Watarajiwa |
Leo katika mwendelezo wa
Somo la Uchumba hadi Ndoa na Vitu muhimu vya kuangalia unapotafuta au kujiandaa kuwa na mwenzi wa maisha yako
,nawaletea kwenu hili swala muhimu sana la kujifunza kutokana na makosa ya huko
nyuma.
Kama ulishakuwa katika
mahusiano mengine huko nyuma na hayakwenda vizuri yakavunjika basi unalo jukumu
la kujiuliza maswali hivi ni kwanini yale mahusiano yalivunjika. Je mimi ndie
nilishababisha na kwanini? Je kama ni huyo mtu mwingine alivunja je ni kwanini
aliyavunja? Au ni watu wengine walivunja kama vile ndugu za mwenzako au
marafiki ni kwanini waone kwamba labda hatustahili kuwa pamoja?
Ukishatathimini hayo
utaweza kujua kwamba labda mara nyingine sio kwamba unatakiwa umwachie tu Mungu
ila na wewe unayo kazi ya kufanya ili yasitokee tena. Watu wengine wanapoona
mahusiano yamevunjika wanajisahau kwamba na wao ni wanadamu kwahiyo wanakuwa tu
na mtazamo kwamba mimi nilikuwa perfect na wala hataangalia kama kuna vitabia
ambavyo vilichangia mahusiano yake ya nyuma yavunjike.
Ni kweli kabisa kuna
wakati mahusiano yanavunjika mpaka kila kitu kinamwinua Mungu kwa hilo maana
mtu alikuwa ananyanyasika na huo uhusiano haukuwa mpango wa Mungu kabisa.
Lakini sio wakati wote kwamba huyo anayelalamika ndio aliyekosewa ila makosa
yalikuwa yake ila mwenzake alimalizia tu kwa kuvunja.
Mtu anaweza kuwa kwenye
uhusiano akawa na majivuno sana kiasi kwamba hata huyo mwenzake anamdharau
anamuona kama vile amebahatika sana kukutana nay eye. Anamdharau hata mbele za
watu,mwenzako anajaribu kukurekebisha lakini hurekebishi sasa anaanza
kukukimbia taratibuuu halafu baadae unakuja kulalamika yaani alianza
kutokueleweka kumbe wewe ndio ulisababisha.
Kama umejichunguza
ukagundua kabisa kwamba kuna tabia fulani unayo ambayo mwenzako aliyeingia
mitini alikuwa anailalamikia kwamba haipendi ni vizuri ukachukua hatua
kubadilika maana utaingia kwenye mahusiano mwengine na usipokuwa makini
atakimbia na huyo kumbe tatizo ni wewe.
Kuna mtu alinishuhudia
alikuwa ameingia kwenye mahusiano na kijana ambaye ni wa maisha tu ya kawaida nay
eye huyo dada alitoka katika familia yenye uwezo mkubwa lakini pia alikuwa na
tabia ya kujiinua sana na kudharau watu ambao ni wa hali ya chini. Sasa hizo
tabia akazipeleka kwa huyo mtarajiwa akawa anamdharau sana na kumringia
mwenzake alijitahidi kumweleza lakini alishupaza shingo hakubadilika,
alishangaa tu analetewa kadi yule kaka anaoa kwakweli alijifunza somo kubwa
japo kwa maumivu makubwa. Akaniambia kutoka hapo aliweza kujifunza kutokana na
makosa aliyoyafanya akajifunza kujishusha maana pia haikuwa rahisi,Ila
alimuomba sana Mungu amuondolee kiburi na majivuno na amfundishe kujishusha,
Mungu ni mwaminifu maana alimshughulikia akamfanya kiumbe kipya kwelikweli,
na baadae Mungu alikuja kumpa mwenzi wake wa
Maisha na kwasababu alishashughulikia ule udhaifu wake Mungu alifanya njia
wakafunda ndoa nzuri tu.
Nimekupa huu ushuhuda ili
ujue kwamba pamoja na kwamba unaomba, unafunga au unafanyiwa ukombozi ujue
unalo Jukumu la kubadili tabia kwa kujifunza kutoka makosa ya nyuma
usicheleweshe muujiza wako mpendwa.
Amua leo kubadilika, amua
leo chukua hatua inawezekana hata ofisini, au marafiki kuna mrejesho nyuma
wamekupa ili ubadilike hivyohivyo ndivyo vinawafanya wale wadada au wakaka
wakimbie hebu badilika kama hatutakula Pilau siku za Usoni.
Pamoja na hili soma masomo
mengine ya Vitu vya kuangalia unapojiandaa kuwa na mwenzi wa Maisha
yaliyoandikwa katika blog hii.
Ubarikiwe sana
nashukuru kwa somo lako,mungu akubariki sana
ReplyDeleteKWANZA NAMSHUKURU MUNGU KWAKUNIWEKA HAI MPAKA SASA,PIA NIKUSHURU KWAKUTUPA ELIM YA KIMUNGU.BINAFSI NIMEJIFUNZA MENGI.MUNGU AWAPE AFYA YA MWILI NA ROHO ILI MUWEZE KUENELEA KUTUPA ELIMU ZAIDI.MUNGU AWABARIKI SANA
ReplyDelete