Mara nyingi watu wenye nyadhifa au
majukumu mbalimbali katika makanisa,majumbani,ofisini,vyuoni,au mashuleni huwa
wanakuwa na shida moja ya kutowaamini watu wengine na majukumu wanayoyafanya.
Kama nyumbani utakuta baba au mama
anashidwa kuwaamini vijana wake wakubwa tu kwamba wanaweza kupewa jukumu Fulani
na kufanya bila tatizo,tena mara nyingine wanaweza kufanya vizuri ya wazazi
wao.
Sasa hii inamfanya mzazi awe anajichosha
sana na majukumu mengi,utakuta sehemu ambayo alitakiwa amtume kijana wake
anaenda yeye tena anakuwa ameacha kazi zake za maana sana.
Kuna kijana mmoja alikuwa analalamika
kwamba baba yake haruhusu mtu yoyote aguse gari yake kabisaaaaaa yani it is strictly
prohibited,sasa nikajiuliza sasa kwa mfano siku moja huyo baba amebaki nyumbani
na kijana wake peke yao halafu from nowhere baba akapata shida au ugonjwa ambao
anahitaji mtu amkimbize hospital je
atakodi Tax au watapanda daladala? Sisemi kwamba wazazi wawe Laissez-faire kwa watoto wao la
hasha,lazima kuwe na taratibu lakini nyumba isije ikageuzwa kuwa kambi ya Jeshi
jamani.
Mara nyingine vijana wanalalamika kwamba
wazazi wanashindwa kuwaamini hata wanavyokuwa wanapanga mipango mbalimbali ya
familia,au kama katika familia kuna sherehe Fulani baba anataka afanye yeye
kila kitu maana anaona vijana wake hawawezi,sasa matokeo yake anaweza kuweka
vitu ambavyo enzi zao ndio vilikuwa vizuri lakini kwa kipindi hiki labda jamii
haivikubali sana,sasa hapo ndio mahusiano na watoto yanakuwa yakuburuzana,na
watoto wanakususia maana wanajua hawaaminiki,halafu mzazi unajizidishia stress
maana umri nao uliofika hutakiwa kujichosha sana na mambo madogo madogo,jamani
wazazi wenzangu tumuombe Mungu atusaidie tuwaamini watoto wetu na tuwawezeshe
kufanya majukumu mbalimbali ili na sisi tuweze kujikita katika mambo mazito
zaidi,Amen!
Tabia hii pia iko makanisani,unakuta
mchungaji anashindwa kuwaamini wasaidizi wake,sasa kila siku yeye ndio
anaongoza sifa,maombi,anahubiri yeye,anabatiza yeye,yaaani ni yeye siku
nzima,sasa mwanadamu ana tabia ya kuboreka,ni vizuri kuwaamini kwamba watu wa
chini yangu nao wameumbwa na Mungu huyuhuyu aliyeniumba mimi,kwahiyo wanaweza
wazungu wanasema Trust them…na kukiwa na watu tofauti tofauti wanafanya vitu
mbalimbali kanisani kunakuwa na taste nzuri maana unakuwa umegusa makundi
karibu yote.
Wamama pia tuna tabia hiyo kutowaamini
watu tunaoishi nao kama wanaweza,matokeo yake mama analisha familia yake
chakula saa 6 za usiku maaana ilibidi wasipike mpaka atoke kwenye shughuli zake
usiku,amini na wafundishe jinsi unavyopenda ili ukichelewa waendelee watu wale
ontime na kupumzika,Halleluyaaaaaaaa
Maofisini ndio usiseme,kama wewe ni Boss
una wafanyakazi wako hebu waamini kama wanaweza maana wamesoma na wanajifunza
kama wewe ulivyojifunza,waamini ili siku ukiwa haupo kazi za watu zisilale
mpendwa halafu usiwe na hofu surbodinates wako wakijua kazi zako si lazima sana
wachukue hiyo kazi yako Mungu ni mwaminifu atawafungulia mlango au
atakufungulia mlango sehemu nyingine,Amen!
Hata kama una duka au chochote wewe amini
tu wale wa chini yako wana kitu tofauti na ulicho nacho kwahiyo
wanaweza,wawezeshe ili ikipunguzie na wewe kazi ufanye mambo mengine.
Faida za kuwaamini wengine kama wanaweza ni kama ifuatavyo:
1. Inakupa
wewe fursa ya kuweka mtazamo wako katika mambo yenye manufaa
2. Kuwajengea
uwezo watu wa chini yako kama watoto,wasaidizi kanisani na wafanyakazi katika
ofisi
3. Inakupa
uwezo wa kuongeza ujuzi zaidi katika kile unachofanya pale unapokuwa
unamfundhisha mtu na wewe unajifunza
4. Ukiwaamini
watoto,wasaidizi kanisania,watu wa chini yako ofisini inawaamasisha kufanya
vizuri zaidi na kuwafanya wajitoe kikamilifu katika kila kazi uliyowapa,Aaaamen!
Kwa leo ndio ujumbe wangu……Kama una
laziada maana na mimi sio kama najua kila kitu naomba maoni yako…KARIBU
Mungu akubariki sana unapojiandaa na
sikukuu zilizo mbele yetu
No comments:
Post a Comment