Karibu katika somo hili la Uchumba hadi ndoa, kama wewe
ni mgeni katika masomo haya karibu sana naomba upitie katika mtiririko wa
masomo ya nyuma utajifunza mambo mengi ya muhimu.
Leo naleta kwenu somo hili muhimu la umuhimu wa
kuhakikisha mwenzi wako anajali malengo na ndoto zako.
Kabla hujaoa au hujaolewa ulikuwa na malengo na ndoto
zako za maisha kwamba unaona kabisa Mungu amekuita uwe labda Mchungaji,
Mmishionari, Mwinjilisti,Mfanyabiashara,Mkulima,Mshauri nakadhalika
nakadhalika, sasa hayo maono yako ndio huduma yako ambayo umeitiwa na Mungu
hapa duniani kwahiyo huna budi kuyafikia. Utauliza mfanyabishara inawezaje kuwa
wito, ni wito kabisa maana unatoa huduma kwa jamii kwasababu usipotengeneza
unga wa ugali Mungu atakuuliza niliweka maono hayo ndani yako watu wamekufa na
njaa kwasababu hukufanya sehemu yako.
Au jamii ikakosa nguo za kujisitiri hautajisikia vizuri
kwasababu unajua kabisa hapa nilipaswa nihudumie jamii kwa huduma ya kuuza
nguo.
Kila shughuli Halali ambayo Mwanadamu anaifanya inakuwa
na Baraka za Mungu maana hata tukiangalia katika Biblia watu walikuwa na
Shughuli mbalimbali tumchukue Petro Yesu alimkuta katika shughuli zake za Uvuvi
wa Samaki ndipo akamwambia amfuate atamfanya mvuvi wa watu.
Pia kama mtu umeitwa kuwa Mchungaji, Nabii, Mtume au
Mshauri usipofanya ujue kuna watu wakifa bado hawajampokea Kristo utakwenda
kuulizwa kwanini kuhumuhubiria, au mtu akakata tamaa akajiua utaulizwa kwanini
hukumtia moyo wewe mshauri.
Kwahiyo Malengo na Ndoto zako ambazo unazo ziheshimu
sana sanaa kwasababu sio mtu au mkuu wa ukoo wenu, bibi, babu yako ameweka
ndani ya ni Mungu amekubariki nazo, kwasababu hiyo angependa kuona zinatimia
bila kutoa sababu yoyote, anakudai.
Unapokuwa umepata mwezi wa maisha mshirikishe ndoto
zako ili ajue yuko na mtu wa aina gani na wewe utapata nafasi ya kujua mawazo
yako juu ya hizo ndoto kwamba anazijali au ataziua.
Kuna mpendwa alimshirikisha mwezi wake ndoto zake
wakiwa tu katika hatua ya uchumba akamwambia nina ndoto ya kuwa kitu fulani
kwahiyo inanilazimu nikasomee Shahada ya Uzamili, yaani yule mwezi alikuja juu
akasema mimi sitaki kabisa mke mwenye kusoma soma na kufanya shughuli shughuli
nataka akae nyumbani aangalie watoto na nyumba yaani ikawa kasheshe kweli.
Sijui waliishia wapi ila yule dada yeye alikuwa na ndoto na huyu mwezi
hakuijali kwasababu yeye alikuwa na matakwa yake, labda yule dada yeye angekuwa
na ndoto ya kutofanya chochote nafikiri isingekuwa tatizo lakini alikuwa na ndoto.
Huo mfano inaonyesha kwamba kama wako pamoja lazima
kuna ndoto zimeuwawa hapo kwahiyo huyo dada anadeni kwasababu hajafanya wajibu
wake Mungu aliomwitia.
Vilevile kama una mwenzi ambaye haamini Imani yako saa
nyngine anaweza asiamini malengo na ndoto yako kwasababu hivyo vinakuwa
vimechochewa na kile unachokiamini sasa
kama yeye anaamini tofauti na wewe hataruhusu zitimie. Na ndio maana neno
linatuasa katika 1 Wakoritho 6:14 “Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na
uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?” Usije ukaambatana
na mtu asiamini kwasababu wema na uovu au mwanga na giza haviwezi kukaa pamoja.
Kile unachoamini wewe ni mwanga lakini kwa vile yeye
yuko gizani anaweza asikijali ukajikuta haufanyi lile kusudi Mungu alilokuwekea
hapa duniani, Haleluyaa
Mwenzi mwingine anaweza asijali malengo na ndoto yako
kwasababu anaona unafanya tu vitu lakini hujamshirikisha, hebu leo chukua hatua
mshirikishe afahamu nini kinakukosesha usingizi je una wito wa kuwa mwanasiasa
ili upiganie haki za nchi yako mwambie tu maana ukikurupuka ndipo hapo
atakuzuia utabaki ukilalamika. Hii sio kwa wachumba tu hata WANANDOA
shirikishaneni nini malengo na ndoto zenu.
Umuhimu wa Kumshirikisha Mwezi ndoto zako:
1. Utaweza kujua kwamba uko na mtu ambaye
anajali na atakupeleka katika malengo yako au atakayeyaua
2. Kama anajali malengo yako basi ataweza
kukushauri hata jinsi ya kuboresha zaidi hayo malengo na ndoto
3. Atakuombea
kama anajali hayo malengo na ndoto zako
4. Atakupa uhuru wa kufanya shughuli mbalimbali
zinazohusika na kufanya malengo na ndoto zako zitimie kama vile kwenda semina
na warsha mbalimbali
5. Utafikia malengo na ndoto yako kwa
furaha kwasababu unajua yuko mpenzi wako anayeyajali pia
6. Utakuwa huru kufanya shughuli
zinazohusika na malengo na ndoto yako kwasababu mwenzako anajua , huna haja ya
kuficha ficha vitu kusema uongo ili kukwepesha kujulikana kile unafanya
Inawezekana uko katika mahusiano na tayari huyo mwenzi
anaonyesha dalili ya kutojali kabisa malengo yako, hebu liweke katika maombi na
ujichunguze je umemshirikisha na sababu za kuzuia ni nini woga au labda
anahofia washirika wako wa kuelekea hiyo ndoto? Kama washirika hawambariki
tafuta kwanini labda mko karibu kuliko yeye? Kama ndio katika haya badili jinsi
unavyoenda ili aridhike, ILA kama anakataa tu kwasababu yeye hataki ufanye
chochote kile endelea kuomba Mapenzi ya Mungu juu ya hilo Bwana atafanya njia
na kama sio wako utashangaa tu anajiondokea taratiibu.
Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Blog Mengi
Mazuri yanafanya, kama tunavyojua hii ni Zaidi ya Blog
BARIKIWAAA
No comments:
Post a Comment