Monday, August 10, 2015

KUILINDA IMANI na Pastor Simon Mwamlafu

Neno Yuda 1: 3-4
“Wapendwa, ingawa nilikuwa na hamu kubwa kuwaandikieni kuhusu wokovu
wetu, nimeona ni muhimu niwaandikieni nikiwasihi mwendelee kuipigania
kwa nguvu imani ambayo Mungu amewakabidhi watakatifu mara moja tu kwa
wakati wote. 4 Hii ni kwa sababu watu wasiomcha Mungu ambao tangu
zamani wamekwisha kuandikiwa hukumu hii, wamejiingiza miongoni mwenu
kwa siri. Hawa ni watu ambao wanapotosha neema ya Mungu wetu na
kuitumia kama kisingizio cha kutenda maovu. Wao wanamkana Yesu Kristo
ambaye pekee ndiye Mkuu na Bwana wetu.”

Kanisa limevamiwa na watu ambao sio wa kweli au wasanii, wamejiingiza
kwa siri na nia zao za kupotosha Imani ya Ukiristo.
Hawana nia ya kumtumikia Mungu wala kwenda mbinguni wana mipango ya
siri. Hawana nia ya Wokovu.
1 Timotheo 4: 1-2
“Roho anasema wazi wazi kwamba katika siku za mwisho watu wengine
wataiacha imani yao na kusikiliza roho za udanganyifu na mafundisho ya
mashetani. 2 Mafundisho hayo yanaletwa na wanafiki waongo ambao
dhamiri zao zimekufa kama vile zimechomwa kwa chuma cha moto. “

Mambo ambayo yamelikumba Kanisa la sasa
1.      Kuna mambo mengi yamelikumba Kanisa la sasa kama mafundisho potofu
na manabii wa uongo.
1 Yohana 4:1
“Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone
kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea
duniani.”
Sio kila mtu anasema Bwana Asifiwe ni mtumishi wa Mungu
Kuna watu wamejiingiza hawana nia njema na wokovu, ni wapotoshaji wa
Neno la Mungu
Kuwa makini na mafundisho unayoyapata
Kuna maombezi yanaendeshwa sasahivi watu wanakuwa kama walivyozaliwa
na jinsia tofauti
Kuna watu wamejiingiza makanisani hawana nia nzuri na kanisa
1 Timotheo 4: 3-4
Itakuja wakati watageukia mafundisho ya uongo na kuacha mafundisho ya uzima.
Usiamini kila roho zipime roho
Kuna waumini wengine ni watafiti ,kila siku anabadili kanisa ,
wamekuwa kama helikopta kila siku kutafuta poa kutua
Wachungaji wanapata  shida na waumini watoro, wanawapa wachungaji
stress maana wanarandaranda makanisani

2.      Mwenendo wa Kanisa unabadilika ukilinganisha na tulikotoka hasa
kwasababu ya utandawazi kukua kwa kasi
Waumini wengi hawataki kukemewa wanataka wachungaji wahubiri
wanachotaka wao na sio kile Mungu anataka. Na ndio maana
wanarandaranda wakitafuta wachungaji watakaoubiri wanachotaka,
wakisikia mahubiri ya kukemewa tu wanahama kanisa wanaenda kutafiti
kwingine.
Lakini inabidi kumuomba Mungu akutane na wewe, Mungu akuguse
,akutembelee na kukufinyanga

3.      Badala ya dunia kufuatisha Kanisa , Kanisa linafuatisha namna ya Dunia
Turudi kwenye misingi ya wokovu, turudi kwa Mungu

Mathayo 6: 33
“ Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya
yote mtaongezewa.”

Mungu ameahidi mtu akikaa na Mungu basi Baraka zitamfuata,basi tukae
na Mungu kwanza, tumtafute Mungu kwanza hayo mengine yote yataongezwa
kwetu
Wengine wanakimbilia kuwekewa mikono na kila aina ya watumishi ili
wafanikiwe, wengine wananyeshwa maji , mafuta, chumvi ili wabarikiwe.
Waumini wa leo wamegeuza baadhi ya watumishi kama waganga wa kienyeji
ili  kuwatabiria maisha yao na mustakabali wao. Wengi wanataka miujiza
lakini hawamtaki mtenda miujiza.

