Monday, January 28, 2013

Rachel Scharp Muimbaji wa Nyimbo za Injili atoa wito kwa Waimbaji wa Tanzania kuwa wabunifu na sio kuiga kila kitu kutoka nje ya nchi


Rachel Mfinanga Sharp akisoma Press release

Mungu wa Ajabu Album


Rachel Scharp ni muimbaji wa Nyimbo za Injili anayeishi nchini Sweden,ni mtanzania aliyeolewa na raia wa Sweden.Mwisho wa wiki iliyopita alifanya hafla ya kuitambulisha Albam yake ya pili yenye Jina “Ni Mungu wa Ajabu”hapa Dar es Salaam,Tanzania.
Pastor Machibya akiweka wakfu albam ya Mungu wa AjabuKatika hafla hiyo iliyokuwa na wanahabari mbalimbali na waimbaji wa nyimbo za Injili kadhaa,Rachel alisema ameona ni vizuri aitambulishe albam yake nyumbani Tanzania na pia video yake ameirekodia hapahapa nchini,mkoani Arusha chini ya UMU Production katika uongozi wa Jojo Jose Mwakajila,hii video imerekodiwa pia maeneo ya Sweden(Malmo),Berlin Ujerumani,Bagamoyo,Serengeti na Moshi.  Ametumia zaidi midundo ya kiutamaduni  na ametumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza pia.
Rachel na mama yake
akimtambulisha mdogo wake
 

Rachel alisisitiza kuwa soko haliko nchi wanazoongea Kiswahili tu bali hata mataifa mengine wanapenda nyimbo za Kiswahili na za kiutamaduni,na yeye anajivunia sana Kiswahili.
Upendo Kilahiro alikuwepo na alituburudisha kweli
 
Akatoa wito kwa waimbaji wa nyimbo za Injili wasipende sana kuiga mahadhi ya nchi za nje maana ameona wengi wanaiga sana mapigo ya Afrika ya Kusini wanataka kuwa kama Joyous Celebration,lakini wanasahau kwamba zile ni nyimbo zenye asili ya kwao za utamaduni wao. Watanzania tunapoiga zile tunapoteza identity maana ikipigwa watu watajua ni wa sehemu nyingine sio wa Tanzania. Lakini kama tutachukua mahadhi ya Mdumange,mdundiko,sindimba,lizombe likaboreshwa itakuwa nzuri na mtu akisikia atajua tu huu ni wimbo kutoka Tanzania.
Mungu ni wa ajabu hewani
 
MC,The Comedian,The King Chavala akitafakari jambo

Rachel safari yake ya uimbaji ilianza akiwa mdogo na alishawahi kuimba kwaya za Msewe Lutheran Fellowship,Jangwani  Secondary na sasa anaimba kwaya huko Malmo Sweden na ni kiongozi wa sifa na kuabudu katika kanisa la Elim Pentecostal .

Ana watoto wawili wa kiume.

Wanahabari na Mablogger mbalimbali;


 

Papaa ze Blogger,kwa mbali namuona Furaha MasinAlbam ya Rachel inasambazwa na UMU Production,Arusha

 

No comments:

Post a Comment