheba na kisha akafanya amauaji…na katika vifungu viwili vya ajabu vya Biblia tunaona msamaha wa hali ya juu ambao Daudi aliomba na kupokea – lakini ngoja niulize, madhara hayakuendelea kuwepo?
Ndiyo. Mungu akasema, “Daudi, utaishi katika bonde la machozi maisha yako yote. Upanga hautaondoka nyumbani mwako”
Alimzika mwanae aliyefariki. Kisha mwanaye mmoja akambaka bintiye. Na Mungu akasema ni matokeo ya moja kwa moja ya dhambi zake.

Namna gani ubakie safi?
1.             Linda ufahamu wako
Mlango wa macho na mlango wa masikio ni muhimu sana…. Ni barabara kuu ya ufahamu.
2 Petro 2:14 “macho yaliyojaa uzinzi”
Wanaume, lindeni macho yenu. Biblia inasema (Zaburi 101:3) “Sitaweka mbele ya macho yangu neno la uovu”. Dai mstari huo
Ayubu alisema “Nilifanya agano na macho yangu, basi nawezaje kumwangalia msichana kwa kumtamani?” jiweke mbali na muziki ambao maudhui yake ni tamaa ya kingono.

2.             Usiatamie dhambi

Ikiwa huwezi kuingia duka la videa na kusalia msafi, usiingie kabisa!
Ikiwa huwezi kuperezi kwenye vituo vya televisheni pasipo kutazama kitu kichafu, basi zima kabisa. Ikiwa hamwezi kuwa peke yenu kwenye gari, basi msikae peke yenu.
“Usiupe mwili nafasi”

3.             Azimia kabla

Fanya maamuzi ya awali kubakia msafi, na kuwa hutaingia kamwe kwenye uhusiano na mtu ambaye hajafanya maazimio kama hayo.
Maneno ya mpumbavu: “Atabadilika mara tutakapooana”
Wewe unasema: “Nimechelewa mno mchungaji” (Tayari nimeshatoa)
Habari njema! Siku moja mwanamke aliletwa kwa Yesu, akiwa ameshikwa akifanya uzinzi. Alitarajia kuhukumiwa, lakini Yesu akamwambia, Sikuhukumu, enenda zako na usifanye dhambi tena!


Huwezi kubadili yaliyopita, lakini mustakabali wako waweza kuwa bila madoa!

Friday, April 11, 2014

COUPLES SEMINAR COUPLES SEMINAR It is here again......


You are all Welcome to  the Couples Seminar (Semina ya Ndoa) to be held in Dar es Salaam

 

When: 21st April 2014 -Easter Monday


Time: 9:30 a.m to 5.00 p.m
 
 
Where: Mirado Hall, Sinza Makaburini, Dar es Salaam, Tanzania

Theme: Successful Marriage, Successful Family, Successful Nation


Entrace Fee: 35,000/= Couples

                     20,000/= Singles

Speakers : Dr Elly
                   Eng. Lucas and Happiness Mgalula
                   George & Sayuni Mngodo

Event Host: Pastor Yared and Matilda Dondo
                      Mr and Mrs Harris Kapiga

What to expect: After having an interview with one of  the seminar hosts, he revealed that he expects a major transformation to all the couples who will attend.

Main Topic: The main topic for the day is scheduled to be Romance and Sex in Marriages which has been one of the key concerns in today's marriages.


Food and Soft Drinks will be served

Friday, February 14, 2014

Should Christian Celebrate Valentine Day


 
 
Today is called “Valentine’s Day” by many throughout the world. Should Christians observe it?

Some Christian Media, Organizations and Institutions endorses its observance .Hence apparently they feel that Valentine’s Day is appropriate for professors of Christ.

But is it Christian?

The old World Book Encyclopedia (Valentine’s Day. Volume 19. 1966, pp.205-206) states,

…the customs of the day have nothing to do with the lives of the saints. They probably come from an ancient Roman festival called Lupercalia which took place every February 15. The festival honored Juno, the Roman goddess of women and marriage, and Pan, the god of nature…The Romans celebrated their feast of Lupercalia as a lovers’ festival for young people. Young men and women chose partners for the festival by drawing names from a box…After the spread of Christianity, churchmen tried to give Christian meaning to the pagan festival. In 496, Pope Gelasius changed the Lupercalia festival of February 15 to Saint Valentine’s Day February 14. But the sentimental meaning of the old festival has remained to the present time. Historians disagree about the identity of St. Valentine”. Furthermore it also states, “LUPERCALIA…was celebrated on February 15 in honor of Faunus, a rural Italian god. Faunus was later identified with Pan, the god of herds and fertility…Priests…ran around striking all the women the met (Lupercalia. Volume 12. 1966, p.456).

