GET YOUR COPY NOW
Philipian 4:4
Philipian 4:4 "Rejoice in the Lord always. I will say it again: Rejoice!"
Wednesday, October 15, 2014
Uchumba hadi Ndoa: Do you want your Spouse to change
Wengi wanataka kuona madadiliko kwa wenzi wao lakini hawako tayari kubadilika kwanza, hebu mpendwa wangu chukua hatua ya kubadilika leo.
Utakapobadilika na mwenzi wako utashangaa anabadilika
Muombe Mungu akuonyeshe ni eneo gani unatakiwa kubadilika na ukabadilike leo
Hata kama unaona hiyo tabia ni ngumu, mkabidhi Mungu yeye anaweza yote hakuna jambo gumu asiloliweza.
Mungu atusaidie na akakusaidie pia, Amen
Thursday, October 9, 2014
City Harvest welcomes you to Couples Seminar
You are all invited to Couples Seminar which will be held at City Harvest
Venue: Victoria Service Station Building, 2nd Floor along Mandela Road
Venue: Victoria Service Station Building, 2nd Floor along Mandela Road
Time: 9:30 to 5pm
Contribution: 5,000/=
per person for bites and logistics
Successful Couples
will make a Successful Family which will make Successful Society hence having Successful
Nation
You are Warmly Welcome
Thursday, October 2, 2014
Welcome to End of Month Fellowship with Dar es Salaam Workers Christian Fellowships (DWCFs)
Here comes another colourful Thursday, once
in a month, where all Dar es Salaam Workers Christian Fellowships (DWCFs)
gether together under one roof in the wings of the Al-mighty.
It is JB Belmonte Hotel again
with Pastor Mastai again, and praise and worship team from FPCT
at 17:00 hours onwards!
The ivitation is free to anyone, and there
is no entry fee or qualification. Come meet Jesus!
For more info see attached flyer.
You are warmly welcome J
Friday, September 5, 2014
Semina ya Siku tatu (3) ya Kufunguliwa kwa Mwanamke mjini Moshi na Pastor Neema Shoo
The Woman of Value iliyo chini ya Mchungaji Neema Shoo ( MTBC Moshi) inakuletea Semina ya Siku tatu ya Wanawake, Mabinti na Wamama kwa siku 3.
Semina itafanyika kuanzia Ijumaa tarehe 10 saa 9 Mchana hadi 12 Jioni
Jumamosi tarehe 11 saa 4 asubuhi hadi saa 10 Jioni
Jumapili tarehe 12 saa 10 jioni hadi 12 jioni
Semina Itafanyika Katika Ukumbi wa Hindu Mandal Moshi Stand
Katika Semina hiyo watumishi mbalimbali watahudumu Pastor Neema Shoo, Bishop Mary Lutumba-DSM, Prophet Essien Godwin SImon-Ghana na Pastor Dickson Mtalitinya- Moshi.
Upendo Kilahiro and MTBC Moshi watatuongoza katika sifa na kuabudu
Wagonjwa na wenye shida mbalimbali wataombewa
Wanawake wa Kilimanjaro , Arusha na kote Tanzania hii Semina siyo ya kukosa mwambie na mwingine
Tuesday, August 26, 2014
Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama na Ubora wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa -III na Mwalimu Samwel Mkumbo
Karibu atika mifululizo yote ya somo hili kutoka mwanzo mpaka sasa
imekuwa ni suala la kuangalia ni kwa jinsi gani nafsi zetu zinahusika sana
katika Uhai wa Kanisa. Sehemu ya mwisho nitasema nawe kwa kifupi sana kuhusu
Uhusiano wa nafsi ya Kanisa.
Karibu tujifunze pamoja…..
Luka 12:15 inasema hivi;
Akawaambia, Angalieni,
jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo
navyo.
Ni heri kila mmoja akahakikisha ya kwamba Nafsi yake iko na
furaha kila wakati, kwa ajili ya uhai wa kanisa lako, lakini pia kwa ajili ya
uhai wa nyumba yako kama msingi wa kanisa, kwa ajili ya ofisi yako, kwa ajili
ya ukoo wako.
Lakini pia ni vema kila mmoja akahakikisha anafanya bidii kumfurahisha
mwingine na kuifanya nafsi ya mwingine isiwe na jeraha hata moja, kuifanya
nafsi ya mwingine isitende dhambi, kila mmoja acheze karibu na mwenzake, kama
kucheza basi tucheze peke yetu, hakikisha unamlinda mwenzake asipate shida wala
asipotee.
1 Wakorintho 8:12 tunasoma hivi;
Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri
iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo
Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama na
Ubora wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa
Sasa labda tutazame kwa nafasi nyingine uhusiano wa Nafsi
yako ikiwa na Usalama na ubora wa nafsi yako na Uhai wa Kanisa ikiwa ni la
nyumbani au ni mahali unapoabudu au ofisini kwako au hata shuleni kwako
unakosoma.
