Fundisha watoto wako Kuomba
Mama na Binti wakiomba |
Maisha ya sasa yako soo demanding yaani yanabana sana kiasi kwamba watu wanakimbizana huku na kule ili kupata mkate wa kila siku.
Kama Mkiristo pamoja na changamoto zote lazima tusimame katika nafasi zetu.
Jambo la muhimu kwa watu wenye watoto ni kuhakikisha unafundisha watoto wako kuomba haijalishi wana umri gani,inapaswa umfundishe mtoto kuomba kuanzia hata hajazaliwa uwe unamuombea mara kwa mara,na akizaliwa uwe unaomba nae na kuendelea katika hatua zake za ukuaji anatakiwa aone familia inakaa pamoja na inaomba.
Maombi ya familia kwa pamoja yana maana sana kumjengea msingi mtoto,kama neno linavyosema hapo juu kwamba mfundishe mtoto njia atakayoiendea maana hataiacha atakapokuwa.
Akianza kuongea mfundishe kuombea chakula,na watu wote wanaoishi ndani ya nyumba yako unatakiwa uwatrain hivyo kwamba kabla watoto hawajala au kulala lazima waombe kwanza hiyo itageuka kuwa culture au utamaduni ndani ya nyumba yako na itawajenga watoto kujua umuhimu kwa kuomba.
Hata sometimes uwe unakwenda nae kwenye huduma mbalimbali za kuombea watu then anaona jinsi mtu anavyoombewa na mwisho anatoka na ushindi basi hapo mtoto atakuwa na picha ndani yake ya ukuu wa Mungu,atajifunza kukemea pepo na kuombea wagonjwa. Siku nyingine nitawaelezea experience your watoto kumuombea mtu na pepo likatoka.
Kama ikitokea wewe mwenyewe hujisikii vizuri au mwenzake anaumwa mzoeshe mtoto akuombee au amuombee huyo mtu anayepatwa na hiyo shida,basi hapo utakuwa unafanya training ya kuwaanda watumishi wakubwa wa kizazi kijacho….Najua kabisa Ibilisi hapendi lakini maneno ya Mungu katika Mathayo 19:26 Yanasema kwamba Kwa Binadamu Haiwezekani lakini kwa Mungu hakuna Lisilowezekana!
Faida za kumfundisha mtoto kuomba:
· Atakomaa na kukua Kiroho
· Atajengwa katika kusudi Mungu alilomuitia
· Ataweza kupambana na hila zote za Iblisi popote atakapokuwa
· Uhakika wa Ulinzi wa Mungu
· Kuja kuwa Mama au Baba bora
Mungu atusaidie tuweze kuwafundisha watoto jinsi ya kuomba,AMEN
Nakaribisha Mwenye cha kuongeza jamani tuweze kujengana……click comment utoe mchango wako
No comments:
Post a Comment