GET YOUR COPY NOW
Philipian 4:4
Philipian 4:4 "Rejoice in the Lord always. I will say it again: Rejoice!"
Showing posts with label Muziki wa Injili. Show all posts
Showing posts with label Muziki wa Injili. Show all posts
Thursday, April 6, 2017
Tuesday, January 10, 2017
MWIMBAJI WA WIKI - JOSHUA SILOMBA
LEO TUKO NA MCHUNGAJI JOSHUA SILOMBA
| Mchungaji Joshua Silomba |
Rejoice
Blog: Labda tuanze kwa kujua majina yako kamili na ikiwa unatumia
jina tofauti kwenye kazi zako za muziki?
Joshua
Silomba: Naitwa Joshua Silomba wakati mwingine huwa naitwa Pastor
Joshua kutokana na huduma yangu ya kichungaji.
Rejoice
Blog: Je, umeokoka? Unaabudu katika kanisa gani?
Joshua
Silomba: Nimeokoka, ninaabudu kanisa la T.A.G Toangoma na pia ninatumika
kama Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo (Mchungaji wa Vijana/Sifa na Kuabudu).
Rejoice Blog: Historia yako kwa kifupi ya kuimba, yaani ulianzaje na wapi
ulianzia?
Joshua Silomba: Nakumbuka nilianza kuimba nikiwa mtoto kabisa kule nyumbani
Vwawa, Mbozi. Baba yangu alikuwa Mchungaji na familia kwa ujumla ni ya Kikristo
hivyo muda mwingi tulikuwa tukiimba nyumbani na kanisani pia hasa kwenye Sunday
School. Nilikigundua zaidi kipaji changu cha kuimba nilipoanza kusoma Shule ya
Sekondari miaka ya 2000, nilipofika kidato cha pili niliendelea zaidi kugundua uwezo
wangu wa kuongoza ibada (kuimbisha), kupiga muziki na pia kutunga nyimbo. Mwaka
2003 nilikabidhiwa rasmi jukumu la kufundisha kwaya ya kanisa la TAG Mji Mkuu nikiwa
Morogoro na tangu hapo nimeendelea kumtumikia Mungu katika maeneo yote niliyoyataja
hapo juu (Kuongoza ibada, kupiga muziki, kutunga nyimbo zangu binafsi na kwaya na
pia kufundisha kwaya na timu za kusifu na kuabudu).
| Joshua akiiongoza ibada na sifa kanisani |
Rejoice Blog: Katika kuimba kwako, je, umeshatoa albumu yoyote? Majina ya
albamu?
Joshua Silomba: Nimewahi kutoa albumu mwaka 2010 iliyoitwa MUNGU WETU
HASHINDWI (audio) na kwa sasa nina albumu nyinginei itwayo JAMBO JIPYA (audio) ambayo
niliitoa rasmi tarehe 04.12.2016.
Rejoice Blog: Wimbo unaoupenda zaidi kati ya nyimbo zako ni upi?
Joshua Silomba: Kwa kweli napenda nyimbo zangu zote kwa kuwa kila wimbo umebeba
ujumbe maalumu na pia sababu maalumu ya kutungwa kwake. Hivyo, kila wimbo una
mguso wa kipekee napozisikiliza na kuziimba pia.
Rejoice Blog: Nani anasambaza na kusimamia kazi zako? Na je,
anakusaidia vizuri?
Joshua Silomba: Kwa sasa sina msambazaji wala mtu anayesimamia kazi zangu,
labda kwa hapo baadaye.
Rejoice Blog: Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia na unapenda
kufuatilia kazi zake?
Joshua Silomba: Kwa Tanzania ni
wengi wanaonivutia katika muziki wa Injili hususani wanaoimba nyimbo za sifa na
ibada. Kwa nje ya nchi kwa sas anapenda sana kumsikiliza na kumfuatilia William
McDowell.
Rejoice Blog: Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba nyimbo za Injili?
