Tusome
kwa pamoja Yohana 5: 5-9
“5 Basi, hapo
palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane.
6 Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo, akatambua kwamba alikuwa amekaa hapo
kwa muda mrefu, akamwuliza, "Je, wataka kupona?" 7 Naye akajibu,
"Mheshimiwa, mimi sina mtu wa kunipeleka majini wakati yanapotibuliwa.
Kila nikijaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia." 8 Yesu akamwambia,
"Inuka, chukua mkeka wako utembee." 9 Mara huyo mtu akapona,
akachukua mkeka wake, akatembea. Jambo hili lilifanyika siku ya Sabato.”
Yesu
alipita katika birika lililokuwa likitibuliwa watu wa kwanza kudumbukia
wanapata unafuu.
Akamkuta
mtu amekuwa mgonjwa kwa miaka 38 amekaa pale eneo la birika akiwa amelala na
kwenye ya godoro.
Yesu
alipofika pale akamuuliza unataka nikufanyie nini, akasema hakuna mtu wa
kunipeleka katika birika.
Jibu
lake linafanya tujiulize hivi kweli hakuwahi kuona mtu wa kumsaidia.
Dunia
haitafuti mtu wa kumpa msaada wa chakula au malazi bali inatafuta mtu
atakayewanganisha na MUUJIZA wao.
Warumi
8: 19
“Viumbe vyote
vinatazamia kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake”
Watu
wana nia, shauku na njaa ya kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Ina maana kuna kitu
hakiko sawa mahali fulani, kinasubiri udhihirisho wa wana wa Mungu.
Kutumika
kama daraja kati ya dunia na utatuzi wa matatizo yao.
Najua
utaniuliza nani ni mwana wa Mungu, hebu tusome mistari ya Biblia hapo juu
Yohana
1:11-12
“Alikuja katika
nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. 12 Lakini wale wote
waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu”
Warumi
8: 14
“Wote wanaoongozwa
na Roho wa Mungu ni watoto wa Mungu”
Kama
umempokea Yesu wewe ni mwana wa Mungu
Katika
Ofisi yako, biashara yako na majirani wajue wewe ni mwana wa Mungu.
Sasa
hiyo ilikuwa msingi, tuingie katika somo la PASAKA sasa..
Fungua
na mimi Kutoka 12: 1-13







