Friday, August 16, 2013

Hofu inachelewesha Muujiza wako


 


Blogger

Kama unaishi maisha ya kuwa na hofu kwamba mambo yako hayatakuwa kama unavyotamani hiyo ni hila ya Ibilisi kuchelewesha muujiza wako.

Neno linasema katika Mathayo 6:31-33 "Msisumbukie, basi mkisema, tuleni nini? au tunyweni nini, au tuvae nini? kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Basi utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo yote mtazidishiwa."

Wako watu wanaofikiri kwamba wakiwa na hofu ndio kujishusha mbele za Mungu, unatakiwa umuelewe sana Mungu kwa kusoma na kutafakari neno lako, Mungu sio kama alivyokuwa Chief wa ukoo wenu ambae alikuwa anawapa watu hofu ili aendelee kuwakandamiza. Yeye amesema kwamba ni Baba kwetu kwa hiyo mtazame kwa Jicho hilo usimtazame tu kama unavyowatazama labda viongozi fulani fulani yeye ni Mungu Mkuu, mwenye uwezo mkuu.

Kama Mungu ameahidi kwamba atakuponya uwe na Imani usiwe na hofu hata kama unaona zile dalili zinapamba moto,mtazame Mungu kwa Imani uamini kwamba Utapona, Amen

Yamkini mume au mke wako amekimbia nyumbani  usiwe na hofu na ukaanza kufananisha maisha yako na wengine waliopita katika changamoto hiyo na hao wenzi hawakarudi tena, Sema wangu mimi atarudi katika Jina la Yesu,anarudi muda si mrefu, Bwana anafanya kitu najua anarudiiiii Haleluyaaaaaaaaaaaaa!

Usiwe na hofu kwamba hutapata kazi,mwamini Mungu na sema kwa Imani kwamba ninapata kazi muda si mrefu, na uishi sawasawa na Maneno ya Mungu.

Labda madaktari wamekuambia kwamba hali yako inaonyesha huwezi kupata Mtoto, Simama neno la Bwana mtu wa Mungu, ondoa hofu mwamini Mungu mwamini sanaaaaa mshike sana, unachelewesha muujiza na hiyo hofu yako,hofu iondoke kwako katika Jina la Yesu. Sema nitapata mtoto haijalishi hali iko hivi au vile ninapata mtoto Katika Jina la Yesuu.

Jaribu lolote,changamoto na mitego ya Ibilisi itaondoka maishani mwako kwa Hofu.

Labda ni hali ngumu ya maisha, Simama ruka ruka sema mimi sio masikini maana Yesu alifanywa masikini ili mimi niwe Tajiri Katika Jina la Yesu, Halleluyaaaaaaaa!

 

Utaweza kuindoa kwa Maombi na Kumtegemea Mungu.

Simama kwa Imani sasa na Ukiri wako uwe wa Imani, AMEN

 

 

 

Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Blog mambo mazuri yanakuja

 

 

2 comments:

  1. Thank you Blogger kwa neno la Faraja na wakati kwangu..nikweli kabisa,.Mungu hajatupa roho ya WOGA bali ya KIASI katika kumjua na kumtegemea yeye.. Ubarikiwe my dia

    By: Frida Brown

    ReplyDelete