Christina Shusho muimbaji wa Nyimbo za Injili |
Muimbaji
mahiri wa Nyimbo za Injili nchini Tanzania Christina Shusho anategemea kufanya
tamasha Kubwa la kusifu na kuabudu litakaloambatana na kurekodi Live Albamu ya
Nataka Nimjue.
Uzinduzi
huo unategemea kufanyika Jumapili tarehe 24/11/2013 katika ukumbi wa Kanisa la
CCC Upanga mkabala na Mzumbe University Dar.
Siku
hiyo Christina Shusho atasindikizwa na waimbaji wengine mahiri wa Nyimbo za
Injili kama Bahati Bukuku, John Lisu, Upendo Kilahiro, Paul Clement, Joshua
Mlelwa, Amani Kapama, The Voice and Kinondoni Revival Choir
Kiingilio
ni 10,000/= Wakubwa, 20,000/= VIP na 3,000/= Watoto
Historia
yake ya kuimba Christina Shusho ilianzia alipokuwa Sunday school kanisani,
akaendelea kuimba Kwaya mbalimbali na mwaka 2004 ndipo alipoweza kutoa album yake ya kwanza
inayokwenda kwa jina la Ni Kitu Gani.
Alipokuwa
akizungumza na Blog ya Rejoice and Rejoice Christina Shusho alisema siku hiyo
watu wategemee kukutana na Mungu wa leo na kuna kitu Mungu anakwenda kufanya
maana atatembelea watu kwa kupitia ibada ya kusifu na kuabudu. Watu watakutana na Nguvu ya Mungu.
No comments:
Post a Comment