Monday, September 2, 2013

Tweka Kilindini na Fred Raphael


 

Neno la kutuongoza linatoka katika Luka 5: 1-8 “1 Siku moja Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongana wanalisikiliza neno la Mungu.

 2 Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa; wavuvi wenyewe walikuwa wametoka, wanaosha nyavu zao.

3 Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja, iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.

4 Alipomaliza kufundisha, akamwambia Simoni, "Peleka mashua mpaka kilindini, mkatupe nyavu zenu mpate kuvua samaki."

5 Simoni akamjibu, "Bwana, tumejitahidi kuvua samaki usiku kucha bila kupata kitu, lakini kwa kuwa umesema, nitatupa nyavu."

 6 Baada ya kufanya hivyo, wakavua samaki wengi, hata nyavu zao zikaanza kukatika.

7 Wakawaita wenzao waliokuwa katika mashua nyingine waje kuwasaidia. Wakaja, wakazijaza mashua zote mbili samaki, hata karibu zingezama. 8 Simoni Petro alipoona hayo, akapiga magoti mbele ya Yesu akisema, "Ondoka mbele yangu, ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi!”

Vitu vizuri haviko juu juu viko kilindini yaani chini kabisa.

Samaki wazuri wako kilindini,madini ya thamani sana halikadhalika yanapatikana kwa kuchimba chini sana.

Kutoka neno tulilosoma hapo juu inaonekana hao watu walikuwa wametumia akili zao sana lakini hawakufanikiwa.

Kuna mahali uzoefu, elimu, na mtandao (connection) ulizonazo zinagota hapo sasa ndio Mungu anachukua nafasi yake.

Mambo mazuri ya Mungu hayako juu juu tu pia inabidi kutweka kilindini.

Kama utampa Bwana nafasi katika maisha yako kwa mshahara uleule, kazi , elimu ulivyonavyo sasa unaweza kufanya makubwa kwasababu umevikabidhi kwake.

Mruhusu Yesu atakufunulia, atakupitisha, utaona vitu ambavyo hujawahi kupata.

Ukitazama katika neno la Mungu utaona uhalisia wako wewe ni nani, Akaacha vitu akamfuata yeye anayeweza kukupa vitu.

Inawezekana umejaribu mengi kwa uwezo wako lakini kwa Neno la Bwana inawezekana.

Kutweka Kilindini ni kujiachia kwamba wewe mwenyewe huwezi ila mwachie yeye atakuwezesha.

Kujitoa kwa Bwana, Kumimina moyo wako na kukaa katika mpango wake.

Watu wengi wanataka matokea tu lakini hawamtaki anayeleta matokeo.

Inawezekana kwa kufikiri unataka kuchukua nyavu urudi nyumbani, Tweka Kilindini Bwana atakuonyesha na kukuongoza na kukufanikisha hapohapo ulipo.

Sikiliza na soma Neno la Mungu kwa bidii, Badilika.

Amua kutweka Kilindini, angukia miguuni  pa Yesu utapata vya kudumu.

Jizamishe ndani ya Neno la Mungu.

Kaa katika maombi mtu wa Mungu.

Je una mkakati gani wa kulijua Neno la Mungu.

Kwa Mungu hakuna kikomo ni wewe tu unavyojimimina, unaweza kufanya makubwa, Halleluya.

 

MUNGU ATUSAIDIE TUWEZE KUTWEKA KILINDINI, TUSIRIDHIKE TU NA WOKOVU ULEULE

No comments:

Post a Comment