Hata Mungu anafurahi ndoa inapokuwa na furaha na raha |
Kwanza
nikuombe sana radhi kutorusha masomo haya kwa muda mrefu lakini sasa kwa uwezo
wa Mungu tutakuwa tunaendelea na masomo yetu kila wiki.
Kwahiyo
uweke katika kalenda na kumbukumbu zako kila siku ya Jumanne tutakuwa na masomo
haya….Karibu tuendelee..
Leo
naomba nizungumzie kitu ambacho ni muhimu sana kwa mahusiano na ndoa pia.
Unapojiandaa kuingia katika ndoa unapaswa kujiandaa jinsi utakavyokwenda kuishi
na mwenzi wako. Maana uhusiano unaouendea sio kama ule uliokuwa nao na Baba,
Mama, kaka, dada au bibi yako ni Zaidi sana mpendwa, unaingia katika uhusiano
wa karibu wa ndani mtu ambaye utalala naye kitanda kimoja kila siku na wakati.
Mwenzi wako wa ndoa ni mtu wa karibu hata kama hujisikii kumuona |
Mtu
ambaye iwe jua iwe mvua utakuwa unamuona.
Mtu
ambaye hata kama hujisikii kuongea na mtu siku hiyo atakuongelesha
Mtu
ambaye hata kama hujisikiaa kumuona atakuwepo hapo na utamuona
Ni
mtu ambaye lazima uwe naye karibu hata kama siku hiyo amekukwaza sanaa
Ndio
maana nikaona kuna umuhimu wa kuwa na masomo haya maana mengi yametokea kama
tunavyoona katika jamii sasa, talaka sasa inatolewa tu kirahisi rahisi tu,
zamani nilipokuwa mdogo kiukweli kabisa nilikuwa sijui kama kuna talaka huo
ndio ukweli wangu. Mungu alinipa neema ya kuwa katika mazingira hayo, sasa
nilipokuwa na nikawa mjini ndipo nikasikia hiyo sentensi lakini bado niliona
kama ni ya kundi fulani tu lakini nakuambia sasa inaogopesha maana imeingia
kanisani. Katika kutafakari haya Mungu akanipa mzigo huu niseme na nyie watu
wake kwamba NDOA BILA TALAKA INAWEZEKANA,Amen..
Haya
tuendelee na Somo letu sasa, kuhusu kuchukuliana ni hali ya kumuelewa mwenzako
pale anapofanya kitu ambacho hakikufurahishi au usichokipenda. Lakini
kuchukuliana sio kupuuzia au kudharau naomba nitofautishe maana wengi wanapuuza
au kudharau mambo wenzao wanayoyafanya hiyo nayo yaweza kuleta shida.
Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Mambo mazuri yanakuja..
Ukimchukulia
mtu utaona mazuri badala ya mabaya, utaona upande wake mzuri Zaidi ya ule
mbaya. Najua utaniuliza kuna mtu mbaya kweli? Ni kweli kabisa kila mtu ana
sehemu mbili za maisha ana upande chanya na hasi au ana upande wa mazuri na
madhaifu , kila mwanadamu ana pande zoote hizo wala usije ukafikiri ni wewe
mwenyewe.
Zamani
nilikuwa nasema nitaolewa na mchungaji maana wao ni watumishi wa Mungu hawana
shida, lakini hata awe askofu, Nabii, Mpwakwa Mafuta etc, ana pande mbili nzuri
na madhaifu maana yeye ni mwanadamu. Ni Mungu tu anatupa nguvu ya kushinda
katika madhaifu yetu.
Sasa
kama mwenzako atakuwa na kitu ambacho hakikufurahishi na umeshamwambia weee na
habadiliki ni jukumu lako Kumuelewa ,
Kumuombea na KUMCHUKULIA yaani hapo utakuwa na ndoa yenye ushindi hapa
duniani, furaha na raha zitakuwa ni sehemu ya maisha yenu, Amen..
Kama
mwenzako ana tabia za Ujeuri, mwelewe kwanza hii tabia imeletwa na nini maana
kuna wakati unaweza kuwa wewe ndio chanzo cha tabia mbaya kwa mwenzako, lakini
pia nyingine ni malezi aliyokuwa nayo.