Kaa ulipo na simama katika Imani, Mungu atakutokea
Imani yetu ni ya muhimu sana yapasa KUILINDA

Mambo yatupasayo kufanya kulinda Imani
1.      Jihakiki kama kweli umezaliwa mara ya pili
Je mwenendo wako ukoje
Wokovu sio kitu cha kisanii ni kitu halisi na ukifanya vibaya utaishia pabaya
Lazima uwe na mahali unapolelewa maisha yako ya Ukiristo sio
kurandaranda kwenye makanisa mbalimbali

2.      Kuishi maisha Matakatifu
1 Peter 1: 15-16
“Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe
watakatifu katika mwenendo wenu; 16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu
kwa sababu mimi ni mtakatifu.”
Tusiwe watu wenye nia mbili

Mathayo 23: 27
“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnafanana
na makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi
lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu.”
Wengine ni wanafiki wanaishi maisha ya wokovu wakiwa karibu na
Wachungaji tu au watu waliookoka,au wakiwa kanisani lakini wakiwa nje
wala hakuna anayejua kwamba wameokoka maana wanajichanganya na namna
ya dunia hii.
 Marko 7: 6
Ufunuo 3: 15- 16
Msimamo wa wokovu lazima ujulikane

3.       Tuishi maisha yenye ushuhuda
1 Peter 2: 11-12
“Wapendwa, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapi taji njia hapa
duniani, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupi gana vita na roho
zenu. 12 Muwe na mwenendo mwema kati ya watu wasiomjua Mungu, ili kama
watawasema kuwa wakosaji, wayaone matendo yenu mema na wamtukuze Mungu
siku ile atakapotujia.”
Majirani zako wanasemaje kuhusu wewe ,mtaani ,kazini wanasemaje
Sisi ni ladha, chumvi na mwanga ,tusilitukanishe Jina la Mungu
Maisha yetu yanatakiwa yabariki na yainue na yawavutie wengine kwa Yesu
1 Timotheo 4:12
Kuwa kielelezo, watu waige kutoka kwako, wamuone Yesu.
Watu wamtukuze Yesu kwa maisha yako

Yohana 12: 26
Ukimtumikia Mungu naye atakuheshimu
Ukikaa na Mungu , Miujiza Itakufuata
Mungu atusaidie ndugu zangu tuilinde IMANI yetu ya KIKRISTO,Amen

Saturday, April 25, 2015

SEMINA YA MWANAMKE WA THAMANI Moshi na Pastor Neema Shoo

Huduma ya Woman of Value Ministry inayoongozwa na Pastor Neema Shoo inakuletea Semina Ya Wanawake wote, Wa Mama na Mabinti
Lini: Tarehe 9 na tarehe 10 May 2015
Wapi : Ukumbi wa KURINGE MOSHI, JIRANI NA PETROL STATION YA PEACE PARK,

Muda: TAREHE 9 JUMAMOSI TUNAANZA SAA TATU KAMILI ASUBUHI MPAKA SAA KUMI JIONI, NA TAREE 10 JUMAPILI TUNAANZA SAA NANE KAMILI MCHANA MPAKA SAA 12:30JIONI

WOTE MNAKARIBISHWA, MAOMBI NA MAOMBEZI YATAFANYIKA KWA WATU WOTE

Pia Chakula na vinywaji vitapatikana kwa bei nafuu

Thursday, April 9, 2015

CITY HARVEST WELCOMES YOU TO THE GREAT SERVICE EVENT


You are all invited you to a terrific Gospel Event of MAKING THE GREAT SERVICE (MGS) with a monthly theme of GET WELL to be presented at City Harvest Church, Mabibo Garage this Sunday on 12 April, starting at 3 p.m.

Speaker: Pastor Harris Kapiga, Motivational Speaker and Clouds TV Presenter will give intellectual and inspirations to young professionals.

City Shakers praise and worship team will perform live alongside well known gospel singers Mirium Kasula and Phillip Rupia.


It will be great event of hand clapping and joyful praise n worship event accompanied by cultural presentations, interactive discussions, interviews, inspirational talks, prophetic dance, G-Talent, games and many more.


COME AND HAVE SOME FRESH MOMENTS AND GAIN GREATER ENERGY IN THE PRESENCE OF THE LORD

ENTRANCE: FREE

Thursday, March 26, 2015

Mshukuru Mungu kwa kila jambo

Bwana asifiwe wapendwa, jana nilienda Kwenye mazishi ya Shemeji yangu, nilipenda sana mahubiri Mtumishi wa Mungu alitoa somo kutoka 1Watesalonike 5:17 " shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu."
Akasema watu wengi wanamkumbukaga Mungu wakiwa na shida, kama ugonjwa, mateso mbalimbali lakini mambo yao yakiwa mazuri wala hawamkumbuki Mungu.
Lakini pia anaendelea kusema watu wengi wanakwenda kumshukuru Mungu wakipata watoto, wenzi wa maisha, Gari, Nyumba nk, lakini watu hawamshukuru Mungu wakipatwa na taabu, mapito, vilio, misiba, majanga mbalimbali wakati neno hapo juu linatutaka kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

