Amani ya Kristo iwe pamoja nawe mtu wa Mungu, Karibu katika makala haya yanayoletwa kwenu na Mwalimu Samwel Mkumbo ambaye ni Graduate wa Chuo Kikuu Dar es Salaam na alikuwa Coordinator wa Fellowship ya God Kingdom Business (GKB)
 |
| Mwalimu Samwel Mkumbo |
UTANGULIZI...
Lengo kubwa la somo hili ni kutazama ni vitu gani
ambavyo kanisa la Tanzania na Ulimwengu kwa ujumla linakosa kwa sababu tu
Kanisa halijachukua maamuzi ya kujua Asili yake na namna ambavyo MUNGU
analitazama Kanisa.
Na labda niweke wazi jambo hili ya kwamba si azimio
kubwa katika Somo hili kusema ASILI ya Kanisa kwa namna ya Historia ya kuzaliwa
kwake kwa kutaja miaka au labda matukio ya muhimu, la hasha! Japo tunaweza
kuangalia Historia kwa sehemu kidogo tu ikibisi kufanya hivyo ili kujua mambo
mengi zaidi.
Maana ninajua wapo wazee wetu wa Imani na wenye kuijua
Historia ya Kanisa la Tanzania na Ulimwengu kwa ujumla na wanafundisha hayo
hivyo basi Azimio kubwa ndani ya Somo hili ni kutaka Kanisa lijue Asili yake
kwa namna ya Uzao na Nafasi yake! Ndio! ASILI YAKE kwa kuangalia UZAO na NAFASI
yake.
SEHEMU YA KWANZA
Moja ya jambo ambalo MUNGU analitaka ni sisi watu
tuliookoka Kujua Asili yetu ndani ya Asili tuliyokuwa nayo. Yaani inapasa
tufahamu kuwa sisi ni kina nani tunatoka wapi na tunakwenda wapi, naam ni watu
wa shina na chipukizi gani?
Na mara kadhaa kwenye Biblia Mungu anataka na watumishi
wake wanafanya juhudi kutaka kutujulisha asili ya Kanisa, maana tunapoijua
asili ya Kanisa kuna mambo ya msingi tunayapata ndani yake na ambayo tusipojua
asili ya Kanisa hatuwezi kuyapata, na hayo mambo si kama ni ya ziada kwamba
tukiyapata sawa na tukiyakosa sawa, HAPANA! Ni mambo ya MSINGI na ni Muhimu
sana Kanisa likafahamu kwa upana wake hasa vijana ambao kesho na keshokutwa
ndio watakaokuja kuliongoza na kulilea Kanisa, ndio! Ni muhimu sana sana.
1 Petro 1:18 inasema
hivi;
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa
vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu
usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;