Labda niweke jambo hili la msingi, tunapozungumzia kanisa ni
lazima tukajua ya kwamba si suala la dhehebu moja tu au suala la watu wanaosali
kwa pamoja lakini suala la Kanisa ni jambo linalohusu watu wote waliookoka na
wanaomkubali BWANA YESU kuwa ni mwokozi wa maisha yao na Mfalme wa Ulimwengu
wote.
Sasa kuna shida ambayo ni muhimu tukaishughulikia vizuri
kidogo ili tusipate shida tunapoangalia utekelezaji wa Somo hili, na jambo
lenyewe ni lazima akili zetu na fahamu zetu zifunguke tukajua mambo kadhaa ili
tuone Umuhimu wa kuona Nafsi ya kila mmoja inakuwa salama na bora ili Kanisa
liweze kuwa Hai.
1 Wakorintho 3:16-17 tunasoma hivi;
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa
Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu
atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
Sasa kuna jambo la msingi hapo natamani tulitazame kwa
makini sana sana, maana kama tusipolitazama kwa makini tunaweza tusielewe
vizuri, na hilo jambo linatuonesha Uhusiano uliopo kati ya Usalama na Ubora wa
Nafsi yako inavyohusiana na Uhai wa Kanisa la Tanzania, Kanisa la Ulimwengu
mzima lakini pia kuanzia na Kanisa la Nyumbani kwako na mahali unapoabudu.
Basi tuutazame huo mstari kwa makini sana sana, kuna maneno
kadhaa ya huo mstari natamani tuyatazame kwa makini …..Hamjui ya kuwa NINYI
mmekuwa hekalu la Mungu….. na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani YENU?.......
Kama MTU akiliharibu hekalu la Mungu,… Mungu atamharibu MTU huyo….. Kwa maana
hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo NINYI.
Maneno niliyoyaweka kwa herufi kubwa yana maana kubwa sana,
Paulo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu anawaandikia Wakorintho akitaka kuwaonesha ni
jinsi gani Uhusiano wa Kanisa unavyotengenezwa na unavyotegemea mtu mmoja
mmoja. Anapozungumzia Hekalu la Mungu anasema ni NINYI au ndilo SISI kama
tukijiweka kwenye nafasi ya Wakorintho na ambayo ni nafasi muhimu lazima
tujiweke hapo ili hiyo nafasi tuichukue kwa Umuhimu mkubwa sana.
Jambo amabalo ni la kulitazama kwa makini kwenye mistari
hiyo ni kwamba inapozungumziwa kanisa basi tunatazama kama Muunganiko wa watu,.
Maana HEKALU LA MUNGU (moja) linajengwa na NINYI (wengi), lakini pia
inawezekana hilo Hekalu la Mungu ambalo ni watu wengi likaharibiwa na MTU yaani
mmoja. Sasa basi kuna jambo la kulitazama tena hapo kwa makini Zaidi, kwamba kama
Hekalu la Mungu linalojengwa na SISI linaweza kuharibu na YULE au WEWE basi pia
linaweza kujengwa na WEWE- Nitalielezea hilo baadae kwa undani.
Wednesday, August 6, 2014
Uchumba hadi Ndoa: Usifikiri utaweza kubadilisha tabia ya mwenzi wako baada ya kuolewa naye au Kumuoa
Bwana
Asifiwe watu wazuri wa Mungu, namshukuru Mungu kwa siku hii nzuri aliyonipa
maana kwakweli muda nao umekuwa mali.
Natamani
sana kila wiki niendeleze Makala haya lakini mara nyingine tunabanwa na muda
lakini pia Mungu ana makusudi kwa kila jambo.
Leo
naomba tuzungumze jambo hili muhimu sana katika mahusiano, linalohusu pale mtu
anapokuwa na matarajio kwamba mwenzi wake atakuja kubadilika tabia yake mbaya
au isiyombariki baada ya kuingia kwenye Ndoa
Hii
inakuwa hivi inawezekana watu wamekaa katika uchumba wanavyoendelea kuna tabia
unaziona kwa mwenzi wako ambazo unaona kwamba ni ngumu yaani hazibebeki, lakini
unaamua kwamba utaendelea maana unajua kwamba ukimuoa au akikuoa utakuwa na Mamlaka ya Kuweza Kumbadilisha au
Kukomesha hiyo tabia.
Sisemi
kwamba watu wenye udhaifu fulani hawawezi kubadilika,HAPANA mtu yoyote yule anaweza kubadilika ila Mabadiliko yatatokea tu
pale mtu ANAAMUA kubadilika na sio kung`ang`anizwa kubadilishwa.
Hakuna
aina ya ubabe ambao wewe mke au mume unaweza kutumiakwenye Ndoa ili kubadilisha
tabia yake, sio pesa, sio chochote kitakachoweza kubadilisha mtu
Unaweza
kuwa na mchumba ambaye ana mahusiano mengi mengi, leo umemkuta na meseji za
Joyce, Kesho za Jane,mara umesikia jana alikuwa na mwingine sijui KFC au Steers
pale, wengine tena wanakutumia labda meseji za kejeli au wengine wanakupigia
simu kwamba huyo ni cha Wote, lakini wewe unang`ang`na kwamba eti huyu mtu
wangu atabadilika pale tu Nitakapomuoa….
