Waimbaji wakiendelea na mazoezi |
Maandalizi ya AFLEWO Tanzania yanaendelea vizuri
sana,weekend hii nilipata nafasi ya kuhudhuria katika mazoezi waliyokuwa
wakiyafanyia katika kanisa la World Alive,Sinza.
Wakienda sawa chini ya uongozi wa Music Director Pastor Sam |
Pia nilifanikiwa kuongea na Mwenyekiti wa maandalizi
aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Geoffrey Obiero,akisema kwa sasa wamepata
waimbaji wengi sana ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo kwasasa wamepata
waimbaji kutoka makanisa 32 ya hapa Dar es Salaam. Kwa mahesabu ya harakaraha
yawezekana wakapata waimbaji takriban 50 kama trend itakwenda kama ilivyo.
Kwa kifupi aliniambia AFLEWO ni kifupi cha “Africa
Lets Worship”,ambayo ilianzia Nairobi nchini Kenya ,na ina maono kuwa na usiku
mmoja wa Kuomba,Kusifu na Kuabudu katika Africa ifikapo mwaka 2017. Na maono
haya yanaonekana yatafikiwa maana nchi nyingi sana zimeshaanza AFLEWO na
nyingine zinaendelea kujiunga.
Kwa Tanzania AFLEWO ina walezi watatu (3) ambao ni
Bishop Deo Lubala,Pastor Abel Orgenes na Pastor Paul Safari.
Wanategemea kuanzisha katika miji mingine kama
Zanzibar,Moshi,Mwanza na kwingine kama mambo yataenda kama walivyopanga.
Music Director akiongoza kwa vitendo hapa si mwingine ni Pastor Sam |
Mwaka uliopita AFLEWO ilifanyikia CCC-Upanga na
ilihudhuria na watu takriba elfu sita(6000). Mwaka huu itafanyikiwa BCIC Mbezi
Beach kwa Mchungaji Gamanywa na wategemea kuwa na watu kama elfu 10 hivi.
Mwenyekiti wa maandalizi anawaomba watu wawe tayari
kupokea watakapokuwa wanamwabudu na kumsifu Mungu siku hiyo maana inakuwa ni
siku ya kuimba bila kukaa na itakuwa ni kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12
asubuhi,Wooow je mpendwa utatoka kweli pale kama ulivyoingia jibu ni hapana,jiandae
basi maana muda bado upo wakujiandaa na kizuri zaidi HAKUNA KIINGILIO.
AFLEWO 2013 Tanzania itafanyika tarehe 3 mwezi wa
tano mwaka huu.
Kwakweli waimbaji hao wamejitoa sanasana ili tu
kuifanya siku hiyo iwe ya kipekee ya kumwinua Mungu kwa njia ya Kuabudu
na Kusifu,maana nimeambiwa kwamba wanafanya mazoezi kuanzia masaa 8 hadi 10 kwa
siku,huko ni kujitoa kwa hali ya juu ambapo kama kuna mtu amejisajili katika
kikundi hicho na huduma ya kusifu na kuabudu haiku ndani yake atafika kipindi atakimbia
tu.
Wakimsikiliza Music Director kwa makini |
Niliweza kuona waimbaji kutoka vikundi na makanisa
mbalimbali wakiwa ni mojawapo ya kikundi cha AFLEWO Tanzania 2013. Upande wa
Vyombo nilimuona mtumishi mmoja ninayemuheshimu sana katika upigaji wa
Gitaa,yaani hiyo tu inaonyesha kwamba AFLEWO Tanzania 2013 haitakuwa ya
kawaida.
Nikamuona Music Director wa AFLEWO Tanzania 2013
Pastor Sam akifanya kazi yake kwa juhudi kubwa tena bila kuchoka ili tu
kuhakikisha kwamba AFLEWO Tz 2013 inajiweka vizuri ili siku hiyo watu wafunikwe
na wingu la utukufu kutoka Mbinguni . Maana tunajua neon linasema Mungu hushuka
katika sifa.
Mazoezi yao si ya sauti tu na viungo kidogo ili
kujenga staminina,kwakweli wanafanya kazi nzuri sanaa.
Waimbaji wakifanya mazoezi ya viungo pia kujimaarisha zaidi |
WOTE MNAKARIBISHWA na tuendelee kuombea maandalizi
.
No comments:
Post a Comment