Mwalimu Samwel Mkumbo |
Hakika Baraka ni jambo
mojawapo la msingi sana kwa watoto wa
Mungu na ni jambo la Faraja tuonapo mwana wa Mungu akifanikiwa katika mambo
yake yote. Kama inenwavyo;
..,….Mzee, kwa Gayo
mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na
kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo…,… (3Yoh
1:1-2)
Sasa basi ni vema ukafahamu
ya kuwa kubarikiwa ni jambo la msingi
sana na tena ni moja ya ushuhuda kwa watoto wa Mungu. Lakini pia Baraka ni
kutukuka sana katika Ukuu wa Mungu na pia juu ya haya yote tunaweza kuona ni
kwa jinsi gani uweza wa Mungu
unajidhihirisha katika mambo yetu ya mwilini naam katika kutuma mema katika
Tumaini jipya la imani yetu.
Lakini pia Biblia inatupa
maelezo kadhaa juu ya kupata Baraka au mafanikio maana si kila mafanikio
(Baraka) zina mkono wa Mungu ndani yake, au ni utukufu wa Mungu mingine ni
mitego ya shetani katika kutuangusha katika imani yetu katika KRISTO YESU,
naam! Maandiko matakatifu yanatupa mifano kadhaa ya Baraka zitokazo kwa Mungu
na zile zinazoletwa na mwovu kama mtego kwetu.
Vielelezo!!
-Habari za Elisha na Naamani.
2
Wafalme 5:1-14 tunaona kisa kizuri na cha kutufundisha
juu ya Baraka.
Nabii Elisha alipata
nafasi ya kufanya muujiza wa uponyaji kwa Naamani (Yule jemadari wa Shamu) juu
ya ukoma wake, na baada ya muujiza huo, mtu huyo, huyo Naamani alitaka kumpa
zawadi Elisha, lakini Elisha hakukubali,. 2
Wafalme 5: 15-16 inasema;
Akamrudia Yule mtu wa
Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema,
Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna
Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa
mtumwa wako. Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo ambaye nimesimama mbele yake,
sipokei kitu. Akamshurutisha apokee, lakini akakataa.
Katika maandiko hayo
utaona ya kuwa Elisha hakupokea Baraka kutoka kwa Yule Jemadari naam, huyo Naamani, lakini ni vema tukafahamu ya kuwa si
kwa sababu Elisha alikuwa na tabia ya kutopokea zawadi na Mbaraka kutoka kwa
watu aliowahudumia, la hasha! Bali ipo sababu nyingine, maana ni Elisha huyu huyu alipokea msaada kutoka
kwa mama Mshunami! Tazama hapa; 2Wafalme
4:8
Kwa hiyo si kila tunuku
unayopewa ni ya kukubali lakini pia si zote ni za kukataa maana kila jambo lina
maana yake na matokeo yake ambayo kwa hayo twaweza kutambua kusudi na mapenzi
ya Mungu kwetu lakini pia hila na mitego ya shetani.
-Mfano
wa Yesu.
Moja ya mifano tunayoweza
kupata kuhusu habari ya Baraka au kutunzwa ni kuhusu habari za Yesu mwenyewe. Luka 4:5-7 imeandikwa hivi;
Akampandisha juu,
akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia,
Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami
humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa
yako.
Katika mistari hiyo
unaweza kuona mfano wa Baraka ambazo huja kwetu kama mtego, maana katika
kutazama hayo waweza kuona namna ambavyo shetani aweza kufanya aina flani ya
mafanikio kwetu na huja kwa mtindo wa kututamanisha sana hata kutuvuta karibu
nazo lakini kumbe ni njia ya upotevu.
NAMNA
YA KUTAZAMA BARAKA/MAFANIKIO YANAYOKUJIA YANATOKA WAPI.
Katika nafasi hii tupate
kujua japo kidogo namna ya kutazama Baraka na mafanikio yetu na yanayotujia
kuwa yanatoka wapi ili iwe ni nafasi nzuri kwetu kujua ni kwa jinsi gani
tutamtukuza Mungu kwa anavyotuwezesha au ni kwa jinsi gani tunaweza kukwepa
mishale ya mwovu anayoturushia kwakutumia kifuniko cha Baraka au mafanikio.
Ø Lengo la Anayetoa.
Kutambua lengo la anayetoa
sadaka ni njia mojawapo ya kujua ni chanzo gani hizo Baraka au mafanikio
yanabubujika, maana kila sadaka au kitu unachopokea au anachokupatia mtu kina
lengo lake, kwa hiyo kutazama nini lengo ni njia mojawapo inayoweza kusaidia.
Vielelezo.
·
Kuhusu Yesu.
Ukitazama vizuri habari za
Yesu hapo juu unaweza kugundua nini
lilikuwa lengo la shetani kutaka kumtunuku mtu au kutoa kitu, tazama
alivyomwambia Yesu;
…….. Nitakupa wewe enzi
hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu,……..,,. Basi, wewe
ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako..,...(Luka
4:5-7). Sasa unaweza kugundua kuwa si kwamba Yesu hakuhitaji hizo fahari ila
nini lengo la shetani kumpa,.. tazama tena alivyosema; …….. Basi, wewe ukisujudu
mbele yangu yote yatakuwa yako..,..
Maana Yesu alikuwa ni
muhitaji wa mambo ya mwilini pia yaani chakula, mavazi na malazi, ndio!
Alihitaji hayo pia na kuna watu
walimhudumia katika hayo na hakukataa, maana imeandikwa hivi katika
Injili ya Luka;
Na
wanawake kadhaa wa kadhaa ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa
wakaponywa;……..na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.(Luka 8:2)
Yesu hakukataa kwa
wanawake na watu hao kumhudumia kwa mali zao lakini alikataa kupewa Milki na
fahari ya Ulimwengu na shetani (kwa kumsujudia), nini sababu? Bila shaka ni
LENGO!!
Tutaendelea wiki ijayo na vipengele vilivyobakia vya namna ya kuangalia Baraka zinazokujia zinatoka wapi
Karibu sana
No comments:
Post a Comment