Tuesday, December 3, 2013

Mkirsto anapoamua Kufanana na Mti wa Mwerezi ndipo Ushindi utaambatana nae

Mwerezi ukiwa umefunika sakafu na kupendezesha JengoFungua na mimi Biblia  Kitabu cha 1 Wafalme 6 :13-18 

13Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.’’

14Basi Solomoni akajenga hekalu na kulikamilisha. 15Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya hekalu kwa mbao za misunobari. 16Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu ya ndani ya patakatifu, yaani Patakatifu pa Patakatifu. 17Ukumbi mkubwa uliokuwa mbele ya chumba hiki ndio ulikuwa na urefu wa dhiraa arobainif. 18Ndani ya hekalu kulikuwa na mierezi, ilionakishiwa mfano wa maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu kilikuwa cha mwerezi, hakuna jiwe ambalo lilionekana.”

Mwerezi ulifatwa Lebanon na Solomoni


Wakati wa Kipindi cha Mfalme Solomoni  miti ya mwerezi ilitumika kufunika mawe yaliyoko kwenye Jengo lililokuwa linajengwa

Wakristo tunatakiwa kufunika mawe yote katika Kanisa

Kanisa tumeitwa kama mwerezi kufunika mawe yote

Mawe ni madhaifu yote ambayo yako katika Kanisa, Familia,Kazi, Watoto, Ndoa n.k

Tunatakiwa kufunika mawe ya kuvunja moyo, kukata tamaa ili watu wakutane na Uwepo wa Mungu

Unatakiwa ufunike mambo ya Ndoa yako maana wewe ni Mwerezi

Siku hizi utakuta vyombo vya Habari vya Kikristo kama Magazeti, Blogs, TVs,Radio n.k vinatumika kuwasema Watumishi wa Mungu Vibaya

Roho ya Kuchafuana imeingia Makanisani, tumesahau kabisa kwamba tumeitwa Kuhubiri Habari Njema na sio kutangaza Mabaya ila Mabaya tunashughulikia ndani kwa Utaratibu uliowekwa.
Kama uko Katika Ndoa na mwenzako ana udhaifu fulani, sio uanze sasa kupita kwa ndugu na marafiki zako ukisema eeenhe jamani usimuone vile mume au mke wangu ana udhaifu a, b,c,d ,Funika mawe mpendwa

Mfunike mwenzako kama ni la Kumrekebisha umrekebishe mkiwa wenyewe kama la kumsaidia umuombeee Mungu hashindwi kitu atamrekebisha, Haleluyaaaaaaaaaaaaaaa!

Sasa una mtoto unafikiri labda tabia yake ni ngumu na imekushinda, uwe mwerezi funika mama , funika ewe Baba, si unaanzia kwa shangazi, then mjomba, then Bibi, Babu, Ukoo hapana funika maweee kama Mwerezi

Mrekebishe kwa Upendo, muonyeshe Upendo, Muombeee hakuna linalomshinda Mungu.

Haya mambo nimejifunza maana kuna mahali nilipita ninaye mdogo wangu nampenda sana lakini katika utaratibu ambazo Mungu na labda Shetani wanajua akakengeuka Imani, kwakweli mwanzoni sikuwa mwerezi nililalamika ila Roho Mtakatifu alinifundisha Siri Nzito ya kufunika, sio Rahisi ila kwa uweza wake Mungu tutayaweza yoteee maana yeye anatutia nguvu, Aminaaaaaaaaaa!


Ukijua Siri ya mtu basi sio unaanza kuitangaza, from point a,b,c,d, funika kama la kurekebisha kwa upendo muite mpendwa hapa haikuwa sawa au muombee, Mungu atashughulika nae.

Haleluya, Basi Mungu akubariki sana na akuwezeshe katika kila hatua ya maisha yako na akuwezeshe kuwa na tabia ya mwerezi tukifunika mawe katika kila mahali tunapokuwa.


Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Blog maana Bwana anafanya mambo makubwa na tuko tayari kutumika na kuleta vile vitu yaani vyakula vya Kiroho na Kuinuliwa ambako Mungu amepanga uvipate, Sema Amina mtu wa Mungu.

 

Mungu Akubariki sanaaaaaa

No comments:

Post a Comment