Frida Brown Muimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania |
Naitwa
FRIDA BROWN LEKEY, lakini huwa napenda kutumia majina mawili ya kwanza yaani
FRIDA BROWN
Blogger:Umeokoka na unaabudu wapi
Nimeokoka,
Yesu ni Bwana katika maisha yangu..Naabudu Kanisa la Imani Hai (a.k.a Winners
Chapel) Ukonga – Banana, Dar es salaam
Blogger: Historia yako kwa Kifupi ya
kuimba,yaani ulianzaje na wapi?
Nimeanza
kuimba tangu Sunday School pale Kurasini Lutheran Church, Then nimeendelea
hivyo nikiwa Ukwata (A-Level), Praise team pale Chuo cha Uhasibu Arusha. Na
mara nyingi nikiwa nyumbani, Kazini uwa napenda sana kuimba.
Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa
Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?
Naamshukuru
Mungu kwakunifanikisha kutoa Album ya kwanza katika kuimba kwangu yenye nyimbo
nane(8). Jina la Album ni TEMBEA NA YESU
Mmh
nazipenda nyimbo zote kwakweli,. zaidi sana Eligibo Mungu Mwenye Nguvu..
Blogger:Ni kwanini unaupenda huo
wimbo/nyimbo
Eligibo ni
wimbo unaoeleza Majina ya Mungu kwa Lugha ya biblia na maana zake,.Ni wimbo
wakuabudu na ninapoimba unanisogeza karibu na uwepo wa Mungu. Hakika Mungu wetu
ni Eligibo
Blogger:
Nani anasambaza kazi
zako? Je anakusaidia vizuri?
Kwasasa sina msambazaji, nauza CD mwenyewe ila
nafikiria kutafuta msambazaji wa hii kazi
Blogger:
Kuna mafanikio gani
umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili
Mmh
mafanikio yapo ndani ya Roho yangu na Maisha yangu ya Wokovu.. Album hii
imekuwa mlinzi wa Maisha yangu kwamaana inanikumbusha ‘’Usiwahubirie wengine
alafu wewe ukakataliwa’’. Kwakifupi inanifanya nisonge mbele
Blogger:
Umekutana na changamoto
gani katika safari yako ya kuimba
Changamoto
kwakweli zipo unapopiga hatua yoyote ya mafanikio maishani lakini kwa upande
wangu Kibali cha Mungu kilinifunika toka nimeanza kurecord mpaka sasa,kwakweli
namshangaa sana Mungu wangu..To him be all thy Glory
Blogger:
Amen, Unaonaje Music wa
Injili hapa Tanzania?
Kwakweli
Umekuwa sana kwa maana yakuwa na wasikilizaji wengi.
Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji
wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na
kujichanganya na mambo ya dunia hii
Kila
muimbaji aifanye Album yake kama Mlinzi wake kwamaana yakufananisha anachoimba
na matendo yake. Mwisho wasiku Nimaombi yangu Mungu atusaidie sana kutenda
sawasawa na Neno lake.
Blogger: Zaidi ya kuimba ni kitu gani
kingine unachofanya
Nimeajiriwa
kama Mhasibu katika kampuni ya Mtu Binafsi.
Blogger:
Hongera sana Frida,kumbe unaweza kumtumikia Mungu hata kama unafanya
kazi,unafundisha jamii kitu hapa maana wengine wanatingwa na kazi tu hawafanyi
chochote kwa ajili ya Mungu,enhee tuendelee…Je kimaisha je uko wapi? Umeolewa
au bado? Watoto wangapi?
Naishi
Mikocheni B - Dar es salaam, Sijaolewa
Blogger:
Una Ujumbe gani kwa
Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania
Tuombeane,
na kila mmoja awiwe ndani yake kumsaidia, Kumwinua mwingine kwa namna moja au
nyingine. Uimbaji wetu sisi sio wamashindano bali ni katika kuujenga mwili wa Kristo
hivyo basi Tufanye uimbaji Huduma na si vinginevyo
Blogger:
Amina,Una Ujumbe gani
kwa Jamii inayoburidishwa na nyimbo za Injili
Kwakweli
nawashauri wasiwe wasikilizaji wa Nyimbo tu bali watendaji wa jumbe mbalimbali
wanazozisikia.
Blogger:Asante sana kwa Muda wako,Mungu
akubariki na kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu.Amen
Ukihitaji
CD ya Frida Brown,tuwasiliane nitaweza kukupa mawasiliano yake.
To God be all thy Glory....Congratulation Frida,.MUNGU wa mbinguni akuinue zaidi na zaidi,.
ReplyDeleteNimependa sana majibu ya mtumishi huyu. Mungu azidi kumtumia kwa unyenyekevu sawa na majibu yake. MUNGU AKUBARIKI FRIDA.
ReplyDeleteNilivyoisikiliza CD yako na wewe alivyo ni jambo ambalo mungu amekutendea maajabu katika uimbaji wako.Uokovu wako usirudi nyuma "hongera sana Frida mungu aendelee kukuongoza na kukubariki Amina"
ReplyDeleteUbarikiwe sana mdogo wangu mungu aendelee kukupa upako wa kipaji hicho cha uimbaji... by GEORGE.
ReplyDeleteHongera sana mwanangu!
ReplyDeleteManeno yamejaa hekima.
Mungu akuongoze daima.
Mungu wa Oyedepo na akutunuku kibali.
Charls
Hongera dada yangu mungu azidi kukuinua ubariwe sana by Haika Lekey
ReplyDeleteAmeeen Mdogo wangu... kwa MUNGU kila kitu kinawezekana...
DeleteMungu awabariki wote...Aminaaa Pst.Charls,. nitazidi kunyenyekea kwa yeye aliyeianzisha safari hii nikijua atanikweza kwa wakati wake, Tuzidi kuombeana tu....by Frida Brown
ReplyDeleteYani sitaacha kusema kila nipatapo nafasi..Frida album yako inanibariki sana. Yani ndo CD yangu kwenye gari na mara nyingine huwa natamani hata nisimame humo ndani na mara nyingine napiga hata makofi. Kwakweli ubarikiwe sana na Mungu azidi kukuinua. Colle
ReplyDeleteAsante sana dada yangu Colle..namshukuru Mungu sana kwa muujiza huu,.Endelea kuniombea Mungu azidi kunitumia kama apendavyo kwa utukufu wake..
DeleteHongera sana Frida mungu akubariki by Dorothy UK
ReplyDeleteThx my School mate..
DeleteHongera sana Frida mungu akubariki by Dorothy UK
ReplyDeleteHongera sana Frida mungu akubariki by Dorothy UK
ReplyDeleteHONGERA sana my dear.. CD yako nzuri sana imenibariki...Mungu azidi kukuinua.
ReplyDeleteits me MARIEDO
Thx sanaa mdada..Glory to GOD
DeleteHongera sana Frida, Nyimbo zina mafundisho mazuri sana. Mungu akuzidishie neena kwa kazi nzuri unayofanya.
ReplyDeleteJ.P.
An unexpected blessing
ReplyDeleteis always the best gift!
Congratulations
by fa2 MDC
UPENDO UWE NGAO YAKO!!
ReplyDeleteMUNGU AKUSIMAMIE MDADA,
NAFARIJIKA MNO,NAOMBA CD 15 IJUMAA
BEI YAKE NI SHILINGI NGAPI?
MAMA BONY (FTR)
Ni shilling 5,000 tu mama Bony,.my No 0715 889271 psee ni sms.. Mungu akubariki
Delete