Mwalimu Samwel Mkumbo |
Utangulizi:
Maana hapa
hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. (Waebrania 13:14)
Mtu huweza
kutoka asubuhi kwenda katika shughuli mbalimbali wengine huenda mashambani
wengine maofisini na wengine kwenye shughuli za aina nyingine, biashara lakini
ifikapo jioni au usiku HURUDI NYUMBANI, inawezekana kama ni watoto au ni wazazi
waliachana asubuhi wengine wakienda kazini wengine shuleni lakini jioni
WATARUDI NYUMBANI.
Mtu anapotoka
mji mmoja na kwenda mji mwingine kwa ajili ya kuishi huko aidha kwa sababu za
kikazi au hata biashara, akafanikiwa na akaanzisha maisha huko akawa na familia
huko na akajenga na makazi yake huko, lakini siku akifariki mara nyingi wengi
HURUDISHWA kuzikwa NYUMBANI.
Katika kitabu
hiki ambacho kitakusaidia kukueleza mambo kadhaa juu ya wokovu ulioupokea
katika maisha yako, utajifunza mambo mengi na ni maombi yetu ya kwamba kitabu
hiki kiwe msaada mkubwa sana kwako.
Mambo
utakayojifunza:
Sura ya
Kwanza: katika sura
ya kwanza utajifunza namna ambavyo dunia hii si mahali pa kupategemea na ya
kwamba si mahali pa kudumu, na pia utajua kama dunia si mahali pa kupategemea
je hatma yako ni nini, na ni nini mwisho wa maisha yako.
Sura ya
Pili: itakusaidia
kujua ni nini unachotakiwa kufanya kama dunia si mahali pa kudumu ili uweze
kufika unakotakiwa kwenda, utajifunza kuwa unahitaji sana maandalizi ya
kuelekea mahali unapotakiwa kwenda.
Sura ya
Tatu: mambo ya
msingi ikiwa ni mwendelezo wa sura ya pili ni kujua ya kwamba unakokwenda
hutakiwi kwenda mikono mitupu, kuna mambo unayotakiwa kuyabeba, hivyo kwanza
utajikuta kuna maswali unatakiwa kuyajibu ya ulichobeba kwanza na kisha utajua
ni nini unatakiwa kubeba.
Sura ya
Nne: sura hii
itakuelekeza mambo ambayo ni muhimu uyafahamu katika safari hii, mambo
yatakayotokea njiani, mambo ambayo yanapotokea usishangae, lakini pia utapata
tumaini kwa kujua ya kwamba hauko peke yako.
Nimalizie
utangulizi huu kwa kusema JIANDAE KURUDI NYUMBANI.
Sura ya kwanza.
DUNIANI
SIO KWETU
Nataka niweke
wazo hili kwanza kwako wakati unaendelea kusoma sehemu hii, ni kwamba DUNIANI
SIYO KWETU, ndio! Namaanisha hata wewe hapo ulipo, Duniani siyo Kwako,
haijalishi umeweka nini duniani, au unaipendaje dunia, au dunia inakupendaje.
Si kitu unawapendaje watu wa dunia na vitu vya dunia lakini nataka ujue, na
siyo utani kabisa kwamba hapa DUNIANI SIYO KWETU.
Waebrania
13:13-14 imeandikwa
hivi;
13 Basi
na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. 14 Maana hapa hatuna
mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.
Kwa mujibu wa
mistari hiyo hapo juu, unaweza kuona mambo ambayo yanaweza kutupa msisitizo wa
kuelewa nini ninachomaanisha ninaposema ya kwamba hapa duniani siyo kwetu, na
maandiko yanathibitisha hilo, kuna watu huwa wanaamini baada ya kuhukumiwa kwa
ulimwengu, Shetani na wenye dhambi basi dunia hii ilivyo vivi hivi tutakuja
Kuirithi wale walioamini na kukaa milele na milele, Hapana! Si dunia hii,
kabisa, si dunia hii, ambayo tutairithi, dunia hii si kwetu.
Katika
mistari hiyo ya Waebrania 13:13-14 kuna maneno nataka tuyatazame kwa
jicho la kutuonesha kuwa Duniani siyo kwetu, mstari wa 13 kuna maneno haya… Basi
na tutoke tumwendee nje ya kambi,…. Hiyo inatupa mwanga kwamba kuna
Hatua za kusogea au kutembea kuelekea upande fulani au mahali Fulani kutoka
hapo ulipo.Halafu katika mstari wa 14 kuna maneno haya…… Maana hapa
hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao…… ikiwa inatupa sasa hoja
ya msingi kabisa ninayokuandikia katika sehemu hii, anaposema “Maana hapa
(Duniani) hatuna mji udumuo”. Hiyo inatuonyesha hata kama
kuna mambo gani umewekeza au unayatumainia hapa duniani hayatabadilisha maana
kwamba hapa duniani siyo kwetu.
Hebu
tuunganishe hiyo mistari ya hapo huu katika sehemu zake ili nikufundishe jambo,
tunapounganisha mstari huo wa 13 na 14 kwenye sehemu tunapata maneno haya………”13
Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi………14 Maana hapa hatuna mji udumuo,……”
Sasa unaweza
kuona maana tunayoipata katika mistari hiyo hapo juu ya kwamba….TUTOKE
TUMWENDEE NJE YA KAMBI (Dunia)………MAANA HAPA HATUNA MJI UDUMUO……….
Katika sehemu
ya pili ya mstari wa 14 tunapata maneno haya, “….. bali twautafuta ule
ujao.”, sehemu hii inatupa uhakika kuwa Duniani sio kwetu; na hivyo
tunapata mtiririko mzuri sana katika maneno hayo ambao tunaweza kuuweka hivi;
Kwa maana……TUNAHITAJIKA
KUTOKA…………..