Joshua Silomba: Mafanikio ninayoyaona kwa sasa ni kupanuliwa zaidi kwa wigo
wa kihuduma, watu wengi zaidi wanaendelea kunifahamu na kufuatilia ninachofanya
katika huduma yangu. Pia naendelea kuwafahamu na kukutana na wadau mbalimbali wa
muziki wa Injili kama vile wazalisha muziki (producers), waongoza video (video
directors) na waimbaji ambao wananipa changamoto ya kufanya kazi katika ubora na
viwango vya hali ya juu.
Rejoice Blog: Umekutana na changamoto gani katika huduma yako ya
uimbaji?
Joshua Silomba: Changamoto ni nyingi ila kwa uchache, nimepata sana
changamoto ya kifedha katika kufanikisha malengo yangu ya kihuduma hivyo kufanya
kazi zisizona viwango ninavyovitaka, ucheleweshwaji wa kazi studio au kupoteza kabisa
(nimewahi kurekodi nyimbo ambazo hadi sasa sijazipata kwa miaka zaidi ya
miwili, pia nimewahi kurekodi video ambazo sijawahi kuziona pasipo maelezo yanayojitosheleza).
Changamoto nyingine ni kutopata ushirikiano kwa waimbaji wengi waliotangulia kwenye
huduma hii ya uimbaji na mwisho, mfumo wa vyombo vya habari wa Tanzania (Redio,
TV, nk) hautii sana moyo hasa kwa waimbaji wanaoanza huduma hivyo ziko nyakati ambazo
nilikatishwa sana tamaa na mfumo huu.
Rejoice Blog: Unaonaje muziki wa Injili hapa Tanzania? Na hasa wa aina
unayoimba wewe?
Joshua Silomba: Muziki wa Injili Tanzania unazidi kukua na changamoto inazidi
kuwa kubwa hasa kwa upande wa ubora na viwango. Lakini pia kwa upande mwingine,
muziki wetu umeingiliwa sana na mamluki, hivyo kusababisha waimbaji wengi hata wasio
na shida kuonekana ni wababaishaji.
Rejoice Blog: Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili ambao
kwa njia moja ama nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii?
Joshua Silomba: Nashauri waimbaji wanaojisahau na kujichanganya na mambo
ya kidunia wajitambue na kurejea kwenye misingi ya Neno la Mungu ambalo linatuongoza
kupita katika njia za haki na utakatifu. Zaidi wanatakiwa kutubu na kusimama kwenye
kweli ili utumishi wao usiwe bure.
Rejoice Blog: Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unakifanya?
Joshua Silomba: Kama nilivyosema hapo awali, mimi ni Mchungaji Msaidizi wa
Kanisa la TAG Toangoma na nina wajibika zaidi kama Mchungaji wa Vijana na Sifa na
Kuabudu (Youth/Worship Pastor). Najishughulisha pia na kilimo, ufugaji na biashara.
Pia ni MC kwenye shughuli mbalimbali za kijamii na kikanisa.
Rejoice
Blog: Je, kimaisha uko wapi? Ndoa na watoto vipi?
Joshua Silomba: Ninaishi Toangoma, Dar Es Salaam. Nina mke (Bertha) na mtoto
mmoja (Doreen).
Rejoice Blog: Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa
Tanzania?
Joshua Silomba: Tupendane, tuwe na umoja na pia tuishi maisha halisi ambayo
yatamtukuza Mungu.
Rejoice Blog: Na kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za Injili
una ujumbe gani kwao?
Joshua Silomba: Waendelee kututia moyo na kutupa ushirikiano tunapotoa nyimbo.
Rejoice Blog: Ahsante sana Joshua Silomba kwa muda wako, Mungu akubariki
na kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu
Joshua Silomba: Amina! Nawashukuru pia Rejoice Blog kwa kazi nzuri mnayoifanya
ya kuibua na kutangaza vipaji vya waimbaji wa nyimbo za Injili. Mungu awainue zaidi
ili muwafikie watu wengi.

