Kama tunalivyokwisha kusikia yule muimbaji wa nyimbo
za Injili ambaye nyimbo zake zinawabariki wengi maana kwakweli nyimbo hizo huwa
zinashusha wingu la Bwana na kufanya muimbaji aingine triple p nikiwa na maana
Patakatifu Pa Patakatifu ambaye si mwingine bali ni John Lisu amesema
maandalizi ya kuizindua au kuiweka wakfu Albam yake mpya inayoitwa” Uko Hapa”
yanakwenda vizuri sana maana kila kitu kama ukumbi,mapambo ,waimbaji na
vinginevyo viko vizuri.
John Lisu aliyasema maneno hayo alipokuwa katika
mahojiano na Watangazaji na Ma-blogger wa Kikikristo,mahojiano yaliyofanyika
katika kanisa la DPC mwisho wa wiki iliyopita.
John Lisu |
John Lisu aliendelea kusema kwamba ana uhakika
kwamba uzinduzi huo utakuwa mzuri maana pia hajafanya kama mazoea bali wameomba
kumsihi Bwana Yesu ashuke na kuonekana siku hiyo.
Albam hiyo itakuwa na nyimbo kumi na moja (11),
anmeiita “Uko Hapa” kwasababu yeye
hajawahi kukaa na kuandika nyimbo hata siku moja bali anazipata akiwa amejitenga
akiwa anamuomba Mungu.Kwahiyo Wakristo tuna cha kujifunza hapa kama unataka
kumsikia Mungu basi utafute muda ujitenge utamsikia,Halleleya!
Katika Albam hii mpya John Lisu anaupenda sana wimbo
wa Fungua Macho,kwasababu ni wimbo wa maombi kwa Mungu.
Kwa kifupi John Lisu alianza kuimba akiwa na miaka 6
na ni mtoto wa Mchungaji,kwahiyo amekulia katika wokovu. Na alikuwa akiimba
sana katika mikutano ya baba yake Mchungaji Lisu,tena alikuwa pia akipiga na
gitaa. Mungu amempa huduma ya kuwaingiza watu katika uwepo wa Mungu kwa njia ya
nyimbo.
John Lisu ana mke aitwaye Nelly Lisu na mbali na
kuimba ni Mjasiriamali.
John Lisu na mke wake |
Mpaka sasa ana Albam moja ya Jehova Yu Hai ila kuna
nyingine ambayo ndio ilikuwa iwe ya kwanza lakini haikutoka na haijulikani sana
inaitwa“Tutakaribishwa Kwake aliitoa mwaka 2003.
Uzinduzi wa Albam ya Uko Hapa utafanyika pale CCC
–Upanga mkabala na Mzumbe University,Waimbaji wengine watakaohudumu siku hiyo
ni Pastor Paul Safari,Glorious Celebrations,The Voice,Bomb Johnson,Next Level
Team na wengine. Muda ni kuanzia saa 9 hadi baadaye na Kiingili ni shilingi
elfu tano (5000).
WOTE MNAKARIBISHWA
No comments:
Post a Comment