Kwanini……….HAPA
HATUNA MJI UDUMUO………..
Bali/Lakini………TWAUTAFUTA
ULE UJAO……………….
Hivyo basi
kwa maana hiyo inatupa uhakika wa kujua ya kwamba hapa duniani siyo kwetu na ya
kwamba katika uhalisia mwanadamu awaye yote katika vyote na yote hawezi kuishi
hapa duniani milele, kuna
wakati wakati wa kurudi alikotoka na atahitaji kuwa na
uhakika wa mahali anapokwenda, ndiyo maana KUOKOKA NI MUHIMU SANA maana unakuwa
na uhakika wa mahali unapokwenda, ndio!, UKIOKOKA UNAKUWA NA UHAKIKA WA MAHALI
UNAPOKWENDA, hivyo basi Hongera sana kwa wewe uliyeamua Kuokoka maana tangu
sasa unapata uhakika wa mahali uendapo.
Mhubiri
12: 7 inasema imeandikwa
hivi;
Nayo
mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Mstari huu
unathibitisha kile ninachokuambia kuwa “Duniani sio Kwetu” ambapo pia
kimeandikwa katika kitabu cha Waebrania ya kwamba hapa “hapa hatuna mji
Udumuo bali twautafuta ule ujao” na Suleimani mwana wa Daudi katika
kitabu cha Mhubiri anasema “Mavumbi (Mwili wako) huirudia nchi, nayo roho
(yaani Wewe) humrudia Mungu aliyeitoa”
Twautafuta
Ule
“Ujao”
Tuliposoma
Waebrania 13:13-14, katika ule mstari wa 14 tulipata maneno haya “………….bali
twautafuta ule ujao”, nami natiwa Nguvu kusema nawe mtu uliyeokoka ya
kwamba pamoja “Duniani siyo kwetu”, na ya kuwa “Hapa hatuna mji
Udumuo” lakini kitendo cha kukubali KUOKOKA na kumpa Yesu maisha yako kama
kiongozi na “Mfalme” wako basi wewe umeanza safari ya “KUUTAFUTA ULE (MJI)
UJAO”, naam!, nan i safari muhimu sana katika maisha yako na inahitaji
maandalizi ya muhimu maana UNARUDI NYUMBANI ambapo Yesu alikwenda
kukuandalia “Makao” na huko kwenye hayo makao yako ambayo Yesu anakuandalia
ndiko “Nyumbani Kwetu”.
2 Nami
nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa
Mungu, umewekwa tayari,……. (Ufunuo
21:2), mstari huu unatupa tumaini ya kwamba upo mji mwingine unaondaliwa kwa
ajili ya watu waliookoka, naam!, kwa ajili yako, pale tu ulipoamua Kuokoka basi
nawe unayo nafasi ya kuwepo katika mji huu unaondaliwa kwa ajili ya wale
waliompokea Bwana Yesu kama mwokozi wa maisha yao na kuomba msaada na kujitoa
maisha yao yawe yenye hofu ya Mungu kila siku na kila wakati.
Lakini kabla
hujafika katika mstari huo wa 2 katika kitabu cha Ufunuo 21, upo mstari
unaotangulia ambao unasema hivi; “1Kisha nikaona mbingu mpya na nchi
mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita,…………..”. (Ufunuo
21:1)
Nilitaka
utazame maneno haya…… Mbingu MPYA na Nchi MPYA……………halafu maneno
yanayofuata yanasema………. kwa maana Mbingu za KWANZA na Nchi ya KWANZA
zimekwisha kupita………… sasa unaweza kuona zaidi jinsi maneno haya
yanavyothibitisha kwamba “DUNIANI SIO KWETU”, naam maana kuna “Mbingu Mpya na
Nchi Mpya” na hizi zinakuja kwa kuwa “Mbingu za Kwanza na Nchi ya Kwanza
zimekwisha Kupita”
Nchi ya kwanza na miji hii itakwenda wapi?
2 Petro3:7
inasema hivi;
Lakini
mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa
hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
Umeona? Labda
soma tena huo mstari, imeandikwa hivi…..”LAKINI MBINGU ZA SASA NA NCHI
ZIMEWEKWA AKIBA KWA MOTO, KWA NENO LILO HILO, ZIKILINDWA HATA SIKU YA HUKUMU,
NA YA KUANGAMIA KWAO WANADAMU WASIOMCHA MUNGU”, hivyo ndivyo imeandikwa, hivyo
basi uzidi kuwa na uhakika zaidi na zaidi kuwa ‘Duniani sio Kwetu”.
Naam! Na hii
ndio inatupa maana halisi ya Ufunuo 21:1 ambapo imeandikwa ………. kwa maana
Mbingu za KWANZA na Nchi ya KWANZA zimekwisha kupita…………, kumbe basi
kila kilichopo sasa, unachokiona ni “Akiba kwa ajili ya Moto”, naam!, Masoko,
Viwanja vya Ndege, Bandai, Magari, Majengo ya Thamani na kila ukijuacho kwa
jina na kila kitega uchumi ambacho kinategemewa na mwanadamu na kila
kisichotegemewa au kisichokubalika vyote ni kwa ajili ya moto, oooh!, ni jinsi
gani inashangaza. Maana cha ajabu hadi wanadamu ambao HAWAJAOKOKA au ambao
HAWATAOKOKA nao ni “Akiba kwa ajili ya Moto”.
Naam, KWA AJILI YA MOTO……………………..
Tutaendelea wiki ijayo, Karibu sana Rejoice and Rejoice blog
No comments:
Post a Comment