Kupata zaidi habari za huduma yangu kwa sasa natumia Facebook, page yangu natumia
jina Joshua Silomba. Msomaji anaweza ku-like na ku-share na wengine ili waweze kujua
habari mbalimbali zinazohusu huduma yangu. Pia YouTube kwa sasa nimeweka wimbo
(audio) unaoitwa Jambo Jipya wanaweza
kuusikiliza kwa kubofya link HAPA
Mawasilianoi zaidi piga: +255717387212/+255754773512
Mwisho kabisa napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa msomaji kutoa muda
wake kufuatilia habari za muziki wa Injili kupitia Rejoice Blog.
~~~
UBARIKIWE ~~~
Labels:
Gospel Music,
Joshua Silomba,
Msanii wa Wiki,
Muziki wa Injili
Monday, January 2, 2017
ALBUM YA NENO IKO NJIANI
Mwanamuziki wa Injili, Frida Felix yuko njiani kutuletea albamu yake inayokwenda kwa jina la "NENO" Kaa tayari kuipokea!
Kwa habari na kufahamu zaidi kuhusu Frida Felix, unaweza kusoma makala ya Msanii wa Wiki hapa ambapo blog hii ilifanya mahojiano naye
Tuesday, December 20, 2016
MSANII WA WIKI - SIXBERT MUBILIGI
NDANI YA MSANII WA WIKI HII....
![]() |
| Sixbert Mubiligi |
Rejoice Blog: Tuanze
kwa kujua majina yako kamili na ikiwa unatumia jina tofauti kwenye kazi zako za
muziki?
Sixbert: Majina
yangu ni Sixbert Eldard Mubiligi, kwenye huduma natumia zaidi Sixbert Mubiligi.
Rejoice Blog: Je,
umeokoka? Unaabudu katika kanisa gani?
Sixbert: Mimi
nimeokoka kweli kweli; ninaabudu kanisa la TAG - nikiwa Morogoro kwangu
ninaabudu TAG Bethel Mwembesongo linaloongozwa na Askofu Mkuu Barnabas Mtokambali.
Nikiwa Mtwara naabudu kanisa la TAG Shangani Miracle Temple chini ya Askofu
George Musa.
![]() |
| Sixbert Mubiligi katika moja ya Mikutano ya Injili |
Rejoice Blog:
Historia yako kwa kifupi ya kuimba, ulianzaje na wapi ulianzia?
Sixbert: Nimeanza
tangu nikiwa mdogo Sunday School Basanza Uvinza Kigoma, na nilipofika umri
wa kutosha kuimba na watu wazima niliimba kwaya ya kwanza ya Neema iliyopo Basanza
Uvinza, ni kwaya ya kanisa la Anglican. Baadaye nikaja Urambo Tabora na
nikaimba kwaya ya ESSACU pale wilayani Urambo. Nilipokuja kwa baba yangu Morogoro
nimeimba kwaya ya Safina pale Anglican Magereza Kihonda. Baadae nilipoanza
kidato cha kwanza ndipo nilipokutana na wapendwa tukatengeneza bendi iliyoitwa
SGS hapo ndipo ulikuwa mwanzo wa kuingia studio hapo ilikuwa 2005 nikiwa kidato
cha tatu na tulifanya kazi kama Maisha bora
Rejoice Blog: Safi
sana. Una historia ndefu kwa kweli katika muziki wa Injili. Katika kuimba
kwako, je, umeshatoa album yoyote?
Sixbert: Yesu
umenipa Heshima na mwaka 2009 nikiwa kidato cha Sita nilifanikiwa
kurekodi albamu yangu iliyoitwa BWANA ATASIMAMA.
Na sasa ninaandaa albamu mpya iitwayo YESU HASHINDWI na albamu ya pamoja kati yangu na rafiki yangu ambae tumeanza nae huduma hii tangu tukiwa sekondari, anaitwa ALFRED MWAKASASA.
Na sasa ninaandaa albamu mpya iitwayo YESU HASHINDWI na albamu ya pamoja kati yangu na rafiki yangu ambae tumeanza nae huduma hii tangu tukiwa sekondari, anaitwa ALFRED MWAKASASA.
![]() |
| Sixbert akiwa na mwimbaji Joshua Silomba |
Rejoice Blog:
Nani anasambaza na kusimamia kazi zako?
