Mwalimu Samwel Mkumbo |
Uhai wa kitu
chochote kile unategemea namna au jinsi mwenye huo uhai au aliyekabidhiwa
dhamana yuko katika hali gani, unaweza kulaumu juu ya uharibifu wa jambo au
mambo Fulani lakini kabla ya kulaumu angalia kwanza yeye aliyeharibu au
aliyekabidhiwa mikononi mwake yuko katika hali gani.
MATENDO
20:28 inasema hivi;
Jitunzeni
nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa
waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu
yake mwenyewe.
Sasa kabla
sijaendelea Zaidi nataka niseme jambo la msingi sana hapa, kichwa cha Somo letu
kinatuhitaji tuwe na ufahamu wa kuhakikisha kwamba kila tunachokiongea katika
somo hili ni mambo makubwa mawili, NAFSI YAKO NA KANISA LAKO. Wewe ni nafsi
moja katika kanisa, Je unayo kazi gani wewe kama Nafsi?
Unaweza
usijue wala usiliangalie kwa uzito, lakini inapasa kuelewa tafsiri hii;
KANISA ni Nafsi za watu zilizounganishwa
kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani wameijenga katika msingi wa
YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi zilizokubaliana za watu wengi wa aina
mbalimbali si kanisa maana ili wawe kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia
mamoja na kuwa na Imani moja ambayo hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.
TAZAMA
NAMI:
Ili kanisa
liwe na Nguvu na likae katika mstari unaotakiwa ni lazima nafsi za watu ndani
ya Kanisa ziwe ziko salama kabisa, yaani ziwe zimetunzwa katika hali ambayo
uhakika wa kundi kuishi kwa Amani utakuwepo kwa uhakika.
Labda
tuunganishe vipande viwili vya huo mstari wetu wa msingi ili uone jambo la
msingi kidogo….. Jitunzeni nafsi zenu,,.,.. mpate kulilisha kanisa lake
Mungu,.,.,..
Mfano wa
Mtumwa Mwaminifu
Bwana
akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana
wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri
mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia,
atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake,
Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake,
akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na
saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na
wasioamini (LUKA
12:42-46)
Sasa hapo ninataka nikufundishe jambo ambalo kimsingi
ambalo halipo kwenye Mistari hiyo hapo juu, na lenyewe ni juu ya adhabu
aliyopewa huyo wakili. Ona mtari huu;,..,.. akaanza kuwapiga wajoli wake,
wanaume kwa wanawake, AKILA NA KUNYWA NA KULEWA;,.,….
Maana suala
sio kusema bwana wake anachelewa ila baada kuona bwana wake anachelewa alifanya
nini? Na wala sio kuwapiga watumwa ila baada ya kuwapiga watumwa alifanya nini?
Yeye alichokifanya ni KULA NA KUNYWA NA KULEWA,..,..
Biblia
inaposema yeye ALIKULA NA KUNYWA NA KULEWA, maana yake aliacha kufanya
alichotakiwa kufanya lakini pia aliiharibu nafsi yake kwa MVINYO yaani kwa
Ulevi. Maana suala si kula na kunywa kwa sababu hayo ni mahitaji ya mwili wa
kila mtu, lakini suala ni KULEWA na biblia inasema KILEO HUDHIHAKI,. Na pia
HUPOTOA HUKUMU ZA HAKI.
MAANDIKO
KADHAA:
1 YOHANA
5:20-21 inasema
hivi;
Nasi
twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue
yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya
Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. Watoto
wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.
Sasa
ninatamani tuangalie jambo zuri kidogo katika mstari huo hapo, ya kwamba
msisitizo wa maneno ya mtume Yohana juu ya hayo aliyoandika haupo kwenye kutaka
kuwaeleza habari ya Kuthibitisha kuwa YESU AMEKWISHAKUJA, wala pia si juu ya
Habari ya kutaka kuwaeleza kuwa WAO WALIOAMINI WAKO NDANI YA YESU AMBAYE NI
KWELI NA MUNGU WA KWELI, lakini hayo yote aliyasema ili kuipa nguvu sentensi
yake ya mwisho ya kuwaambia JILINDENI NAFSI ZENU SANAMU.
TAZAMA NAMI:
Sasa tukianza
kuangalia maneno ya Yohana kabla hajatoa msisitizo wa kuilinda nafsi zetu dhidi
ya Sanamu, maneno yaliyotangulia kuna mahali yanatuelekeza;
Nasi
twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue
yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya
Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele………
Sasa kwenye
huo mstari nataka kwanza Ninyofoke na lile neno Nasi TWAJUA.,.. ikiwa na
maana kwamba hayo yatakayofuata au atakayoyasema YANATOKA KWENYE UFAHAMU au ni
UJUZI alionao juu ya Mungu, na Yesu Kristo mwana wake wa pekee.
Kwa hiyo
Yohana anaposema kule mwishoni ya kwamba JILINDENI NAFSI ZENU NA SANAMU, maana
yake JILINDENI NAFSI ZENU NA UJUZI AMBAO HAUTAELEZA JUU
YA HAYO ALIYOELEZA, kila KUJUA kusikokuonesha wewe ni
nani mbele za MUNGU ni wa kujilinda nao, ujuzi usiokuwambia habari ya dhambi
zako, ni wa Kujilinda nao, Ujuzi usiokuwambia ya kwamba dhambi zako zinaweza
kusamehewa kwa Damu ya YESU iliyomwagika pale Msalabani huo Ujuzi ni wa
Kujitenga nao, Ujuzi wowote usiokwambia kwamba unahitaji utakatifu kwa kiwango
cha juu, na uache dhambi zako, uache kukaa na wenye dhambi kama si suala la
kuwahubiria injili, ujuzi usiokwambia usikae mahali wanauza pombe, usiangalie
dansi, usiangalie watu watendao mambo ya aibu, usiweke chaneli mbaya zinazoweza
kuharibu watoto ujuzi usikwambia hivyo ni wa KUJITENGA NAO.
TAZAMA
NAMI:
Ujuzi wowote
unaokuja kwako unakuja kwa malengo makubwa yafuatayo, na ambayo ni lazima mtu
ujiulize kwa undani sana ili upate kuona ni nini iko nyuma yake…,..,.
Kupima
namna unavyojua au ujuzi wako au
ufahamu
wako juu ya jambo Fulani.
Mwanzo 3:1
inasema hivi:
Basi nyoka
alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.
Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti
yote ya bustani?
Ukitazama
msingi wa hilo swali kwa undani utagundua shetani alikuwa na majibu ya swali
alilouliza au alikuwa hana uhakika na majibu aliyokuwa nayo juu ya swali
alilouliza au alikuwa anataka kulinganisha majibu yake na ya Hawa kuhusu kile
anachofahamu juu ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa hiyo ALIKUWA ANAPIMA
HAWA ANAJUA NINI JUU YA MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA.
Basi Yesu
akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye
aliyenipeleka. Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja.
Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati!
Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? (YOHANA 7:33-35)
Ukitazama
namna swali la Wayahudi limekaa katika mtindo ambao wanajaribu kupima ufahamu
wa YESU kwa kuangalia ufahamu walionao wao, yaani ya kwamba YESU ana uhakika na
hicho anachokisema hapo.
Itaendelea…….
No comments:
Post a Comment