Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa
Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana jana majira ya adhuhuri hadi
kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa
na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za
Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.
Wanafunzi hao walidai kuwam, siku ya
Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni
kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume
walipovamiwa na kulawitiwa.
Majambazi hao wamekua wakidai wapewe
laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.
Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo
cha IFM alizungumza jana na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya
jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za
Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume
wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa
hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" ndipo
kamanda Kova aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni
kwenye Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova
aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
Kwa habari zaidi na picha soma www.wavuti.com
No comments:
Post a Comment