Sixbert: Kazi
zangu nasambaza mwenyewe sijapeleka kwa wasambazaji, lakini hizi kazi mbili
itabidi nitafute msambazaji. Kwa upande wa usimamizi bado natafuta mtu
atakayesimamia au hata kampuni ambayo nitafanya nayo kazi.
Rejoice Blog:
Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia na unapenda kufuatilia kazi
zake?
Sixbert: Mwimbaji
ninavutiwa naya ni Ambwene Mwasongwe na huwa nasikia tu kumfuatilia kazi zake.
Kwa kifupi ndiye Fanuel Sedekia wa wakati huu maana anayatunza mafuta ya
madhabahu katika uimbaji
Rejoice Blog:
Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba nyimbo za Injili?
Sixbert: Mafanikio
ni mengi cha kwanza uimbaji umenipa digrii Udom na mengine mengi maana
kumtumikia Mungu kuna faida, lakini kubwa zaidi nimepata watu wengi sana ambao
ni wa familia ya Yesu Kristo
![]() |
| Sixbert akiwa na waimbaji wengine studio |
Rejoice Blog:
Umekutana na changamoto gani katika huduma yako ya uimbaji?
Sixbert: Waoh!
Changamoto kubwa ni fedha ambapo huduma hii inahitaji pesa kuliko vile watu
wanavyofikiria. Changamoto nyingine ni baadhi ya watumishi utakuta anakuita
kwenye huduma wewe binafsi alikuambia mtumishi hali ni ngumu lakini ukifika
kwenye mkutano au semina unakutana na muimbaji kutoka Dar ambae anaondoka na bahasha
ya laki saba wewe hata mafuta ya gari hupati. Hii kwangu huwa inaumiza hata
ungekuwa wewe mwandishi ungeumia
Rejoice Blog:
Unaonaje muziki wa Injili hapa Tanzania? Na hasa wa aina unayoimba wewe?
Sixbert: Muziki
wa tanzania unakuwa kila siku, na tasnia inang'aa kwa kweli
Rejoice Blog:
Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili ambao kwa njia moja ama
nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii?
Sixbert: Kama
umeamua kumtumikia Mungu unatakiwa uwa halisi hapo Mungu atayaachilia mafuta
yake juu yako.
Rejoice Blog:
Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unakifanya?
Sixbert: Mbali
na huduma, mimi ni mwalimu wa sekondari Manispaa ya Mtwara pia mjasiriamali
![]() |
| Sixbert akiwa na mkewe Joyce |
Rejoice Blog:
Je, umeoa na una watoto?
Sixbert: Yeah
mimi ni mume wa mke mzuri Joyce Sixbert. Pia Bwana Yesu katuzawadia Mtoto wa kike
anayeitwa Prettyn.
Rejoice Blog:
Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania?
Sixbert: Niwaombe
watumishi ambao Bwana kawapa kibali cha kuonekana mbele za jamii jitahidini
kutamani kuwawezesha wengine ili familia ya wana wa Asafu ikue maana
binafsi napenda waimbaji waongezeke kila siku. Na pia tuache ukabila kwenye
huduma.
Rejoice Blog:
Na kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za Injili una ujumbe gani
kwao?
Sixbert: Ujumbe
wangu kwa jamii watusapoti, huduma hii inawahitaji wao ili isonge mbele. Amen
Rejoice Blog:
Ahsante sana Sixbert kwa muda wako, Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea
kumtumikia kwa uaminifu
Sixbert: Amen,
ahsante
Huyo ndiye Sixbert Mubiligi,
kijana aliyeanza kumtumikia Mungukwa muda mrefu kupitia uimbaji. Naamini
umepata kumfahamu zaidi kwa angalau hatua moja mbele
Kwa mawasiliano na Sixbert
kwa habari ya huduma unaweza kumpata kupitia namba 0716552795 au barua pepe mubiligis@yahoo.com
~~~ UBARIKIWE ~~~
Thursday, December 15, 2016
Thursday, December 8, 2016
Tuesday, December 6, 2016
S'fiso Ncwane Hatunaye Tena
Tasnia ya Muziki wa Injili imempoteza mwimbaji wa nyimbo za
Injili kutoka Afrika ya Kusini, S'fiso Ncwane. Taarifa kutoka Afrika ya Kusini zinasema S'fiso alifariki jana siku ya jumatatu asubuhi
kutokana na matatizo ya figo, ikiwa ni muda mfupi baada ya
kukimbizwa hospitali kutokana na kulalamika kujisikia kuumwa.