The pagan being named Cupid (a supposed son of the pagan goddess Venus) was also involved. According to pagan mythology, anyone being hit by Cupid’s arrow falls in love with the first person he/she sees. One source was bold enough to state,

The church replaced elements of various love-gods (Juno Februata, Eros, Cupid, Kama, Priapus) with St. Valentine, an imaginary Christian. A number of contradictory biographies were created for him…By taking over some of the features of the Pagan gods and goddesses, St. Valentine became the patron saint of lovers…St. Valentine’s Day can be traced back to Lupercalia, the Roman “festival of sexual license” (ST. VALENTINE AND VALENTINE’S DAY, http://www.religioustolerance.org/valentine1.htm, February 6, 2004).

Notice what the Roman Catholics teach,

The roots of St. Valentine’s Day lie in the ancient Roman festival of Lupercalia, which was celebrated on Feb. 15. For 800 years the Romans had dedicated this day to the god Lupercus. On Lupercalia, a young man would draw the name of a young woman in a lottery and would then keep the woman as a sexual companion for the year (The Origins of St. Valentine’s Day. http://www.americancatholic.org/Features/ValentinesDay/, January 31, 2004).

It is of interest to note that the same Catholic source states,

The Catholic Church no longer officially honors St. Valentine, but the holiday has both Roman and Catholic roots.

Does Valentine’s Day sound like a holy festival of love or a pagan holiday of lust?

Wednesday, September 18, 2013

Uchumba hadi Ndoa: Ni Vizuri Watarajiwa kukubaliana juu ya mipaka watakayokuwa nayo kwa Ndugu wa pande zote mbili



 

Shalom Mtu wa Mungu, leo nakuletea somo muhimu sana juu ya kukubaliana na mwenzi wako jinsi mtakavyokuwa mnaishi na ndugu zenu, yaani wakwe kwa upande wa mwanaume na mwanamke pia.

Ni muhimu mkaweka  msingi mapema maana wazazi na ndugu za pande zote mbili ni muhimu sana sana kwenu wala hawahitajiki kuupuuziwa ila tu msipoweka mipaka inaweza kuleta shida kubwa sana katika maisha yenu ya huko mbele mtakapokuwa mmefunga ndoa.

Wakati mwingine ndugu za pande zote mbili wamekuwa wakijisahau na kufikiri wana nafasi ya kuamua juu ya maisha yenu kama wanandoa. Lakini katika Biblia tunaona kuna mifano mingi jinsi wanandoa walivyoishi vizuri na wakwe zao kukawa na uhusiano mzuri kati ya wakwe na mkwe kama Ruth na Naomi walivyopendwa na kuishi vizuri na wakwe zao.

Lakini pia tunaona jinsi ambavyo Mfalme Daudi alivyopata shida na baba mkwe wake Mfalme Sauli hadi Sauli akataka kumuua Daudi.


Mahusiano mabaya kati ya mkwe na wakwe yanaweza kusababisha wanandoa kuishi kwa shida kubwa sana na mara nyingine imesababisha ndoa kuvunjika kabisa na kuleta chukizo mbele za Mungu.

Sasa ili kuepusha hayo ndio maana tuko hapa leo kukuambia kwamba msije mkajisahau mkaongelea tu jinsi mtakavyojenga Masaki au Kibada bila Kuzungumzia jambo hili mapema maana kama usipoliweka sawa hutaishi kwa Raha, Ninaposema Ndugu hapa namaanisha ni mama,baba,kaka,dada,shangazi,mjomba,bibi ,babu na ndugu wengine wa kwako wewe au wa mwenzi wako pamoja na uzao wao.

Zingatieni yafuatayo ili kuepusha hiyo migogoro inayosababishwa na ndugu;

 

1. Zungumza na Mwenzako

Mzungumze jinsi mtakavyoweka mipaka kwa ndugu zenu wote itayaepusha ndugu kuingilia mahusiano yenu

Kwa mfano sikilizeni ushauri kutoka kwa wakwe maana pia ni mzuri sana kwasababu wao kwanza wameona mengi kuliko nyie ila kabla ya kufanya maamuzi make chini mkubaliane lipi mfanye au lipi mliache kwanza. Kwa kufanya hivyo mtakuwa na mahusiano mazuri maana mmeshirikishana kwenye maamuzi juu ya mashauri mliyopata.                             

Ni hatari sana ukapigiwa simu na mama au baba au mjomba wako kwamba mwanangu kuna kiwanja huku Mwabepande wewe kwa vile ulikuwa na hela Bank ukaikimbizia huko ukanunua bila kumuambia mwenzako, halafu baadae ajue kwamba umemruka katika maamuzi . Mshirikishe maana ndio unategemea kuishi naye anaweza kukupa ushauri mzuri ambao utaweza kupata kitu kizuri na cha thamani na saa nyingine kukuepusha na hasara.