QUEEN MCHOMVU ....Gospel Singer
Wiki hii nimepata nafasi ya kuonana
na mwimbaji wa Injili aitwaye Queen Mchomvu
Kwakweli jinsi tulivyokutana
namshukuru Mungu tu aliniwezesha tunavyoendelea na mazungumzo utajua ni kwanini
nasema hivyo.
Mazungumzo yetu yalikuwa face to
face au uso kwa uso na yalikuwa hivi;
Blogger: Bwana Yesu asifiwe dada
Queen: Amen
Blogger: Wewe ndio ulikuwa unaimba
pale mbele enhee
Queen; Ndio
Blogger: Unaabudu wapi?
Queen: EAGT City Center na nimeokoka
Blogger: Amen
Blogger:Una album ngapi:Album 4 ,2 zimetoka
sokoni na video zake,2 ziko njiani,album zenyewe hizo hapo?
1.
Jehovah Masiah
2.
Maiti yaweza kuokoka
3.
Nashangaa
4.
Kibao kitegeuka
Blogger: Kwanini umeimba Maiti
yaweza kuokoka?
Queen:Kutokana na experince
niliyoipata tunavyokwenda kushuhudia watu wengine wanakataa wanasema hakuna
kuokoka duniani tutaokoka tukishakufa,ndio nikatoa huu wimbo kwamba kuokoka ni
hapa hapa duniani maana maiti haiwezi kamwe kuokoka tukisha kufa ni hukumu hakuna
wokovu.
Blogger: Historia yako kwa Kifupi ya
kuimba
Queen:Tangia mtoto mdogo sana,maana
kwanza nimezaliwa katika familia ya waimbaji baba na mama pia ni waimbaji,hata
kukutana kwao walikutana katika kwaya wakachumbiana na kuaoana kwahiyo unaweza
kuona wameniambukiza Roho ya uimbaji?
Blogger: Weee wewe ndio Queen wa Sunday School
ya Temeke? Mamaa Jamani kweli Mungu wa ajabu maana nilikuwa najiuliza uko wapi
nakumbuka sana ulivyokuwa mtoto mdogo sana ukiimba kwa ujasiri mkumbwa sana
mbele za watu ,sauti nzuri ,ulikuwa saa ingine unawekwa hata juu ya kiti ili
watu wakuone yaani Mungu wa ajabu ametukutanisha tena.
Blogger: Wimbo unaoupenda
Queen: “Njooni Tumwabudu” Kwasababu huu wimbo
niliupata siku niliyokuwa nakwenda kurekodi niliupata pale kwasababu huko nyuma
mtu aliyekuwa anitolee album yangu akanitapeli wala hakunifanyia kazi tena,ndio
nikakutana na mtu akajitolea kurekodi kwa gharama sawa na bure,kwakweli nilijua
ni Mungu na ndio nikaimba wimbo huu.
Blogger:Unaonaje Music wa Injili
hapa Tanzania?
Queen: Kwakweli umepiga hatua sana
na kwasasa una funs (washabiki) wengi sana tena wengine hata sio wa Imani
yetu,kwahiyo tunamshukuru Mungu
Blogger:Unatoa Ujumbe gani kwa
waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na
kujichanganya na mambo ya dunia hii
Queen: Kwakweli inasikitisha maana
wanatukanisha Jina la Mungu maana wao sio waimbaji tu ni watumishi wa Mungu,sasa
wanavyojichanganya wanafanya waimbaji wainjili waonekane kwamba ni wasanii tu
wakati ni watumishi wa Mungu
Queen akiwa amepozi |
Blogger:Zaidi ya kuimba ni kitu gani
kingine unafanya
Queen: Mimi ni Professional Hair
Dresser nimesomea kabisa na nina Saloon,pia ni mpambaji wa shughuli mbalimbali
Blogger:Ok Maisha Mengine Je
ninayopenda kusikia?
Queen: Ha ha Haa Nina niko single na
nina mtoto wa kiume anaitwa Prince ana miaka 11
Blogger: Hongera kwa Kukuza mpendwa
Blogger:Ujumbe kwa Waimbaji wa
Nyimbo za Injili
Queen:Tuwe na Umoja na kama tumeamua
kumuimbia Mungu basi tufanye kwa kumaanisha bila usanii wowote,maana Neno la
Mungu linasema
Blogger:Ujumbe kwa Jamii
Queen:Naomba Jamii ituombee sana
maana kwakweli kazi ni ngumu sana
Blogger: Amina,Asante sana Queen ,Mungu Akubariki nakutakia siku njema na utumishi mwema!
NIMEIPENDA SANA NYIMBO YA MAISHA MAUA
ReplyDeletenimeipenda sana nyimbo ya maisha ni kama maua asante
ReplyDelete