Ncwane ambaye alikuwa akihudumu kwenye tamasha Limpopo
wikiendi iliyopita alianza kulalamika kujisikia kuumwa na kisha
akakimbizwa hospitali mpaka pale umauti ulipomfika, ikiwa ni
taarifa kutoka kwa msemaji wa familia Sipho Makhabane.
Pamoja na kushiriki katika tamasha hilo huko Limpopo, S'fiso
hakuweza kumaliza kuhudumu baada ya kujisikia kuumwa na
kupelekwa hospitali ya Life Fourways
Chanzo: SA
Breaking News
ELANDRE - MSANII WA WIKI
LEO TUNAYE ELANDRE NA GOSPEL HIP-HOP
Leo katika Msanii wa Wiki
tuko wa Gospel Hip Hop ajulikanae kwa jina la ELANDRE. Ni muziki wa aina ya kipekee sana kwenye tasnia ya Muziki wa Injili
Tayari kuna baadhi
wanamfahamu kwa kazi zake na wengine hata wamehudumu naye pamoja katika huduma
mbalimbali.
Tumebahatika kupata
nafasi ya kumfahamu zaidi leo na kujua zaidi kuhusu huduma yake ya Muziki wa Injili
kwa namna ya kipekee na pia kuhusu maisha yake binafsi.
Rejoice Blog: Labda
tuanze kwa kujua majina yako kamili na ikiwa unatumia jina tofauti kwenye kazi
zako za muziki?
Elandre: Majina
yangu kamili ni Emmanuel Andrew Mkumbwa. Kwenye mziki ndo natumia jina Elandre.
Rejoice Blog: Je,
umeokoka? Unaabudu katika kanisa gani?
Elandre: Nimeokoka.
Na ninaabudu katika kanisa liitwalo Bread of Life ambalo lipo chini ya King’s
Touch Ministries. Mchungaji wangu anaitwa Fred Okello, na pia ninahudumu pale
kama kiongozi msaidizi wa sifa [kusifu na kuabudu].
Rejoice Blog:
Historia yako kwa kifupi ya kuimba, ulianzaje na wapi ulianzia?
Elandre: Nikiwa
kidato cha tano, tulikua na kikundi cha maombi ambapo tulikua tukishiriki kila
Jumamosi. Kuna siku mtumishi kutoka Uganda akaja akaibua vipawa vilivyokua
vimelala ndani yetu kwa neno la unabii. Haikuchukua mda nikaanza kuandika
mashairi, maana alitoa mfano hai kabisa wa hiki kipaji/kipawa na nlikua
nakipenda sana kitabu cha Zaburi. Ndipo nilipoitolea wimbo wangu wa kwanza uitwayo Praise The Lord [Psalm 150]. J
Rejoice Blog: Sawasawa. Katika kuimba kwako, je, umeshatoa album yoyote?
Elandre: Nimetoa
album moja inayoenda kwa jina PROJEKT THREE6TEEN inayopatikana pia mtandaoni kwenye soundcloud hapa na pia reverb nation hapa.
Rejoice Blog: Wimbo
unaoupenda zaidi kati ya nyimbo zako ni upi?
Elandre: "Elijah" ambao nimemshirikisha mwanadada kutoka Zambia aitwae Tasila Mwale.
Rejoice Blog:
Ni kwa sababu gani unaupenda wimbo huo zaidi?
Elandre: Wimbo
huu una miondoko ya ki-Afro pop ukichanganywa na rap. Nilitumia mda mfupi sana
kuundika na kwa uhai ulionao, huwagusa wengi wanaousikia na kuisikiliza meseji
iliyomo ndani. Nahisi pia naupenda kwa sababu unachezeka.
