Hili Somo limenibariki sana naomba na Mungu aseme na wewe unaposoma Somo hili muhimu
Specimen |
Luka 16: 1-13 “Akawaambia
wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na meneja wake. Ilisemekana kwamba
huyo meneja alikuwa anatumia vibaya mali ya tajiri yake. 2 Basi huyo tajiri
akamwita meneja wake akamwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayosikia kukuhusu?
Nitay arishie hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu kwa maana hutaendelea
kuwa meneja tena.’
3
“Yule meneja akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu anataka
kuniondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, na ninaona aibu kuombaomba!
4 Najua nitakalofanya ili nikipoteza kazi yangu hapa, watu wanikaribishe
nyumbani kwao.’
5
“Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa tajiri wake, mmoja mmoja. Akamwuliza wa
kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ 6 Akajibu, ‘Galoni mia nane
za mafuta ya alizeti.’ Meneja akamwambia, ‘Chukua hati hii ya deni lako,
ibadilishe upesi, uan dike mia nne.’ 7 Kisha akamwuliza wa pili, ‘Na wewe deni
lako ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ Yule meneja
akamwambia, ‘ Chukua hati yako, uandike mia nane.’
8
“Yule tajiri akamsifu yule meneja mjanja kwa jinsi alivy otumia busara. Kwa
maana watu wanaojishughulisha na mambo ya dunia hii hutumia busara zaidi kuliko
watu wa nuru kukamilisha mambo yao. 9 Nami nawaambieni, tumieni mali ya dunia
hii kujipa tia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.
10
“Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu hata katika
mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo hatakuwa
mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza
mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama
ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu
wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia
mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi
kumtumikia Mungu pamoja na mali.”
Katika mstari hapo juu Bwana Yesu anazungumza na
wanafunzi wake kama alivyokwisha kuzungumza na Petro katika Mathayo 16:13 -18 “13 Basi Yesu alipofika katika wilaya ya
Kaisaria Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu husema mimi Mwana wa Adamu
kuwa ni nani?” 14 Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji, wengine husema
ni Eliya; na wengine husema kwamba ni Yeremia au mmo jawapo wa manabii.” 15
Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani? 16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe
ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
17
Na Yesu akamwambia, “Umebarikiwa, Simoni mwana wa Yona, kwa maana si mwanadamu
aliyekufunulia hili, bali ni Baba yangu aliye mbinguni. 18 “Nami nakuambia,
wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu
za kuzimu haziwezi kulishinda. 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lo
lo te utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lo lote
utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
Bwana Yesu anataka kujenga Kanisa lake na milango ya
Kuzimu haitalishinda.
Kanisa ni mtu anayemwamini Kiristo yaani mimi na wewe.
Kuweza kushinda milango ya kuzimu lazima Mkiristo aweze
pia kuwa na Utawala wa fedha, kama
ilovyoandikwa katika mstari wa Luka 16:1-13 hapo juu.
Tajiri amesikia kwamba wakili anatapanya mali,
akamwambia wakili atoe hesabu na atamnyang`nya uwakili.
Wakili dhalimu akakumbuka kwamba Bwana wake amekopesha
watu kwa riba ambacho ni kinyume na Torati, akawaita akawapunguzia madeni yao
ili aweke urafiki nao maana ameona kwamba kazi yake ya uwakili inaondoka.
Bwana anategemea amtumie Mwamini alihudumie kanisa kwa
utawala wa fesha kama vile kutoa Zaka na sadaka nyingine.
Vitu muhimu vya kujifunza katika Neno hili:
1.
Mwamini anatawala fedha lakini sio za
kwake, Mali zote ulizonazo umepewa uzitawale lakini ni za Mungu sio za Kwako.
Wakili alikuwa anatawala mali za Bwana wake hazikuwa za kwake. Kwa yule aliye
katika sharia fungu la kumi tu ndio la Bwana lakini sisi tulio katika neema
vyote tulivyonavyo ni mali ya Bwana, Vyote ni vya Mungu.
Je Mpendwa uko chini Neema basi kama
uko chini ya Neema vyote ulivyonavyo ni vya Bwana ameweka tu mikononi mwako,
Vitu hivyo ni kama Mali, Watoto,Wakati , fedha nakadhalika
Kumbukumbu la Totati 6:7 “nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na
kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na
uondokapo.”
Watoto: Hata watoto wetu
tumepewa kama Zawadi tu tuwalee kama Mungu anavyotaka
Wakati: Siku ya hukumu
utatoa hesabu jinsi ulivyotumia wakati wako je ulitumia kwa ajili ya Bwana au
kwa ajili yako mwenyewe?