Mahubiri yalikuwa mazuri nilifurahi sana yule mtumishi alikuwa ananikumbusha jambo hilo muhimu.
Kuonyesha kwamba NENO Hilo lilikuwa la kinabii baadae nilikutana na rafiki yangu ambaye miezi michache iliyopita alipatwa na janga kubwa sana yeye na familia yake lakini aliniambia jinsi alivyomshukuru Mungu na ameona Mungu akimtetea na kuendelea muonekania na anakuja kugundua haikutokea kwasababu labda Mungu hampendi bali Mungu analo kusudi jema kwa familia yake na ni kwa utukufu wa Mungu yote hayo yanatokea.
Kwahiyo ndugu yangu hebu muombe Mungu akupe Moyo wa Shukrani kwa lolote unalopitia yamkini ni Gumu sana linakuliza linakuacha huna raha, huna tumaini hebu tu mshukuru Mungu yeye anajua kwanini ameruhusu hayo ilimradi hujamkosea basi   mshukuru
Mungu akubariki na uwe na siku yenye ushindi

Monday, March 16, 2015

The Surprise of an answered Prayer by Pastor Dondo

Pastor  Dondo
Opening Scripture Comes from Acts 12:1-17
 "It was about this time that King Herod arrested some who belonged to the church, intending to persecute them. He had James, the brother of John, put to death with the sword. When he saw that this met with approval among the Jews, he proceeded to seize Peter also. This happened during the Festival of Unleavened Bread.After arresting him, he put him in prison, handing him over to be guarded by four squads of four soldiers each. Herod intended to bring him out for public trial after the Passover.
So Peter was kept in prison, but the church was earnestly praying to God for him.
The night before Herod was to bring him to trial, Peter was sleeping between two soldiers, bound with two chains, and sentries stood guard at the entrance. Suddenly an angel of the Lord appeared and a light shone in the cell. He struck Peter on the side and woke him up. “Quick, get up!” he said, and the chains fell off Peter’s wrists.
Then the angel said to him, “Put on your clothes and sandals.” And Peter did so. “Wrap your cloak around you and follow me,” the angel told him. Peter followed him out of the prison, but he had no idea that what the angel was doing was really happening; he thought he was seeing a vision. 10 They passed the first and second guards and came to the iron gate leading to the city. It opened for them by itself, and they went through it. When they had walked the length of one street, suddenly the angel left him.
11 Then Peter came to himself and said, “Now I know without a doubt that the Lord has sent his angel and rescued me from Herod’s clutches and from everything the Jewish people were hoping would happen.”
12 When this had dawned on him, he went to the house of Mary the mother of John, also called Mark,where many people had gathered and were praying. 13 Peter knocked at the outer entrance, and a servant named Rhoda came to answer the door. 14 When she recognized Peter’s voice, she was so overjoyedshe ran back without opening it and exclaimed, “Peter is at the door!”
15 “You’re out of your mind,” they told her. When she kept insisting that it was so, they said, “It must be his angel.”
16 But Peter kept on knocking, and when they opened the door and saw him, they were astonished. 17 Peter motioned with his hand for them to be quiet and described how the Lord had brought him out of prison. “Tell James and the other brothers and sisters about this,” he said, and then he left for another place."

If you go through these verses you will find two groups Peter who was in prison waiting for trial and the second group is the church praying for Peter to be released. 
When you are praying God will surprise you 
He can use people, or angels but no matter what what he will use can surprise you 
If you want to get surprise from God you jus pray, Prayer is the key to get God surprises 
We need to pray because God cannot do anything unless is through an answered Prayer 
Dont limit God, our God is a Big God
He is the same God yesterday, today and forever he has not changed, he will surprise you but only when you pray

Thursday, March 12, 2015

Wewe ni Mshindi Ishi kama Mshindi

Anza siku yako Leo kwa ushindi Maana wewe ni mshindi Kumbuka kuzaliwa kwako tu ni ushindi

Kulikuwa na mashindano makubwa ya mbegu za uzazi lakini ya kwako ndio ilishinda zingine zikafa

Usijidharau maana asili yako ni ushindi, hata kama mazingira yako ya sasa hayafanani na ushindi yasikutishe hayo yatapita wewe ni mshindi songa mbele ukashinde

Amini kwamba utafanikiwa na kila utakachokifanya Kitafanikiwa

Nenda sasa ukashinde Leo ndio siku yako ya kufanikiwa na kushinda

Wednesday, February 4, 2015

MAOMBI YA KUFUNGUA MALANGO NA MILANGO -1 na Mchungaji Florian Katunzi



Mchungaji Florian Katunzi

Karibu katika mfufulilizo wa somo hili jipya linalofundishwa na Mchungaji Florian Katunzi wa EAGT City Centre, ambalo naamini ukilifuatilia kwa makini hautatoka kama ulivyo. Pia napenda kukwambia ya kuwa jiandae kukipokea kitabu hiki ambacho bado kipo jikoni na kitakuwepo mtaani hivi punde.
 