Rejoice Blog:
Nani anasambaza na kusimamia kazi zako? Na je, anakusaidia vizuri?
Elandre: Hamna
anayesambaza kazi zangu. Natafuta sana mtu atakaenisaidia kuifanya hii kazi.
Rejoice Blog:
Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia na unapenda kufuatilia kazi
zake?
Elandre: Lecrae
ambae ni msanii kutoka Marekani, nahisi ndio the most successful Christian
Rapper kwa sasa. Ana bidii sana katika kuifanya kazi ya Mungu kupitia kipaji
alichopewa.
Rejoice Blog: Kuna
mafanikio gani umeyapata katika kuimba nyimbo za Injili?
Elandre: Tangu
mwaka 2007 nilipotoa singo yangu ya kwanza mpaka sasa mafanikio nliyoyapata
katika kuimba nyimbo za injili ni pamoja na kutengeneza connections na wasanii
wengine kutoka nje ya Tanzania, baraka za afya tele na uhai, na mpaka sasa
tunaendelea vizuri. Najua mafanikio ya kifedha yanakuja hivi punde.
Rejoice Blog: Umekutana
na changamoto gani katika huduma yako ya uimbaji?
Elandre: Kupenya
katika hili soko letu la Tanzania ndo imekua ni changamoto kubwa sana kwangu,
pia kwa watenda kazi wenzangu tunaofanya nao muziki kama huu. Vyombo vya habari
haviukubali na kuuchukulia huu mziki kama fursa. Maana naamini kwamba sisi sio
wasanii tu, ni zaidi ya wasanii na miziki yetu ina uhai na nguvu za kiMungu maana
Mungu anaishi ndani yetu. Pia changamoto nyingine imekua kumpata msimamizi wa
kazi zangu, nimekua nikifanya karibia kila kitu peke yangu. Bado najifunza mengi
na nitaendelea mpaka kieleweke maana huwezi jua labda nimeitwa kua msimamizi wa
wengine wanaokuja nyuma yetu.
Rejoice Blog: Unaonaje
muziki wa Injili hapa Tanzania? Na hasa wa aina unayoimba wewe?
Elandre: Bado
tunakua. Bado njia haijawa wazi. Bado wasanii wengi hawajielewi na kwa sababu
hiyo huenenda katika njia za wasanii wengine wasio wakristo/wa nuruni. Kujitambua
kumekua ni changamoto kubwa sana, nahisi pia ni kwa sababu wengi hawajatulia na
kuketi chini ya mchungaji mmoja atakaekuza, na kukiendeleza kile kilichomo
ndani yao. Muziki huu bado unakua, kwa nionavyo mimi bado uko katika steji za
utotoni, unahitaji maziwa na malezi zaidi ili kukua. Lakini ukikua utaleta
mabadiliko makubwa sana katika miziki ya Injili hapa nchini.
Rejoice Blog:
Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili ambao kwa njia moja ama
nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii?
Elandre: Warudi
kundini. Mafanikio yako ndani ya Kristo Yesu pekee. Shida kubwa ni kutolitii Neno la Mungu, na kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu. Lakini tungekua waaminifu
katika hili, tusingetoka nje kwa nia ya kutafuta hela au maisha. Sisi ndo
tungekua tunafuatwa na waduniani kujua nini wafanye ili wafanikiwe.
Nimeji-include na mimi katika hili swala la uaminifu maana nahisi ndo “key
factor” katika hili suala.
Elandre: Tofauti
na mziki mimi ni Graphic Designer.
Rejoice Blog:
Je, kimaisha uko wapi? Ndoa na watoto vipi?
Elandre: Bado
bachela. Ndoa bado. Mungu akipenda mtasikia shangwe hivi karibuni. J
Rejoice Blog: Safi sana. Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania?
