Kwa kifupi Mwalimu Samwel Mkumbo ni Mhitimu wa Chuo Kikuu mwenye wito na karama ya Kufundisha Neno la Mungu.
Karibu tuendelee na Sehemu ya Pili ya Somo hili lililoanza wiki iliyopita, kama hujasoma sehemu ya Kwanza nakushauri pitia katika blog hii usome sehemu ya kwanza ili kupata mtiririko mzuri wa Somo.
Mwalimu Samwel Mkumbo |
Ø Chanzo cha Mapato ya
Anayetoa/ Chanzo cha Sadaka yenyewe.
Kuna
wakati tunaweza kujua nini uamuzi wa kufanya au nini ni nia ya sadaka
tunayopokea kwa kuangalia chanzo cha mapato ya anayetoa, au chanzo cha sadaka
hiyo. Tazama mfano huu;
Huyo
mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme,na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo
muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme……….. Lakini
Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme,
wala kwa divai aliyokunywa…….. (Danieli 1: 5, 8).
Ninachotaka
tuone hapo ni kwamba pamoja ya kwamba hawa vijana watatu, naam, huyo Danieli,
Meshaki, Shedraki na Abednego walipata nafasi ya kupata chakula kizuri kutoka
katika meza ya mfalme tena wakiwa katika nchi ya ugeni bila kusahau walikuwa na
hadhi ya utumwa, lakini hawakukubali kupokea hiyo Baraka au zawadi kutoka
Ikulu, tena Biblia imeweka kweupe sababu yao, ni kwamba hawakutaka kujitia unajisi.
Maana
walijua ya kuwa kuna uwezekano ya kuwa kama
ni nyama basi zitakuwa zilizokuwa zimetolewa sadaka kwa miungu ya
Wababeli, lakini pia hawakupenda kunywa mvinyo yao wala kitu chochote, lakini
pia hawakutaka kujitia unajisi kwa chakula cha mfalme na ilikuwa ni mila na
desturi ya wayahudi kutoshiriki chakula na watu wa mataifa.
Japokuwa
biblia haijaweka kweupe ni lini hasa au wakati ambao hao wakina Danieli
waliacha kula mtama au ni lini walianza kula vyakula vya kawaida lakini sabab
kubwa ya kukataa ni kwamba walikataa chanzo cha chakula hicho.
Ø Uhusiano wa mtoaji na watu
wengine.
Kuna
wakati mwingine watu hupenda kuwafadhili watumishi wa Mungu na kuonesha wema
kwa watumishi wa Mungu, tena sana. Lakini unakuta mtu huyo huyo huwatendea watu
wa nyumbani mwake mambo maovu, na hata kama si watu wa nyumbani mwake lakini
hata watu wengine wa kawaida huwatendea mambo yasiyo mema wala hawafadhili, au
kuwatendea wema nga kidogo. Jambo kama hilo si jema na ni vema mtu kama huyo
uwe nae makini sana maana inaweza kuwa mtego sana kwako, lakini pia inaweza
kuwa laumu kwa hao anawatendea mabaya maana wanaweza kuona kuwa unawafanyia
fitina,. Tusome pamoja hapa;
……..Kwa
hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya
waaminio….(Wagalatia 6:10).
Lakini
kwa makini tena tazama maneno haya…………tuwatendee watu wote mema;….na hasa jamaa ya
waaminio…..
Ushauri
wa Ziada.
Katika
kukaa katika nafasi nzuri ya utumishi na mahusiano mazuri na watu na namna ya
kuangalia jinsi tunavyotumika tazama kitabu cha TIMOTHEO.
No comments:
Post a Comment