Mali na Fedha: Tutatoa
hesabu jinsi tulivyozitumia je tulitumia katika kazi ya Bwana au mambo yetu
wenyewe
1 Wakorintho 13:2 “Na ikiwa nina zawadi ya kutoa unabii+ nami
nazijua siri takatifu+ zote na ujuzi+ wote, na ikiwa nina imani yote kuweza
kuhamisha milima,+ lakini sina upendo, mimi si kitu.”
Sisi ni watumwa wa Upendo,
ina maana unaweza kuwa katika ngazi ya juu sana kama Nabii anayefundisha kwa
ufasaha sana lakini kama huna upendo ni kazi bure. Au mtu ana dhahada ya
Uzamivu katika mambo ya Theologia lakini kama hana upendo ni kazi bure.
Na njia mojawapo ya
kuonyesha upendo ni jinsi tunavyotawala fedha tulizopewa na Bwana kwa kutumia
katika kazi ya Bwana.
2.
Utoaji wa Fungu la Kumi ni wajibu wa Kila
Mkristo mwamini na litolewe kwa uaminifu.
Hiyo sio ya kwako unatakiwa utoe kwa
Uaminifu, Ili tujenge Kanisa la Kristo jambo la Kiroho ni kutoa fungu la Kumi
kwa Uaminifu.
Hizo 9 ya kumi zilizobaki bado sio za
kwetu tunakuwa nazo tu ili tuzitawale tumepewa uwakili bado ni mali ya Bwana,
kwahiyo unatakiwa umuulize Mungu akuongoze jinsi utakavyozitumia na akuonyeshe
mapenzi yake nini. Maana hata hizo zilizobaki haziwezi kutosheleza mahitaji
yetu ya kila siku ila tukimkabidhi Bwana atuongoze yeye atatoa katika hazina
yake kukutana na mahitaji yetu na tutakuwa na maisha ambayo hatuishi kwa hofu.
Neno la Mungu katika Wafilipi 4:19 “Na Mungu wangu atawapeni ninyi kila kitu
mnachohitaji kwa kadiri ya uta jiri wake mtukufu katika Kristo Yesu”
Hatuishi kwa hofu juu ya maisha haya
Bwana atashughulika na mahitaji yetu kama neno lake linavyosema hapo juu.
Tusiwe na hofu kwa kuzuia fedha
kufanya kazi ya Bwana maana atatujaza kadiri ya utajiri wake.
Mali tuliyonayo inatusiaidia kuwa na
hazina mbinguni, tuweke hazina Mbinguni
3.
Mwamini anatakiwa kuwa mwaminifu kwa kidogo
au kingi alichonacho
Waamini wengi wanachukia kutoa zaka
hadi wanakuwa na maandiko ya kuwatia moto wasitoe zaka kwasababu hawajajifunza
kuishi kwa upendo.
Yakobo 5:3 “Dhahabu yenu na fedha yenu vimeingia kutu na kutu yake itakuwa ushahidi
dhidi yenu na itakula miili yenu kama moto. Mmejilimbikizia utajiri kwa siku za
mwisho.”
Watu wenye mali nyinge wanaona wakitoa
fungu la kumi kubwa ni jingi sana kwa kanisa.
Na wenye mali kidogo wanaona hawana
kitu cha kumtolea Bwana na wakitoa watabaki masikini.
Hoja zote hizi zinaonyesha moyo wa mtu
na mahusiano na Mungu, Kwasababu mahusiano yakiwa mazuri mtu atatoa kwa upendo.
Hatutakiwi kuzipenda fedha hadi
zikatutawala bali tunahitajika kuishi kwa Utaua na kuzitawala Fedha.
1 Timotheo 6:10 “Maana kupenda fedha ni chanzo cha uovu wote. Tamaa ya fedha imewafanya
wengine watangetange mbali na imani na kuteseka kwa huzuni nyingi”
Mithali 3: 9-10 “Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.”
Tunatawala fedha kwa ajili ya wakati
ujao, Mali nyinge au Kidogo sio sababu ya kutotoa Zaka, kuwabariki masikini na
wenye uhitaji mbalimbali.
Vitu vyote Mungu alivyokupa ni
kwaajili ya Kujenga Ufalme wa Mungu,vitu kama Elimu, Hekima, Ujuzi vitumie pia
kuujenga ufalme wa Mungu.
Kumbukumbu la Torati 16: 17 “Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri
ya baraka ya Bwana, Mungu wako, alivyokupa”
No comments:
Post a Comment