Bwana Yesu asifiwe wapendwa,leo tunaendelea na Somo
letu la Vitu muhimu vya kuangalia au kufanya unapojiandaa kuwa na mwenzi wako
wa maisha.
Nitazungumzia jambo muhimu sana ambalo watarajiwa wote
wawili yaani mwanamke na mwanaume inabidi kujifunza na kuliombea ili mnapokuja
kuishi pamoja muwe na ndoa yenye Amani na inayomtukuza Mungu. Jambo lenyewewe
ni;
Hasira – Mjipange kuizuia isije ikawaharibia mahusiano
ya sasa au ya mbele.
Hasira kwa kifupi ni hali ya mtu kujisikia vibaya,au
kuchukia na kuwa na msukumo mkali unaomfanya mtu afanye kitu ambacho
hakutegemea kukifanya mara nyingine.
Kwa miaka mingi ambayo Mungu amenipa hapa
duniani,nimekuwa katika familia yetu,familia zingine,makanisa
mbalimbali,mashule,vyuo,maofisi mbalimbali sijawahi kuona mtu ambaye hana
HASIRA.
Kwa hiyo nataka nikuambie kwamba kila mtu ana hasira
ila tu tofauti tu ni jinsi watu wanavyoweza kuikabili. Hasira inaweza kuwa
mbaya au nzuri au mbaya.
Ninaposema nzuri ni kwamba kuna ile hasira ya kuchukia
vitu vibaya au dhambi hiyo ni nzuri.
Hebu tuangalie neno la Mungu linaloonyesha ni hasira
ambayo iko chanya (positive) ,fungua na mimi Zaburi 7: 11 “Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku”
Katika neno la Mungu hapo juu tunaona kwamba Mungu naye
anachukizwa lakini anachukizwa na dhambi.
Pia Kutoka 11:
4-8 tunaona jinsi ambavyo Musa alikuwa na hasira juu ya matendo mabaya ya Farao
twende tuone Maneno ya Mungu yanavyosema;
“4
Musa akasema, Bwana asema hivi, Kama usiku wa manane mimi nitatoka nipite kati
ya Misri;
5
na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa
kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa
huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote
wa wanyama.
6
Ndipo kutakuwa na kilio kikuu katika nchi yote ya Misri, ambacho mfano wake
haujakuwa bado majira yo yote, wala hautakuwako mfano wake tena kabisa.
7
Lakini katika wana wa Israeli hapana hata mbwa atakayetoa ulimi juu yao, juu ya
mtu wala juu ya mnyama; ili kwamba mpate kujua jinsi Bwana anavyowatenga
Wamisri na Waisraeli.
8
Tena hao watumishi wako wote watanitelemkia kwangu mimi, nao watanisujudia,
wakisema”
Sasa Hasira ninayotaka kuzungumzia hapa kwa msisitizo
sio hii ya kuchukia mabaya ni ile ambayo inakusababisha ukafanya au ukasema
Maneno mabaya au makali na kuleta madhara kwa muhusika.
Neno la Mungu katika Yakobo 1:20 “Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki”,
Kama neno linavyosema ni vizuri watarajiwa ambao mnapanga kufunga ndoa mkaanza
kujifunza na kuomba msiwe na Hasira ambayo itaaribu uhusiano na Mungu na wa
kwenu nyinyi wenyewe mtakapokuja kuishi pamoja.
Hili litawezekana kama mtakuwa wawazi kwa kila mmoja
wenu na kupeana mrudisho nyuma mnavyokuwa katika hatua zote za maisha yenu,kuanzia
uchumba hadi kwenye ndoa.
Mkiwa wawazi na kuishi maisha halisi kwa kila mmoja
inasaidia kutoweka vitu na kusameheana kwa haraka, lakini kama hakutakuwa na
uwazi mwenzako hatajua umekwazika na nini kwa hiyo ni rahisi akafanya kitu
kikakukwaza na kuumiza, hapo ndipo hasira inakuja kwako unaweza kutumia Maneno
makali au matendo kwasababu moyo wako unawaka moto umejaza vitu vingi
hujasamehe,wenzetu wanasema una blow –out ni mbaya sana yaani unalipuka.
Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa napenda kusema
nitakulipukia kama Sodium, kwa wale mliosoma Chemistry mtaelewa mlipuko wa
Sodium ulivyo ni mkubwa haswaa. Nilipoendelea kujifunza neno la Mungu
nikagundua kwanza mdomo wangu na Maneno ya kinywa change yana nguvu ya
mustkabali wangu maana neno linasema katika Mithali 18: 21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao
watakula matunda yake.” Hili neno lilinifundisha sana sana nikaacha hayo
maneno na kukataa kabisa maana neno linakufanya uwe kama unavyosema,kama na
wewe una kitu unasema cha tofauti badili kwanza. Nilisoma pia katika kitabu cha
Think Big Dr Ben anaelezea pia kusoma Mithali kulimsaidia sana kuwa mbali na
hasira mbaya.
Ushauri wangu kama una hasira fanya yafuatayo;
1. Muombe
Mungu akuondolee hasira mbaya
2. Ongea
na mwenzako akusaidie pale anapoona una tabia ya hasira akupe mrudisho
nyuma,kukushauri na kukuombea
3. Soma
sana neno la Mungu fanya kama project ya kusoma Neno, anza na Mithali kwanza
ina mistari mingi
4. Pata
muda wa kutulia unapokuwa umekwazika bora unyamaze kwanza baadae utafute
suluhisho
5. Kama
unajijua unaweza kushikwa na hasira za haraka jihadhari na watu wenye hasira
mbaya wanaweza kukufanya ufanye jambo la hasira,ukae nao kwa akili
6. Kama
hasira yako ni ile ya kuvunja na kurusha vitu na umeokoka au kupiga, nakushauri
ongea na Mchungaji wako au wanamaombi wa kanisani kwako wakuombee maana hicho
ni kifungo
7. Chukua
hatua na kuchukia hasira mbaya, ukiichukia utajifunza kujizuia kimenisaidia
kiasi hiki
8. Kuna
rafiki yangu alinishudia alikuwaga na hasira sana sana, alianza kujifunza kuwa
mtu wa mzaha mzaha tu kutochukulia vitu anavyofanyiwa serious ili msaidia
kurejesha mahusiano na kuepusha magomvi. Ni njia nzuri pia hii unaweza kuifanya
Najua umepata Dozi nzuri sanaaa leo, na tumenufaika
woote maana hata hapa najifunza na mimi
Namshukuru sana Roho
Mtakatifu anavyoendelea kunitumia katika Somo hili najua kuna mahusiano
yanaponywa, Na utukufu ni Kwako ewe Bwana Yesu.
Tutaendelea…..
Amen, This is so true not only to those who want to get married but even those who are already in the marriage. May the Lord bless you so much and use you more and more for His only glory!!
ReplyDelete