Kuna
kisa nilikisikia hivi karibuni kaka alikuwa mchumba, kumbe huyo dada alikuwa
anaendeleza mahusiano ya zamani kisirisiri, sasa kibaya sana siku mbili kabla
ya harusi kuna mtu alimuona huyu mwanadada akiwa ametoka kwa yule mtu wake wa
zamani, huyu kaka aliambiwa lakini akasema huyo mimi nikimuoa nitamkomesha
hataweza kutoka hata ndani nitamfungia, NITAMBADILISHA.
Je
Ndugu yangu unafikiri kweli kwa tabia hii huyo dada yetu ataacha mahusiano hayo,
kama kweli anashindwa kuheshimu ndoa yake kabla hajaingia maana hapo hata huyo
mume hajamjua vizuri je akishaishi naye kweli ndio ataiheshimu hiyo Ndoa. Hebu
tafakari hili mpendwa wangu....
Neno
katika Mathayo 6: 24“Hakuna mtu awezaye
kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au
ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na
mali pamoja.”
Ukisoma
Maneno ya Mungu hapo juu neno liko wazi Kabisa kwamba mtu huwezi kutumikia
mabwana wawili yaani huwezi kushika mambo mawili lazima kuna moja utalidharau
na kuzingatia lingine.
Tuesday, August 5, 2014
USALAMA NA UBORA WA NAFSI YAKO UNAVYOHUSIANA NA UHAI WA KANISA na Mwl Samwel Mkumbo -Sehemu ya Kwanza
Karibuni katika makala haya yanayoletwa kwani na Mwalimu Samwel Mkumbo
![]() |
| Mwalimu Samwel Mkumbo |
Uhai wa kitu
chochote kile unategemea namna au jinsi mwenye huo uhai au aliyekabidhiwa
dhamana yuko katika hali gani, unaweza kulaumu juu ya uharibifu wa jambo au
mambo Fulani lakini kabla ya kulaumu angalia kwanza yeye aliyeharibu au
aliyekabidhiwa mikononi mwake yuko katika hali gani.
MATENDO
20:28 inasema hivi;
Jitunzeni
nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa
waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu
yake mwenyewe.
Sasa kabla
sijaendelea Zaidi nataka niseme jambo la msingi sana hapa, kichwa cha Somo letu
kinatuhitaji tuwe na ufahamu wa kuhakikisha kwamba kila tunachokiongea katika
somo hili ni mambo makubwa mawili, NAFSI YAKO NA KANISA LAKO. Wewe ni nafsi
moja katika kanisa, Je unayo kazi gani wewe kama Nafsi?
Unaweza
usijue wala usiliangalie kwa uzito, lakini inapasa kuelewa tafsiri hii;
KANISA ni Nafsi za watu zilizounganishwa
kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani wameijenga katika msingi wa
YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi zilizokubaliana za watu wengi wa aina
mbalimbali si kanisa maana ili wawe kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia
mamoja na kuwa na Imani moja ambayo hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.
TAZAMA
NAMI:
Ili kanisa
liwe na Nguvu na likae katika mstari unaotakiwa ni lazima nafsi za watu ndani
ya Kanisa ziwe ziko salama kabisa, yaani ziwe zimetunzwa katika hali ambayo
uhakika wa kundi kuishi kwa Amani utakuwepo kwa uhakika.
Labda
tuunganishe vipande viwili vya huo mstari wetu wa msingi ili uone jambo la
msingi kidogo….. Jitunzeni nafsi zenu,,.,.. mpate kulilisha kanisa lake
Mungu,.,.,..
Mfano wa
Mtumwa Mwaminifu
Bwana
akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana
wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri
mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia,
atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake,
Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake,
akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na
saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na
wasioamini (LUKA
12:42-46)
Sasa hapo ninataka nikufundishe jambo ambalo kimsingi
ambalo halipo kwenye Mistari hiyo hapo juu, na lenyewe ni juu ya adhabu
aliyopewa huyo wakili. Ona mtari huu;,..,.. akaanza kuwapiga wajoli wake,
wanaume kwa wanawake, AKILA NA KUNYWA NA KULEWA;,.,….
Maana suala
sio kusema bwana wake anachelewa ila baada kuona bwana wake anachelewa alifanya
nini? Na wala sio kuwapiga watumwa ila baada ya kuwapiga watumwa alifanya nini?
Yeye alichokifanya ni KULA NA KUNYWA NA KULEWA,..,..
Biblia
inaposema yeye ALIKULA NA KUNYWA NA KULEWA, maana yake aliacha kufanya
alichotakiwa kufanya lakini pia aliiharibu nafsi yake kwa MVINYO yaani kwa
Ulevi. Maana suala si kula na kunywa kwa sababu hayo ni mahitaji ya mwili wa
kila mtu, lakini suala ni KULEWA na biblia inasema KILEO HUDHIHAKI,. Na pia
HUPOTOA HUKUMU ZA HAKI.
Subscribe to:
Posts (Atom)