Elandre: Tuutafute
uso wa Mungu. Hapo ndipo mafanikio yalipo. Pia tupendane jamani, tuombeane badala
ya kupigana mawe. Sisi ni familia moja, inabidi dunia itutazame sisi kama mifano
hai. Hamna alie mkamilifu kwa hiyo tuinuane pale mmoja wetu anapoanguka.
Rejoice Blog: Na
kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za Injili una ujumbe gani kwao?
Elandre: Wazidi
kutuombea sana.
Rejoice Blog: Ahsante
sana Elandre kwa muda wako, Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea
kumtumikia kwa uaminifu
Elandre: Asante
sana hata kwa hii fursa mlinipa na kuniheshimu. Much love kwenu na nnawatakia
mafanikio makubwa katika mwaka ujao, muwe the top blog hapa Tanzania na chombo
chenu kizidi kukua mje kukamilisha ndoto zenu pia.
Rejoice Blog: Ameen
Unaweza kuwasiliana na kumpata Elandre kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, na pia kumwalika kuhudumu kwenye shughuli mbalimbali za kumtukuza na kumwinua Mungu... vilevile kushirikiana naye katika kukuza kazi za sanaa katika Injili hapa nchini na duniani kote
Elandre: Social media handle yangu ni @iamelandre yaani hii inatumika kote Facebook, Twitter, Instagram na Youtube [Ukitaka kuona video zangu]
www.reverbnation.com/iamelandre
Huo ndiyo mwanzo wa kufahamu zaidi kuhusu Elandre, kuna mengi mengine kuhusu kazi zake za Injili kupitia muziki wa HipHop na shughuli zake nyingine. Usikose kuendelea kufuatilia kipengele hiki cha Msanii wa Wiki kila wiki siku ya jumanne kupata kuwafahamu zaidi wasanii wanaomtukuza Mungu kupitia kazi mbalimbali za sanaa, hususani Muziki wa Injili hasa hapa nchini Tanzania.
Ikiwa unapenda tufanye mahojiano na Msanii fulani wa Injili hapa nchini Tanzania,au ikiwa wewe ni msanii wa muziki au sanaa yoyote katika Injli na ungependa kutambulisha zaidi kazi zako, basi usisite kuwasiliana nasi kwa njia ya simu (call, text, whatsapp) kupitia namba 0714484504 (Alex). Ubarikiwe sana!
~~~ TUKUTANE WIKI IJAYO! ~~~
Labels:
Elandre,
Gospel HipHop,
Gospel Music,
HipHope,
Msanii wa Wiki,
Muziki wa Injili,
Projekt316
Tuesday, November 29, 2016
MSANII WA WIKI - LEMBO JR
LEO KATIKA MSANII WA WIKI - EMMANUEL LEMBO JR
Rejoice Blog: Labda tuanze kwa kujua majina yako kamili na ikiwa
unatumia jina tofauti kwenye kazi zako za muziki?
Lembo Jr: Jina langu ni Emmanuel Stephen Lembo, ila katika huduma nafahamika
kama Lembo Junior
![]() |
| Lembo Jr |
Rejoice Blog: Je, umeokoka? Unaabudu katika kanisa gani?
Lembo Jr: Nimeokoka nampenda Yesu, kwa sasa naabudu NAIYOTH CHURCH
- GEITA
Rejoice Blog: Historia yako kwa kifupi ya kuimba, yaani ulianzaje na
wapi ulianzia?
Lembo Jr: Naweza sema,nilianzia utotoni sundayschool kids choir...ila
kuingia rasmi kwenye tasnia hii mpaka kuanza kusikika kwa medias ni 2007-2008
nikiwa UDOM
Rejoice Blog: Katika kuimba kwako, je, umeshatoa album yoyote? Majina
ya albamu?
Lembo Jr: Mpaka sasa niko na 4 albums ila tatu ndizo zajulikana
1.TUTEMBELEE. 2 USIFIE JANGWANI. 3.UWE KILA KITU. 4.WINGU LIMESIMAMA WAPI
Rejoice Blog: Wimbo unaoupenda zaidi kati ya nyimbo zako ni upi?
