Friday, April 5, 2013

Wajue New Jerusalem Brothers ,waimbaji wa nyimbo za Injili wanaokuja juu na mtindo wa "Akapella" nchini Tanzania


New Jerusalem Brothers waimbaji wa Injili kwa mtindo wa Akapella nchini Tanzania

Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa urahisi.
New Jerusalem Brothers Tz

Blogger:Umeokoka na unaabudu wapi

Yaap sisi tunampenda Mungu sana kuliko chochote ndo mana tuna mtumikia kama vijana

Blogger Historia yako kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?

Kikundi chetu kilianzishwa mwaka 2007 kikiwa na watu watatu ila mpaka sasa tupo sita

Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?

 Yaaaaaaap tuna album yetu mpya inayojulikana kwa jina la nitamsifu bwana ni mpya bado haijaingia sokoni bado.
New Jerusalem Brothers katika perfomance

Blogger: Wimbo unaoupenda katika nyimbo zako

Nyimbo ziko nane siunajua sisi nikikundi kila mtu atachagua ya kwake ila wimbo ambao tunaupenda sana unaitwa Yesu wangu


Blogger:Ni kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo

Ni wimbo unaotugusa sani unatuonesha nini ambacho bwana yesu alifanya lakini unatupatia tena matumaini kuwa pamoja na kuteseka kwake tutamuona tena

Blogger:Nani anasambaza kazi zako? Je anakusaidia vizuri?

Kwa sasa bado hatujapata msambazaji wa kazi yetu bado

Blogger:Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili

Mungu amekuwa akifungua njia hasa kwenye masomo yetu lakini pia tumeweza kufikisha

ujumbe kwa watu walio kata tamaa wa aina mbalimbali

Blogger:Umekutana na changamoto gani katika safari yako ya kuimba

Kukatishwa tamaa na watu mbali mbali pia tatizo kubwa la kifedha na kutoweza kufikia au kufanya kutimiza malengo yetu kwa wakati

Blogger:Unaonaje Music wa Injili hapa Tanzania?

Muziki wa Injili umekuwa kwa kasi sana na pia naona watu wanazidi kubalikiwa kwa njia mbalimbali
NJB

Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii

Hii ni kazi ya mungu wala si ya mwanadamu yawapasa kum kumbuka Mungu sana pia wawe watu wa maombi sana kwa sababu shetani afurahi so wawe makini sana

Blogger:Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unachofanya

Huwa tunapenda sana kucheza mpira kwa sababu wengi wetu ni wachezaji wa mpira na pia huwa tunapenda kuwafundisha wengine habari za Mungu

Blogger:Je kimaisha je uko wapi? Umeoa au Hujaoa bado? Watoto wangapi?

Hatujaoa


Blogger:Una Ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania

Wa muweke Mungu mbele kwa sababu yeye ndie kila kitu katika maisha yetu

Blogger: Una Ujumbe gani kwa Jamii inayoinuliwa,kufundishwa na inayoburidishwa na nyimbo za Injili

Yale tunayoimba wayachukue na kuyafanyia kazi wasiishie kusikiliza tu yawe kama msingi katika maisha yao

 

1 comment:

  1. Valuаble infoгmation. Luckу me I ԁiscovered your websitе unintentionallу, аnd I am surpгised why thiѕ
    accident ԁid not took place eаrliеr!
    Ӏ bοokmaгked it.

    Havе a look аt my homepage :: http://members.f7social.com

    ReplyDelete