Saturday, March 18, 2017

Mahusiano Kuelekea Ndoa - 5

Na Sir Azgard Stephen

Sir Azgard & mkewe
Shalom wana wa Mungu. Leo niendelee kidogo pale nilipoishia jana, hasa nizungumze sababu kadhaa za wadada kukaa kwenye mahusiano muda mrefu bila kuwa na uhakika wa hatma ya mahusiano hayo. Moja ya vitu vigumu duniani ni kukaa katika sintofahamu. Kukaa katika hali ambayo hujui nini kitatokea kesho.

Katika maisha ya mahusiano, kukaa katika mahusiano na sintofahamu ni miongoni mwa changamoto ya moyo.

Unaingia kwenye mahusiano na mkaka, mwaka wa kwanza unapita, mwaka wa pili, na kuendelea, na hujui ni lini huyo kakajusi atakuoa, zaidi sana huna uhakika kama atakuoa au la. Hii hupelekea vidonda vya tumbo kwa sababu ya mawazo.

Nitoe sababu kadhaa za jambo hili kutokea:

1. Kuingia kwenye mahusiano na mtu ambaye hayuko tayari kuoa. Utayari hapa namaanisha uhitaji. "Demand" ina "components" mbili muhimu, ability and willingness. Mtu anaweza akawa willing lakini hana uwezo. Hapa naweza kutupiwa mawe, lakini ni ukweli dhahiri kwamba hii ni miongoni mwa sababu. Nitoe mfano, mkaka amekuchumbia akiwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu. Hana uhakika wa wapi atakuwa na atafanya nini. Anakuja kupata kazi miaka 4 baadaye, wakati huo mmekaa kwenye uhusiano miaka mitano. Alikuchumbia ukiwa na miaka 24, sasa hivi una miaka 29. Kinachotokea ni yeye kujiuliza swali hili, hivi nimuoe kweli au nitafute mdada mdogo! Hii inakutengenezea probability, na likely unaweza kujikuta unaachika. Ni "nature" tu, kuwa mdada huwa anakuwa kwenye "peak" akiwa kati ya 22 na 27, mara nyingi (sio mara zote) mdada akifikisha 30 inakuwa ni changamoto kwake, wadada mnanielewa. Hii si katika roho, ni katika mwili, naomba nieleweke hapa.

Huwa nasema, ingia katika mahusiano na mkaka ambaye yuko tayari kuoa kesho, nikiwa na maana ana uwezo (demand) ya kukuoa hata kama ndoa ingewezekana kufanyika kesho. Sasa kuna watu wameingia kwenye mahusiano wakiwa wanafunzi, na wengine wakakaa kwenye uhusiano miaka 7 na zaidi, na wakaoana, na wako fresh kabisa,wapo. Ila ninachokisema hapa ni kwamba,kwa wengi hii imekuwa sababu ya sintofahamu.

2. Kuingia kwenye mahusiano bila malengo. Kwa lugha rahisi hii tunaita mahusiano butu. Yaani uko kwenye mahusiano na mtu, lakini hamjui hata mnaelekea wapi na lini kitatokea nini. Huyo kakajusi mnajuana ninyi tu, hakuna hata ndugu yako/yake anayejua. Hii ni "risk," kwani siku akiwaza vinginevyo hakuna anayejua, anasepa kimyakimya. Mkiwa kwenye mahusiano shaurianeni kuwafahamisha watu kadhaa, hasa watu wa karibu ikiwamo ndugu wachache wa karibu. Kuna wakati tufani inavuma, hawa ndio watawasaidia kushika makasia.

3. Kushikishana matatizo yooote. Yaani wewe uko kwenye mahusiano na kakajusi, anajua mpaka mshahara wa baba yako kuwa ni mdogo. Unamweleza kila kitu, na changamoto ikitokea home fasta ushamwambia na unataka akusaidie. Sifundishi roho mbaya, lakini kwa kweli kipindi cha uchumba kinajengwa zaidi na habari nzuri kuliko habari mbaya. Mshirikishe huyo kakajusi shida zako au za familia yako pale inapolazimu, tena si kwa kumuomba msaada bali kumshirikisha akusaidie kuomba. On the way akiona vyema kukusaidia itokee, lakini usimwambie. Hii inaweza kuwa ngumu kumeza,lakini naturally wakaka hawapendi kuombwa hela. Kuomba hela kwa mkaka ina connotation fulani sio nzuri. Anaweza asiseme, upendo hufunika wingi wa dhambi, lakini kwenye Medula Oblangata, kule kwenye subconscious mind kuna kitu inapandikiza ambacho si kizuri, kitachangia kwenye maamuzi ya kukuacha. Matatizo sio fedha tu, matatizo yoyote. Yafanye matatizo yako kuwa yako,japo kwa kipindi hiki tu,mkishaoana ndio yatakuwa yenu.

4. Kutokuwa wewe. Huwa nashauri, don't disguise. Be you. Tabia ni ngozi huwa haijifichi milele. Kuwa wewe from the beginning, ili huyu kaka asiwe na tabia mpya za kuzoea muwapo safarini. Kama kila siku kuna kitu kipya kinaunfold huyu kakajusi anachkua muda mwingi kutafakari kama ataweza kukibeba, akimaliza hiki kinajitokeza kingine. Akujue tu kuwa wewe uko hivi, ili muwepo pamoja achukue muda kukuzoea au hata kukushape. Hii itasaidia mbivu na mbichi kujulikana mapema.

5. Kuwa king'ang'anizi. Ni vizuri kupigania kilicho chako mpaka dakika ya mwisho, fight to the last minute, lakini sio vizuri kuwa king'ang'anizi. Yaani unaona kuna dalili zote kuwa huyo kakajusi haku-feel, hakupendi, lakini wewe unaendelea tu kumng'ang'ania. Kuna wakaka hawana "courage" ya kukwambia it is over, watafanya matendo tu. Ukiona hivyo, futa pumzi jua ni kwanini hakufeel, kama unaweza kurekebisha fanya hivyo, kama huwezi muite weka kila kitu kweupe. Tell him why don't you feel/love me. Asiposema tell him anaweza kuamua vinginevyo just in case. Kama anakupenda mtaendelea, kama ilikuwa kweli hakupendi "atasepa".

Huwa inaumiza, lakini ni heri kutokuwa nacho kuliko kuwa na ambacho sio chako.

6. Kuonja pembeni. Yaani kushirikiana tendo la ndoa. Ni kweli kuoa/kuolewa ni wajibu na utume katika nyumba ya Bwana, lakini pia kuna need of sex. Hii wapendwa wengi hatuikubali, lakini kwa kweli ndio hivyo. I married my wife, together with other things, because I am in need of sex. Sasa ukimpa huyo kakajusi, atachuchumilia nini? Atakuwa hana haraka kwasababu kile ambacho anaharakisha kukipata anakipata. My dear you will be in that relationship for 7 years. Mwisho wa siku anakuchoka na anakuacha. Si kila ambao wameonja pembeni wameishia kutokuoana, lakini sio kitu kizuri kufanya hivi. Haimpi Mungu utukufu, lakini pia itawavuruga.

Basi kwa hayo machache nikutakie siku njema

Sir Azgard

No comments:

Post a Comment