Leo tunaanza na Sehemu ya Kwanza
 
Zipo aina nyingi za maombi yanayotajwa kwenye Biblia takatifu, na yenye matokeo dhahiri yenye kudhihirisha uweza wa ki-Mungu wenye nguvu za kuangusha ngome zote za giza.  Katika kitabu hiki nitafundisha aina ya maombi ya kufungua  malango na milango.

 

KUOMBA maana yake ni Kumwita Mungu. “Katika shida yangu nalimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.” Zaburi  18:6

 

Ndani mwa maombi haya  BWANA  atakufungulia milango, na hakuna malango yatakayofungwa mbele yako tena. Neno la Mungu linatuambia:

 

 “Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafame; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.”  (Isaya 45:1-3)

 

Kipindi hiki wana wa Israeli walikuwa uhamishoni Babeli, kumbuka walitekwa na kuchuliwa uteka mpaka nchi ya Babeli na Jemadari Nebukadreza, mnamo mwaka 605 KK, baada ya kuwashinda wamisri  katika vita ya Karkameshi. Wakati huo kulikuwa na makundi mawili yaliyopelekwa uhamishoni Babeli, kundi la pili lilikuwa ni lile lililochukuliwa mwaka 586 KK.

 

Huyu Nebukadneza, ni mtoto wa kiume wa Nabopolasa, aliyemridhi baba yake kuwa mtawala wa dola ya Wakaldayo mwaka 605 KK. Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha  The Cambridge Acient history  III Uk. 212.  Nebukadireza alikuwa  jemadari kijana aliyekuwa ana misuli ya vita na tena shujaa na mwerevu wa mapigano, hivyo alikuwa na sifa zote za kurithi kiti cha baba yake.

 

Wachambuzi wa mambo ya kale wanamuelezea kuwa alikuwa ni askari na mwanasiasa aliye heshimiwa sana kutokana na uwezo wake wa kuongoza mapigano na kujenga hoja katika uwanja wa kisiasa.

 

Baada ya kutwaa madaraka, mfalme huyu mpya alihusika kujenga  vyema himaya na alama za Babeli katika maeneo mbali mbali ya dunia, tena alijiongezea sifa kwa kumuoa Malkia wa Media  Amyhiya, binti wa Cyaxareas, aliyekuwa na utawala wa Kaskazini.

 

Neno la Mungu katika kitabu cha Daniel 2:36-43, linatuonyesha kuwa baada ya Nebukadreza aliyekuwa kiongozi wa dola yenye nguvu sana ya Ukaldayo kiasi cha  ufalme wake unafananishwa na kichwa cha dhahabu kwa  thamani yake, hata hivyo, alipojiinua kiasi cha kutaka kuabudiwa, ufalme wake, ulikomeshwa na Dola ya Ukaldayo iliingia hatua ya mwisho pamoja na kuchaguliwa kwa Nabondus mnamo mwaka 556 KK.

 

Baada ya kufa kwa Nebukadreza kinafuata kipindi kifupi cha kupinduana na kuchinjana kwa watawala na mwisho kabisa utawala wa Dola ya Ukaldayo unafutika kabisa na unaibuka utawala wa Wamedio, Umedi na Uajemi (Medionapersia) chini ya Mfalme Koreshi Mwajemi na Dario wa wamedi, walioungana pamoja na kuangusha Dola ya Ukaldayo mwaka 538. Utawala wa wabanabe ulidumu kwa kipindi cha miakamia mbili (200), mpaka 331 KK.  Ndani ya kipindi hiki cha utawala wa Wamedi na Wajemi, tunamuona Koreshi, tuliyemsoma katika andiko letu la msingi akitimiza unabii uliotolewa kwa kinywa cha Nabii Isaya miaka mia moja hamsini (150) kabla ya kutimizwa kwake  katika mwaka 538.

 

Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya wakaldayo. Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka ambayo Neno la BWANA lilimjia Yeremia Nabii, kutimiza ukiwa wa Yerusalem, yaani, miaka sabini. nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwake maombi na dua, pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu.” (Daniel 9:1-3).

Tuesday, February 3, 2015

Ujumbe wa Mwaka 2015: Mwaka Mpya na Mambo Mapya

Bwana Yesu Kristo Asifiwe ndugu mpendwa msomaji wa Blog yetu ya Rejoice and Rejoice
Tunakukaribisha tena katika blog yetu mwana huu wa 2015
Mengi tutaenda kuyaona katika blog hii, tunaendelea tena kwa uweza wake Mungu
Nakukaribisha sana endelea kututembelea mambo mazuri yanakuja
 
 
Ujumbe wangu kwako tunapoanza mwaka huu wa 2015, naomba usome hapo chini