Friday, July 25, 2014

JE UMEKATALIWA

                 
 

Mara Nyingi utasikia mtu akisema yule jamaa Ana Roho ya kukataliwa au mimi jamani kila ninachokifanya nakataliwa au kila ninapoenda nakataliwa.                         
 
Inawezekana umekataliwa mambo mengi katika maisha tena kibaya zaidi umekataliwa na watu wako wa karibu kama ndugu, jamaa na marafiki au pia waweza.kujikuta umekataliwa na wafanyakazi wenzako au wafanyabiashara wenzako au watumishi wenzako, wanafanya maamuzi makubwa lakini hawakihusishi labda wanakudharau wanaona kwamba hustahili kujua.     
Mara nyingi familia zimekuwa na tabia ya kuwakataa na kuwatenga wenye kipato kidogo katika familia, yamkini wewe ni mzaliwa wa kwanza lakini familia haikudhamini IMEKUKATAA kwasababu hawaoni mchango wako na.kwakweli hujafanya makusudi ni kwamba huna tu cha kutoa, wameuza uzaliwa wako wa kwanza kwa mdogo wako ambaye ndio Tajiri wa familia, wanaamua maamuzi makubwa ya familia hawakushirikishi kwasababu tu huna kitu.     Ndugu yangu watu wamekudharau ,wamekucheka, wamekung'ong'a kwasababu huna kitu au huna elimu au huna mtoto au huna mwenzi wa maisha, labda hali yako ya kukataliwa imesababisha huna hata pa kukaa wala huna wa kukupa chakula Ndugu yangu nimekuja kuongea na wewe siku ya Leo waliokukataa ni wanadamu tu ila Mungu hajakukataa wala hana mpango wa kukutaa unayo sababu ya kufurahi siku ya Leo kwasababu mfalme wa wafalme ,Mungu Mkuu,Jehova,Yahweh,HAJAKUTAKAA.                 
 
Ukisoma 1 Petro 2: 4-9, utaona jinsi hata Yesu alikataliwa lakini maandiko yanasema katika mstari wa 4 "Mmwendee yeye jiwe lililo hai lililokatakiwa na wanadamu lakini kwa Mungu ni TEULE LENYE HESHIMA".                         
 
Yesu alikataliwa na wanadamu, alipigwa, alidhihakiwa, alitemewa mate,alidharauliwa , ALIKATALIWA tena kwa watu wake wenyewe wakimkejeli huyu si mtoto wa fundi seremala tu iweje Leo a anatuletea wokovu kwasababu wao walikuwa na madaraja kwamba labda katika ukoo Fulani tu au watu wa aina Fulani ndio tu wanaweza kuwa wazuri wakasahau Yuko Mungu ambaye njia zake hazichunguziki,anayejua Mwanzo na Mwisho wake, Leo ndugu yangu ukumbuke Mungu ni yeye yuleyule hajabadilika anakuon tofauti na watesi wako wanavyokuona, hali ya sasa isikufanye ukakata tamaa ukakosa Baraka na Miujiza Mikubwa iliyo mbele yako, hivi unajua ndugu yangu wewe ni Uzao mteule,kuhani wa kifalme, taifa takatifu, mtu wa Milki ya Mungu? Usisikilize kelele zao Mungu anakuwazia mawazo Mema, hakuna mwanadamu mwenye usemi wa mwisho juu ya mustakabali wako aliyekuumba ndio anajua mustakabali wako yeye ndio anakujua, wao wakiona maskini, Mungu anakuona Tajiri, wakikuona huzai Mungu anaona hakuna tasa katika Israel, wakiona wewe wa mwisho Mungu anakuona kichwa wala si mkia, Wewe ni Mshindiiii.                          
 
 Inuka Mungu HAJAKUKATAA.........Haleluyaa

No comments:

Post a Comment