Friday, April 19, 2013

Vitu muhimu vya kuangalia unapojiandaa kuwa na mwenzi wako wa Maisha-Part III

 
Leo katika somo letu la Vitu muhimu vya kuangalia unapojiandaa kuwa na mwenzi wako wa Maisha,nitaendelea ka kipengele cha kuendelea kujiangalia mwenyewe kwanza.
Nimeona ni vizuri nianze na msisitizo wa kujiangalia mwenyewe kwanza, maana watu wengi wamejikuta matatizoni katika ndoa kwasababu walitegemea vitu vikubwa sana kutoka kwa wenzi wao wakati wao wenyewe hivyo vitu hawana. Sasa ili kuwa salama na kuwa na ndoa yenye ushindi ukijishughulikia mwenyewe utajikuta una suluhisho na utaweza sana kumchukulia mwenzio na utakuwa na mtazamo chanya kwamba au mimi ndio sijafanya sehemu yangu vizuri nini.
Leo nitaongea jambo moja muhimu ambalo ni muhimu sana na litakusaidia sana kuja kuwa na ndoa yenye ushindi na ushuhuda,tuendelee…..
 
Uaminifu
Uaminifu ni hali ya ambayo mtu anakuwa nayo inayomfanya awe mkweli na asiyepindisha mambo,anayependa mambo yaliyonyooka bila kusema uongo.
Katika Biblia ukisoma katika 1Samuel 16: 17-19 utaona jinsi ambavyo Mungu anaangalia uaminifu,na jinsi ambavyo mtu akiwa mwaminifu anaweza kupata fursa.
 
Kwa kusoma neno hili ukiwa kama bwana au bibi harusi mtarajiwa au mtarajiwa iko haja ya kujiandaa na kujitengeneza kuwa mwaminifu mpendwa,kabla hujaingia katika mahusiano hebu jichunguze hivi mimi ni mwaminifu kweli katika njia zangu? Maana wapendwa wengine sio waaminifu anatoa taarifa zake za uongo kabisa kwa mwenzi wake.
Cha kwanza kabisa kuwa mwaminifu mbele za Mungu wako,kwa kuwa na njia zilizonyooka,nawaambiaga watu kaa mkao wa kuoa au kuolewa.


Sio unakuwa umeingia kwenye mahusiano a kumbe huku nyuma yamkini ulikuwaga na mahusiano b,basi kwa siri sana unaendelea kuwasiliana na huyo mtu na kutoka out na vitu kama vile,unajitetea we are good friends,what? kwakweli unapoanza kuingiza hii style maana mtu ambaye yuko serious anayetaka kuwa mwenzi wako atakuwa anafuatilia mwenendo wako mara anagundua kwamba kuna miungu ambao uko nayo bado,utakachokiona ni action tu simu hazipokelewi,meseji hazijibiwi na sababu zinaanza unajua mimi kwetu hatutakiwi kuoa ooh blah blah kumbe kashakujua una njia mbimbili.
Tulia mpendwa acha kuahangaika, neno la Mungu linasema katika Warumi 12:2 “Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu”
Amen ,Haleluya wapendwa katika bwana,neno la Mungu liko wazi usiwe kama mataifa maana wao ndio style zao hizo kuwa na njia mbilimbili na tumeona kumekuwa na madhara mengi sana kwa njia hizo,sasa kwasababu sisi ni viumbe vipya twaweza kushinda yote na kusimama kwa ujasiri na kusema hapana kwa vitu ambavyo vitatuharibia uhusiano wetu na Mungu,Amen!
Futa hizo namba za simu ambazo unaona zitakuletea matatizo,acha yote nakuomba sana usiwe kama mtu ambaye hamwamini Mungu ndio anakuwa na watu wengi ili asije akapoteza bahati,kwa Yesu hakuna hiyo yeye ni kweli na amina,akisema atakupa mwenzi atakupa tu hata kama ni katika late 50s mwamini yeye na neno lake.
Watu wengine wanaficha sanasana mambo yao sasa ikatokea mwenzi wake akija kujua huko mbeleni ooh kasheshe maana atajiuliza ni vitu vingapi hujamwambia? Enhee?
Mpendwa usiogope kuwa wazi hutampoteza mwenzi kwa kumwambia ukweli na kama atakimbia kwasababu umemwambia kwamba una mtoto,au watoto,au ulikuwa katika mahusiano fulani,basi hakuwa wa kwako maana angekuwa wako angechukuliana nayo.
Yawezekana wewe ni dada au kaka unasoma hapa sasa na kuna mtu alikusaliti akakubagua kwasababu ulikuwa mkweli ukwambia kuwa una background a,b,c,d,usikate tamaa waka usibadilishe hiyo haiba yako ya kuwa mkweli mpendwa wangu,simama katika Uaminifu tu maana Neno la Mungu linasema Mungu anaangalia uaminifu na kwa huo huleta fursa,soma kwa utulivu kabisa Mistari hii 1Samuel 16: 17-19 na Zaburi 75:7.
Iko fursa inakuja kwa uaminifu wako mpendwa ambayo inakwenda kukupa ndoa yenye Amani na Upendo,Halleluya.
Kuna nguvu kubwa kuwa mwaminifu sana maana inakuweka huru,tafuta sanasana kuwa mwaminifu na Mungu wangu wa Mbinguni akusaidie uweze kusimama katika huo,hata kama utachekwa wewe ng’ang’ania kuwa mwamiminifu.
Kitu chochote ambacho unahisi au kuona kwamba hiki mmh lazima nikiseme mapema,usisubiri mtu ameshakuvalisha pete au umemvalisha pete na mahari mmeshatoa au kupokea hapana sio vizuri maana utakuwa umemlazimisha kuamua. Mapema kabisaa ukiona huyo mtu anakuja kwa nia ya kutaka kuwa pamoja na wewe na una uhakika kwamba yuko serious mweleze mapema ili aamue ataweza kukubeba au hawezi.
Ila tahadhari katika hilo sio kila mtu akikuambia dada nakupenda unamwambia ,Amen ila mimi nina background a,b,c,d wee utafedheheshwa mpendwa  wangu watu wengine sio waaminifu na mambo ya watu,mpaka uione nia yake ya dhati isije ikawa anapita tu.
Na kwa uaminfu huo mwenzako atajua kweli kuwa nimempata mtu ambaye najua hatanificha mambo yake kwamba tutaishi kwa ukweli na uwazi.
Zaidi sana kwasababu Mungu wetu anaangalia moyo na anapenda moyo wenye uaminifu basi atakupa haja ya moyo wako maana anaona kwamba hutaliabisha Jina lake maana huna ajenda za sirini.Amen ,Jina la Bwana libarikiwe sana.
 
Tutaendelea tena wiki ijayo,
 
Weekend Njema tafakari na anza kufanyia kazi

No comments:

Post a Comment