Tuesday, February 7, 2017

UNACHOKITAKA USIOGOPE KUKIPANDA, USICHOKIPANDA USITEGEMEE KUKIVUNA

Baada ya sadaka ya Nuhu, MUNGU aliweka order…………

Mwanzo 8:22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.

Hii ni kanuni rahisi lakini wengi hawajui kwamba impact yake ni kubwa… tena maandiko yanasema juu ya AINA YA MAVUNO INATEGEMEA AINA YA MBEGU MUNGU WALA USIJITAHIDI KUMDHIHAKI MUNGU MAANA IMEANDIKWA, Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Maandiko yanaonyesha kuwa ukipanda mema, tegemea kuvuna mema.. Wagalatia 6:9-10

Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

JE, UNATAKA NINI NA UNAPANDA KITU GANI? Tena maandiko yanaongeza Mathayo 7:12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. Hii ndiyo wengine wanaita kizungu WHAT GOES AROUND COMES AROUND

2 Wakorintho 9:10-11 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.

UZURI NI KWAMBA KILA MARA MUNGU ANAKUPA MBEGU PAMOJA NA MKATE… Kama wewe ni mkulima utaelewa ukivuna mwaka huu, halafu zote ugeuze msosi… cha kupanda wewe umekula… wakati wa mavuno utapiga miayo au kuomba kwa jirani…

Ukisoma 2 Wakorintho 9:10-11 usifikiri hiyo mbegu ni mahindi ila ni sadaka.. ndiyo maana mbeleni utajiri umetajwa pamoja na ukarimu… lakini pia 2 Wakorintho 9:12 Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu

Hizi shukrani Mungu anazipokea kwa sababu kuna watu wanamshukuru kwa sababu wamekirimiwa au wamefanyiwa ukarimu.

Mwaka 2004, nilinunua shati langu la kwanza dukani (kabla ya hapo nilikuwa nachagua mitumba sokoni), nilipofikisha chumbani kwangu nikasikia sauti ndani yangu (Iliyoambatana na amani isiyo ya kawaida) Hili shati ulilolipenda sana ulitoe kwa mtumishi wangu….. kwa kweli sikujua maana ya limbuko wala chochote kinachofanana nacho. Nakumbuka nilikuwa nimeanza kunyofoa pini.. nikarudisha nikampelekea aliyekuwa mwenyekiti wangu wa Fellowship enzi hizo


Tangu 2004 kama nakumbuka sawa sawa sijawahi kununua mashati Zaidi ya 10. MENGI NINALETEWA NA KUPEWA NA WATU

Wakati nimetulia nikajiuliza, hivi kwa nini watu hawaniletei suruali? JIBU NI KWAMBA, SIKUWAHI KUTOA SURUALI KAMA LIMBUKO… Apandacho mtu ndicho atakachovuna

Niko kwenye DIVINE SUPPLY YA MASHATI ….Yule mtumishi alinibariki kwa moyo mkuu…

Nikakumbuka, Paulo aliwaambia Wafilipi 4:19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Haya hayakuwa maombi kwa kila mtu…. (Ijapokuwa wakristo wengi wanapenda kuyakiri lakini bado wamepungukiwa) SOMA Wafilipi 4:18 PAULO anasema Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.

ALIWABARIKI Wafilipi 4:19 SAWA SAWA NA KILICHOPANDWA KWAKE Wafilipi 4:18

Je, unataka nini? Pesa? Nguo? n.k.... Jifunze kupanda unachokitaka kukivuna…. Mungu akusaidie ufanye kwa Imani na upendo….

PROPER GIVING ENDS STRUGGLES
Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

No comments:

Post a Comment