Thursday, March 16, 2017

Mahusiano Kuelekea Ndoa - 3

Na Azgard Stephen

Azgard na mkewe
Shalom wana wa Mungu. Leo nataka nizungumzie swali la pili katika kasomo haka ka mahusiano. Swali hili lilikuwa linauliza kama je ni mimi kupenda au Mungu kunipa mke?

Maandiko yanasema katika Mithali, Nyumba na mali mtu hupewa na babaye, bali mke mwema mtu hupewa na Bwana

Kuna falsafa kadhaa za Kikristo katika swala la mke, hizi chache zikiwa maarufu;

1. Yupo mtu mmoja tu duniani ambaye ndio atakuwa mkeo/mumeo. Ukipishana naye umebugi, yaani imekula kwako.

2. Sio swala la wewe kupenda, ni swala la Mungu kukupa mke/mume, na lazima atakupa mtu sahihi utampenda mbele ya safari.

3. Wewe mhusika ndio muamuzi wa mke/mume wa namna gani unataka kuishi naye.

Falsafa zote zina mashiko yake kila moja, na zina supports zake.

Mimi nataka tu nirejee kule kule kwenye Mwanzo.

Ibrahim alimwambia mtumishi wake aende Harani kumtafutia Isaka mke kutoka katika "nyumba ya baba zake". Ibrahim alikuwa very specific, alikuwa ame-target wapi mke wa mtoto wake atoke.

Yakobo alienda kuoa Harani kwa Labani mjomba wake, Esau alioa binti wa kanaani. Maandiko yanasema, baba yake hakumfurahia Esau kwa kuoa binti za Kaanani.

Kuhusu Ibrahim kumuoa Sara Biblia haijasema mchakato ulikuwaje, lakini maandiko yanasema Sara alikuwa ndugu wa Ibrahimu. 

Mifano iko mingi sana inayotoa namna michakato hii ilivyofanyika.

Hoja yangu hapa ni dhahiri, kwamba suala la kuoa ni la mwilini lenye misingi yake rohoni. Hii ikiwa na maana, mchakato huu kwa kweli lazima Mungu ahusike, na wewe pia uhusike.

Yaani wewe ndio una hatimiliki ya kumhusisha Mungu katika huo mkataba, Yeye atabaki kuwa mwaminifu kukuongoza na kukushauri kama mkataba unalipa au la. Ukienda peke yako kuna vitu hutajua, utakuwa huna akili vizuri, upendo umefunika wingi wa dhambi.

Yaani mwambie Mungu niongoze kwenye mchakato. Ukipenda mahali mwambie Mungu nimependa huyu binti/kijana, muulize niende? Kwa sababu ni shahidi muaminifu na mtoaji asiye na hiyana, atakuruhusu kwa yule ambaye ana uhakika mtaenda sawia.
Nikutakie siku njema

Sir Azgard

No comments:

Post a Comment