Mwalimu Samwel Mkumbo |
Hebu
tutazame mifano michache itakayonisaidia kukuelekeza mambo ambayo ninataka
nikuoneshe mtu wa MUNGU, katika mifano hii utaona mambo kadhaa ambayo
yatafungua ufahamu wako umuhimu wa kujua Asili ya Kanisa kwa kutazama Uzao na
Nafasi yake.
Habari
za Wana wa Skewa.
Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga,
nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa
na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya
hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu,
lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili,
akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na
kujeruhiwa. (Matendo 19:13-16)
Sasa
lengo kubwa si kukuonesha hadithi hiyo nzima, lakini kuna kipengele ambacho
hakipo hapo kwenye hiyo mistari na si kwamba kimesahaulika kwenye hiyo mistari
lakini hakipo kabisa, lakini nataka
nikitumie hicho hicho kipengele ambacho ukiangalia kwa undani hakipo ndicho
nataka nitumie kukufundisha hapo. Kipengele chenyewe ni MAJIBU YA WANA WA
SKEWA.
Maana
ukiitazama hiyo mistari haioneshi wana wa Skewa wakijibu swali waliloulizwa na
mtu mwenye Pepo, hata kidogo, na wala haituambii walishindwa kujibu wakakaa
kimya, wala haisemi kwamba waliguna au waliinama chini au walisema jambo hata
kama ni mioyoni mwao, ila Biblia inatuonesha kuwa baada ya yule mtu kuwauliza
kitu kinachofuata aliwarukia wawili miongoni mwa wale waliokuwepo, na
akawashinda nguvu akawaumiza lakini pia hakuwaacha waondoke hali wamevaa nguo
zao.
TAZAMA
NAMI:
Tuseme
kwamba hii ni kesi, na huyu mtu mwenye pepo ametoa Hukumu kwa wana wa Skewa, na
hukumu yenyewe ni ya kuwapiga na kuwaumiza na kuwachania nguo zao, kwa kosa la
kutaka kumtoa mahali bila ya ruhusa tena bila ya kuwa na mamlaka au hati ya
kumtoa lakini zaidi KWA KOSA LA KUWAULIZA SWALI NA WAO KUKOSA JIBU.
Tazama
tena:
Kwamba
huyu mtu mwenye pepo hana akili sawasawa ndio maana aliwapiga na kuwararua na
kuchana mavazi yao, kwa hiyo alifanya hayo kwa kuwa alikuwa amechanganyikiwa na
hivyo hata hilo alilolifanya alilifanya katika hali ya kutokujitambua kabisa.
Kimsingi
wana wa Skewa hawakuwa na Jibu la kumjibu Yule pepo kwa kuwa HAWAKUWA WANAJUA
WAO NI KINA NANI KATIKA HAYO MASHINDANO na ndio maana walikosa Jibu.
Lakini
biblia inatuwekea mambo kadhaa ambayo ni muhimu tukayapitia na kuyaangalia yanaweza kutupa mwanga wa
namna hiyo kesi ilivyoenda na kuona maana halisi ya kukupa mfano huu.
Kwanza
kabisa hata kama Wana wa Skewa hawakumjibu yule mtu mwenye pepo au katika
mahojiano yao Biblia haikuonesha ni nini wa Wana wa Skewa walijibu lakini
mwanzoni mwa maelezo ya tukio hilo Biblia inatujibu majibu ya swali alilouliza
mtu mwenye pepo.
Kimsingi
SIFA ZA WANA WA SKEWA ndizo majibu ya swali la yule mtu mwenye pepo
alipowauliza wao ni akina nani. Sifa za wa wana wa Skewa zimeelezwa kuamzia tu
ule mstari wa 13 biblia inasema hivi;
Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga,
nao ni wapunga pepo,….. lakini
pia kuna jambo ambalo linaoneshwa tena juu ya sifa za wana wa Skewa katika
mstari ule wa 14…. Walikuwako wana saba
wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo…..
Biblia
imetuonesha mambo kadhaa hapo juu ya sifa za wana wa Skewa, kwanza walikuwa ni Wayahudi, lakini walikuwa ni watu wa Kutanga-tanga, maana yake
hawana Kikao maalumu, hawana Imani thabiti mioyoni mwao, yaani hawana msimamo
wala haijulikani misingi yao wala dhehebu lao wanaloabudu, tena walikuwa ni Wapunga mapepo yaani ni kama Waganga wa
Kienyeji zaidi ya yote WALIKUWA WATOTO WA KUHANI MKUU. Nisikilize kijana
mwenzangu, nisikilize mtu wa Mungu kuwa mtoto wa mtumishi au kuwa mtoto wa
Mchungaji au Mke au Mume wa mtumishi, au Kusali Kanisa au Dhehebu Fulani sio
Tiketi hata kidogo ya kukufanya uwe mtu wa aina Fulani mbele za MUNGU au
shetani kama Hujaookoka.
Sasa
hebu pata picha mtu ameshakuwa wa Kutanga-tanga, tena wakati huo huo tunae
ibadani, akitoka au hata akiwepo Imani yake au mawazo yake hayapo, hayana
utulivu. Imani yake haieleweki, mtu kama huyo asitegemee kuijua asili yake
maana hajijui yeye ni wa kutoka wapi na anakwenda wapi ndio maana
anatanga-tanga kwa sababu mtu anayejua anakotoka na anakokwenda hawezi
kutanga-tanga.
Kwa
hiyo basi yule mtu mwenye pepo alipouliza swali, ni lazima wana wa Skewa
wanganyamaza kwa sababu wasingeweza kujieleza kwa kutumia Sifa zao, yaani
waseme ya kwamba sisi ni Wayahudi,
watoto wa Kuhani Mkuu, lakini kwa Upande wa Imani sisi ni watu wa
Kutanga-tanga, na kwa upande wa Huduma sisi ni Wapunga pepo. Hata kama
ungelikuwa ni wewe au ni mimi basi usingeweza kujibu swali kama hilo, lakini
pia wasingeweza Kuongopa.
Labda
tuseme wangesema wao ni watumishi wa Mungu aliye Hai na wamekuja kumuamuru yule
pepo atoke, Hakika WASINGEWEZA maana wangelikuwa WANAMDANGANYA SHETANI WAKATI
YEYE NI BABA WA UONGO. Hivyo wana wa Skewa wakanyamaza, maana hawakujijua wao ni wa Uzao gani na wana Nafasi gani…..
Itaendelea….
No comments:
Post a Comment