Kuna
mtu ninamjua amelelewa katika familia yenye wakaka wengii sana, yeye akiwa
mtoto wa kike peke yake kwahiyo hata kuongea na vitabia fulani ni vya kiume
kiume, sasa mume atakayemuoa asipomuelewa huyu dada itakuwa ni mtihani maana
anaweza kuongea kitu cha kisela sela mume akaona hivi nimeoa mwanaume mwenzangu
au? Lakini atakapoelewa kwamba hii ni adhari ya mazingira mwenzi wangu
aliyokulia itakuwa ni faida kwa wote maana ataweza kumsaidia mwenzake na pia
atamchukulia pindi tabia ile ya kibabebabe na kisela inajiinua lakini
asipomuelewa hiyo ndoa itakuwa na shida sana.
Lakini
pia ukiona mwenzako anashindwa kukuelewa na wewe inabidi u-efatha (funguka)
mwambie mbona mimi naona kawaida kwasababu nilizoea kuongea hivyo na ndugu zako
sasa sikuwahi kuambiwa kama ni shida basi kama kwako ni shida nitaacha naomba
Mungu anisaidie.
Sasa
kama wewe unajifanya ni mtu wa sheria sheria unataka mwenzako atembelee katika
chaki utapata shida sana katika ndoa, kwasababu kwanza hakuna mtu aliye
mkamilifu na pili mwenzako ataishi kwa uwoga sana na wewe atakuogopa mnoo. Sasa
akikuogopa ni hatari kwa ndoa maana kuna mambo mengi ya muhimu yak wake
hutayajua na anaweza kujaribiwa kuwa na marafiki wa nje..
Kuna
mtu alisema yeye alilelewa katika mazingira ya mpangilio sasa alivyooa mke wake
akawa ni mtu ambaye kwakweli anaweka vitu hovyohovyo, sasa yule kaka akawa
anakwazika sana sana akawa anamwambia mwenzake wewe ni mtu wa aina gani unakuwa
haufanyi vitu kwa mpangilio? Mwenzake naye akawa anakwazika mbona huyu ana
Maneno makali mbona mimi nimekaa kwetu miaka 20 plus hakuna hata ndugu yangu
mmoja alinisema hivyo… sasa hilo swala likaleta shida kubwa katika ndoa hiyo,
kukawa hakuna maelewano ndani ya ndoa , ndio huyu mkaka kwa hekima ya Mungu
akajitenga akamuomba Mungu , ndipo Mungu akamfundisha kuchukuliana na mwenzake,
na ndoa ikasalimika. Niliweza kumuona akitoa ushuhuda hapa nimefupisha ila kuchukuliana
kuliokoa sana ndoa yao.
Kama
ndio mko katika uchumba anza kumuomba Mungu akusaidie uweze kuchukuliana na
mwenzako.
Namna
ya kujifunza Kuchukuliana na mwenzi wako;
Ili
kuchukuliana na wenzako iwe sehemu ya maisha yako unahitaji kujifunza kwa njia
zifuatazo;
1. Anza kuchukuliana
na ndugu zako, wadogo zako na jamaa zako
2. Chukuliana na
wanafunzi wenzako kama uko chuo
3. Jifunze
kuchukuliana na room mate wenzako kama uko chuo
4. Chukuliana na
wapangaji wenzako kama umepanga nyumba ya watu wengi
5. Chukuliana na
washirika wenzako kanisani
6. Jinfunze
kuchukuliana na wafanyabiasha wenzako
7. Popote ulipo
ukatukatana na mtu akakukwaza jitahidi kumchukulia
Ukijifunza
hayo utakuta umeifanya ikawa tabia yako yaani utajikuta unawachekea na
kuwafurahia wale wanaokukwaza na utaishi maisha ya ushindi ambayo Mungu
ametukusudia tuishi hapa duniani.
Halleluya
tukutane tena wiki ijayo katika masomo yetu haya ya Mahusiano na Ndoa, endelea
kututembelea lengo letu ni kuona watu wanaishi kama Mungu anavyotaka tuishi,
kwa msaada wa Mungu tunajua Ndoa na Mahusiano mazuri yanawezekana,
Haleluyaaaaaaaaaaaaaaa!!
Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Mambo mazuri yanakuja..
No comments:
Post a Comment