Lembo Jr: mmmmmmh ni almost nyimbo zote nazipenda maana kila wimbo
najua Mungu alinipaje ILA UWE KILA KITU, TUTEMBELEE NA USIFIE JANGWANI ni zaidi
![]() |
| Lembo Jr |
Rejoice Blog: Ni kwa sababu gani unaupenda wimbo huo zaidi?
Lembo Jr: Nyimbo zina ushuhuda mkubwa sana sikuzipewa hivi hivi, nilipitishwa
sana sanaaaaa
Rejoice Blog: Nani anasambaza na kusimamia kazi zako? Na je,
anakusaidia vizuri?
Lembo Jr: Kwa sasa niko na Madam Gisela Malisa, yuko vyema
Rejoice Blog: Ni msanii gani wa muziki wa Injili anayekuvutia na
unapenda kufuatilia kazi zake?
Lembo Jr: Sipho Makhabane, Emmanuel Mgogo
Rejoice Blog: Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba nyimbo za
Injili?
Lembo Jr: Yako mengi sana kiroho na kimwili. Kiroho; nimekua
nikipokea shuhuda nyingi sana namna nyimbo zangu zimeokoa, zimeponya na kuganga
NAFSI zilizokia zimejeruhiwa. Kimwili kuna kupata kipato ingawa si kikubwa,
ila MUNGU ni mwema. Na pia nimepata EXPOSURE kubwa sana ndani na nje ya mipaka
ya Afrika
![]() |
| Lembo Jr |
Rejoice Blog: Umekutana na changamoto gani katika huduma yako ya
uimbaji?
Lembo Jr: Changamoto ni nyingi sanaaaa kiroho na kimwili pia
kimwili zaidi ni PESA, nitatizo kikubwa, kiroho vita ni KUBWA sana
Rejoice Blog: Unaonaje muziki wa Injili hapa Tanzania? Na hasa wa aina
unayoimba wewe?
Lembo Jr: Muziki huu naona kwa upande wangu uko vyema maana
haujaniangusha
Rejoice Blog: Unatoa ujumbe gani kwa waimbaji wa nyimbo za Injili
ambao kwa njia moja ama nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia
hii?
Lembo Jr: Kikubwa ni kurudi kwenye kusudi la MUNGU na kulitumikia
Shauri la Bwana
Rejoice Blog: Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unakifanya?
Lembo Jr: Kitaaluma nina Bachelor
Degree ya Public Administration (Shahada
ya Sanaa katika Utawala wa Umma), ingawa sijaajiriwa, ninafanya biashara zangu
ndogo ndogo
Rejoice Blog: Je, kimaisha uko wapi? Ndoa na watoto vipi?
Lembo Jr: Naishi na familia yangu Geita, niko na mtoto mmoja tu
Rejoice Blog: Una ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa
Tanzania?
Lembo Jr: Ujumbe TUIFANYE KAZI YA MUNGU KWA UNYENYEKEVU MKUU SANA
Rejoice Blog: Na kwa jamii inayoguswa na kuburudishwa na nyimbo za
Injili una ujumbe gani kwao?
Lembo Jr: Waendelee kutusapoti kwa hali, mali na maombi.
Rejoice Blog: Ahsante sana Lembo Jr kwa muda wako, Mungu akubariki na
kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu
Lembo Jr: Nami NIWASHUKURU SANA SANA KWA MUDA WENU NA KUJALI KWENU
MUNGU AWABARIKI SANAAAA
Huyo ndiye Emmanuel Stephen Lembo a.k.a Lembo Junior ambaye umepata kumfahamu zaidi kupitia Msanii wetu wa Wiki. Ukitaka kuendelea kufuatilia habari zake na kazi yake ya huduma, mpate kwa njia zifuatazo:
Emmanuel Lembo Jr:
Instagram:
@lembojr
Facebook:
Lembo Jr Emmanuel
~~~ UMEBARIKIWA! ~~~
Labels:
Geita,
Gospel Music,
Lembo Jr,
Msanii wa Wiki,
Muziki wa Injili,
Naioth,
Udom
Subscribe to:
Posts (Atom)





















