UNAPITIA KIPINDI GANI KATIKA MAISHA YAKO???
TAMBUA JINSI YA KUISHINDA SAA YA MAMLAKA YA GIZA!
Hakuna mwanadamu asiyepitia kipindi hiki, usipoishinda saa hii itakushinda!
Usipoiharibu itakuharibu Luka 22:52-53. Mamlaka hii ya giza inaweza kujifunua
kazini, kwenye jamii/familia-nyumbani hata katika huduma au katika nchi.
Ninamaanisha nini nikisema saa ya mamlaka ya giza? Ni wakati unapopitia
kipindi kigumu maishani kiasi cha kutamani kujikimbia/ kujiua au kukataa tamaa
na wale uliowategemea wakakukimbia na kukaa mbali na wakati huo unaweza kuona
pia Mungu amekuacha kwani atakaa kimya ili kuipima imani yako je unamwangalia
yeye au tatizo.
Mamlaka hii ina majira yake na ndio maana inaitwa saa ya mamlaka ya
giza.Inatumika na mtu au watu. Pia inatabia ya kukutenga na watu ili ikupate na
ikumalize kwani hata uliowategemea watakaa pembeni. Ila lazima ujue hata kama
wote watakimbia lazima Simon wa Kirene atokee atakuja mtu usiyemtegemea
atakayeletwa na Mungu. Mfano halisi wakati ule wa Yesu , Saa ya mamlaka ya giza
ilipofika kwa Yesu aliitambua. Petro alikaa pembeni akasema simfahamu mtu huyu,
Yuda alimsaliti. Pia wale Mitume waliposhindwa kuomba Mungu aligusa watu, kuna
wakina mama waliokuwa wakilia na kuomboleza, walimfuata Yesu na kumywesha maji.
Kumbuka saa hiyo ni saa ya kudhalilishwa, ni saa ya matusi. Kutakuwa na
kusalitiwa unaweza kugeukwa na mtu uliyemtegemea sana,anaweza kuwa ndugu, mke,
mume, mtoto, mzazi, rafiki,mpendwa hata mtumishi mwenzako n.k. Saa hiyo ikifika
watasema unajifanya unajua kuomba na kuombea watu, watasema eti anajidai Mungu
anamtumia embu fanya muujiza tuone. Watakukejeli. Watasema anajifanya ana
uwezo, ni mzuri sana maneno kama hayo hayakosekani. Saa hii ilipotokea kwa
Yusuph mpaka ndugu walimuuza lakini aliposimama na Mungu alifanikiwa na utukufu
wa Mungu ukamfunika. Shetani alimletea majaribu mengi ili amuangushe lakini
alijitambua akamshinda.Hakuna taji ya utukufu pasipo taji ya mwiba! Yusuph
alipitia mateso mengi sana lakini alipoweka tumaini lake kwa Bwana alishinda.