Habari ya leo mpendwa wangu, Karibu sana katika
Makala haya ya Uchumba hadi Ndoa yanayoletwa kwako na Mshauri wako kila wiki.
Leo tutazungumzia kipengele muhimu cha Kujihadhari
na matarajio potofu kuhusu Ndoa, au yaliyojengwa kuhusu Ndoa.
Matarajio potofu ni ile hali ya kuamini kwamba kuna
vitu fulani vitatokea au vitakuwa hivi halafu wala havitatokea na wala haviko
hivyo unavyotarajia.
Matarajio potofu kuhusu ndoa yako sana katika jamii
zetu sio za Kiafrika tu hata mabara ya Ulaya, yako katika jamii za dini
mbalimbali, kabila na mila mbalimbali
Najua hata wewe kuna matarajio potofu kuhusu Ndoa
ambayo utakuwa umeyaamini kwasababu ulizaliwa katika jamii ambayo yaligeuka
kuwa sehemu ya hiyo jamii.
Katika jamii zetu na mazingira yanayotuzunguka
matarajio potofu yanaweza kuwa na sehemu kubwa inayofanya Ndoa nyingi ziwe
katika shida ambazo zimekuwa nazo leo.
Kitu kibaya ni kwamba hata sisi Wakristo
tumeyaamini na tunayakiri maratajio hayo matarijio potofu, ndio maana leo
nimekuja kukuambia kwamba hayo ni potofu labda ulikuwa hujui.
Tuangalie Aina Tano za Matarajio Potofu kuhusu Ndoa;
1. Ndoa Ndoano au Ndoa si Lelemama
Mara nyingi kwenye sherehe mbalimbali za Harusi
utakuta pande mbili ya Bibi Harusi na Bwana Harusi wanapewa nafasi ya kutoa
nasaha sasa hapo ndio utasikia haya maneno yakisemwa katika nasaha na tena cha kushangaza utakuta watu ukumbini
wananapiga makofi.
Sasa wewe mzazi au mlezi mwenzangu unaposubiri ile sherehe
pale ndio uje kumwambia mtoto Ndoa si Lelemama au Ndoa ni Ndoano kwanini
umechelewa si ungemkataza au ungekataa mahari jamani, Ili basi kumuepusha na hiyo lelemama unafikiri ipo.
Maana kwa kusema pale ina maana unakiri kabisa kwa
mdomo wako Mwanangu Ndoa Ndoano au si Lelemama kwahiyo ukavumilie, pale unamfanya
huyo mratajiwa awe na hofu kubwa kwahiyo atakaa kimtegomtego ili tu akiona tu
kaugomvi kidogo anakumbukaa anhaa hii ndio ileee lelemama niliambiwa na baba au
mama siku ile pale Kibada Skyline Hall…Ohh mwisho wa siku anaanza tu kuhesabu
makosa siku anakurudia na mizigo ooh Baba na Mama ile Lelemama yangu anhaa
hukuwahi kuiona imekuwa lelemama kwelikweli Nimeshindwa na Nimerudi, Utajibu
nini mzazi mwenzangu au mlezi mwenzangu.
Haimaanishi kwamba kama wewe mzazi au mlezi ulipata shida katika
Ndoa yako na mtoto wako lazima apitie ulichopita, hata kidogo , na jaribu
ulilopitia je umetafuta Kusudi maana nimejifunza kila Jaribu ulilopitia katika
maisha lina kusudi sasa kwasababu tunashikilia sana Uchungu inakuwa Ngumu
kuliona Lile Kusudi ambalo ndilo hasa Mungu anataka tulifanye, Haleluyaaaaaaaaa
Sasa na wewe kijana au binti haya na wewe hata
hujaolewa unaanza kukaa barazani ooh unajua Bwana wanaume siku hizi wasanii tuu
Ndoa hamna, hakuna zote Ndoa Ndoano, unajua kinachotokea katika Ulimwengu wa
Roho, tusome pamoja Mithali 18: 21 “Mauti
na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”
Haya kijana na Binti yangu umeona Maneno ya Mungu
yanavyosema,kuwa makini unaongea nini wewe ni mtoto wa Mfalme wa Wafalme
usiishi kama watu wa mataifa ambao hawana Tumaini,badili Maneno ya Kinywa chako
leo, Sema mimi ndoa yangu itakuwa nzuri itabariki watu, itasimama kama Ushuhuda
na utapata hicho unachokisema.Aminaaaaaa