Thursday, April 11, 2013

Vitu muhimu vya kuangalia unapohitaji au kujiandaa kupata mwenzi wa wa Maisha-Part II


Watarajiwa hao
Leo tutaendelea na somo letu la uchumba hadi ndoa,tunaendelea kuangalia vitu muhimu ambavyo mtu anatakiwa kuangalia au kuvifanya anapojindaa kupata mwenzi wa maisha.

Katika somo lililopita tuliangalia vitu ambavyo mtu anatakiwa kujifanyia mwenyewe,na tuliangalia vitu muhimu vitatu ambavyo ni maombi,kuangalia kama wewe ni mtu sahihi ambaye kweli unaweza kuishi na mtu mwingine na uhusiano wako binafsi na Mungu ukoje.

Kabla sijaendelea mbele naomba kukolezea katika swala la uhusiano wako na Mungu,mara nyingi nimeona na kusikia wadada au wakaka wanataka wapate watu ambao wana uhusiano mzuri na Mungu wakati wao they are far from  it,yaani hawana uhusiano mzuri na Mungu .

Uhusiano ninaosema hapa sio kwenda kanisani wapendwa au kwenye tamasha,au kuwa na urafiki na waimbaji wakubwa au watumishi,ninamaanisha ule ushirika wako na Mungu umekaaje? Je Mungu ni rafiki yako? Je ni baba yako? je unawasiliana nae kwa kiasi gani,ukipata crisis tu au wakati ukienda kanisani tu? Kama uko katika kundi mojawapo hapo juu nakusihi kwa Neema ya Mungu ubadilishe mtazamo wako mpendwa maana uhusiano wako na Mungu ni muhimu sana kukupeleka katika mustakabali wako ambao Mungu amekuwekea hapa duniani.

Lakini kama utakuwa na mahusiano hafifu na Mungu kwakweli mpendwa mambo yako mengi hayatakwenda sawa,matokea yake utaweza kuchukia wokovu kumbe wewe mwenyewe ndio mchawi wa maisha yako.Anza leo soma neno,omba,abudu na jishughulishe na mambo yake nayeye atajishugulisha na mambo yake.

Hilo jambo la mahusiano ni jambo ambalo lilinifanya niweze kufikia mustakabali na kweli naweza kusema yeye ni Ebeneza na hata ninao wengi ninawajua wamefanikisha kuwa katika mahusiano Mungu aliyekusudia kwasababu walikazana sana kumkaribia Mungu,na Mungu aliweza kuwaepusha na mitego mibaya akawakutanisha na wenzi aliowakusudia kwao.

Katika somo lililopita nilizungumza juu ya kuwa na mtu mmoja wa karibu unayemwamini awe prayer partner wako ni muhimu sana maana hata neno linasema Katika Mathayo 18:20 “Walipo wawili au watatu kwa jina langu ,nami nipo katikati yao”. Katika Kiswahili kuna msemo unasema kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Ukiomba na mwenzako unapata nguvu,mnatiana moyo wa kuendelea mbele zaidi na zaidi,kupeana shuhuda,kwa kifupi hutachoka na utaona Mungu akijibu maombi kwa njia ambayo utamshangaa si katika swala na mwenzi wa maisha tu mambo yote.

Baada ya hayo naomba niendelee na mambo mengine ya kuangalia;

Kwanini nataka kuoa au kuolewa

Yakupasa ujiulize swali hili hivi mimi kwanini nataka kuolewa au kuoa,ni kwasababu wenzangu wa rika wameolewa au kutoa nuksi,nawakomesha maadui zangu,na mimi niwepo tu kwenye kundi au mengine yanayofanana na hayo?

Kama hizo hapo juu mpendwa naomba kaa chini angalia kwa mtazamo mpya kabisa,ujue ndoa ni nini,Mungu anaionaje ndoa na anataka iweje,na inakwenda na gharama gani? ni vitu gani nitahitajika kuachilia kwa ajili ya hiyo ndoa ninayoiendea? je kila rafiki niliye naye anafaa kuendelea kuwa rafiki nikishaingia katika ndoa? maana wengine marafiki wameharibu ndoa wanawashauri wenzao vibaya.Siku hizi watu wana makundi ambayo ndio yanawaongoza kila kitu,Je hilo Kundi lako ulilo nalo hilo unavyoliangalia angalia kweli utaweza ndoa kwa kuwa nalo? Utamweshimu mwenzako kw akuwa nalo kweli? Makundi mengine ni ndugu? Utaweza kusema hapana baadhi ya vitu kwa sababu ya hiyo ndoa unayoindea? Sio unasema yaani mimi kwakweli lazima kila siku niende kwa wazazi wangu? Enhee na huko nyumbani kwako utaenda saa ngapi mpendwa wangu? Hebu jipime?

Angalia pia Je kazi hii ninayofanya inaendana na ndoa? Kuna mtu alibadili kazi baada tu ya kuolewa maana kazi ya kwanza alikuwa anatoka saa 4 usiku kila siku akatafuta ambayo atatoka mapema apate muda na mwenzi wake,ndo gharama hizo.

Ila katika yote Mungu anatuwezesha tunaweza kushinda vikwazo kama tutamkabidhi yeye aliye mweza wa Yote.

 

Tutaendelea ndio kwanza tuko Part II……………..

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment