Joshua Ngoy Ngoy |
Blogger: Naomba majina
yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili
jamii iweze kukutambua kwa urahisi.
Joshua Ngoy Ngoy
Blogger:Umeokoka? na
unaabudu wapi
Nimeokoka;Ninaabudu
katika Kanisa la Rehoboth Victory Church-Arusha-Mianzini
Blogger: Historia yako
kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?
Nilianza kuimba tangu
nikiwa darasa la tano mkoani Singida kama Kiongozi wa Sifa na mpaka sasa naendelea
vizuri kwa uwezo wa Mungu.
Blogger:Katika kuimba
kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi
Nimeshatoa Album moja na ina nyimbo nane(8)
inajulikana kwa jina la BABA NAKUSIFU
Blogger: Wimbo unaoupenda
katika nyimbo zako
Napenda nyimbo zote ila
zaidi ni 'BABA NAKUSIFU'
Blogger:Ni kwanini
unaupenda huo wimbo/nyimbo
Napenda saana kumsifu
Mungu kwa mambo mengi alionitendea hasa kwa familia yetu
Blogger:Kuna mafanikio
gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili
Mafanikio niliyopata
uimbaji uninisaidia kufahamika kwa haraka sana na nimezunguka Tanzania hii na
njeya Tanzania pia nimepata marafiki wengi Waimbaji/Wachungaji na Watumishi
mbali mbali,
Blogger:Umekutana na
changamoto gani katika safari yako ya kuimba
Changamoto zipo nyingi tu
,unakuta nimealikwa sehemu kwa makubaliano maalum lakini ukifika hapo eneo
husika na baada yakumaliza icho ulichoitiwa unaachwa hewani bila kudhaminiwa
tena na makubaliano yanavunjwa bila kutarajia
Blogger:Unaonaje Music wa
Injili hapa Tanzania?
Kwa kweli Music wa Injili
hapa Tanzania kwa sasa uko vizuri tofauti kabisa na kipindi cha nyuma.
Unapendwa sana na Watu wa hapa (yaani wazawa) hata nchi jirani pia wameukubali
sana Music wa Tanzania.
Blogger:Na Unatoa Ujumbe
gani kwa waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine
wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii
Maoni yangu ni kwamba
wakumbuke kusudi la Mungu kwao maana wengi wanatamani kuwa kama wao lakini
hawakupata Neema hiyo kuwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili. Wawe makini maana
Biblia inasema tutafute ufalme wa Mungu kwanza na haki yake na mengine yote
tutazidishiwa.
Blogger:Zaidi ya kuimba ni
kitu gani kingine unachofanya
Mwana chuo
Blogger:Je kimaisha je
uko wapi? Umeoa au Hujaoa bado
Naishi na wazazi. Sijaoa
Blogger:Una Ujumbe gani
kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania
Nawasihi sana tuwe na
Umoja/Upendo/Mshikamano pia,tukubali mtu akifanya vizuri apongezwe sio
kunafikiana sisi kwa sisi.
Blogger: Una Ujumbe gani
kwa Jamii inayoburidishwa na nyimbo za Injili
Nawaomba sana kutusapoti
kwa kununua kazi zetu na hata tunapowaita kwa matamasha mbali mbali wasiache
kuja kujumuika nasi
Mtumishi wa Mungu Josh
Ngoy nakupongeza sana sana kwa Kazi Nzuri ya uimbaji unayoifanya ,Mungu akuinue
na kukubariki katika utumishi wako.
Kama wale waohitaji album
yake na kumsupport naweza kuwapa contacts zake kwa mawasiliano,tuwainue jamani
watumishi hawa wa Mungu.
MBARIKIWE SANAAAA
No comments:
Post a Comment