Sunday, March 19, 2017

Mahusiano Kuelekea Ndoa - 6

Na Sir Azgard Stephen

Shalom wana wa Mungu. Katika kuendeleza kujibu maswali niliyoweka hapa, leo nizungumzie swali la 4, swali ambalo lilihoji juu ya kuvunjika kwa mahusiano, shida ni nini?

Ukifuatilia tangu maelezo ya swali la kwanza, juu ya upendo, unaweza ukaelewa ni kwa nini watu wanakaa katika mahusiano na wakafanikiwa kuingia kwenye ndoa, lakini wengine wanaishia njiani.

Nianze kwa kusema, kuvunjika kwa mahusiano sio jambo zuri, linaumiza na kujeruhi. Lakini pia ikibidi kuvunja mahusiano ni bora kuliko kuja kuvunja ndoa au kuishi na msalaba milele.

Nimeeleza katika swali la tatu, juu ya kukataliwa na kuishi katika mahusiano katika hali ya sintofahamu. Tungependa watu waingie kwenye mahusiano, na mahusiano hayo yapelekee ndoa, hii ndio furaha yetu, na kwa kweli ndio mpango wa Mungu. Kwa bahati nzuri maandiko yanatupa kisa kimoja tu cha mahusiano yaliyotetereka, na Mungu akaingilia kati. Ni pale Yusufu alipotaka kumuacha Mariamu kwa siri kisa Mariamu ni mjamzito, Mungu akamfafanulia Yusufu na hatimaye Yusufu akaahirisha mpango wake. Kimsingi, mahusiano yakianza na kufikia lengo inapendeza.

Zipo sababu nyingi za mahusiano kuvunjika, mimi niweke hapa chache kati ya hizo:

1. Sababu za wawili hao kuingia kwenye mahusiano hazikuwa dhahiri. Yaani hapa unaingia na mtu kwenye mahusiano ukiwa huna sababu za kuingia kwenye mahusiano. Unakuta watu wako kwenye mahusiano hawana vision, they are just in relationship. Mtu anaona kuliko kuwa peke yake ni afadhali niwe na mtu wa kwenda naye “out”, na kuchat naye usiku kucha. Wawili hawa wakiwa kwenye safari hiyo, mmoja atazinduka usingizini, na kugundua kuwa anatakiwa awe kwenye serious relationship. Anamtafakari aliye naye kwenye mahusiano, hafai kuwa mke/mume. Kinachofuata hapo unaelewa, kuna mtu ataachwa, na mahusiano ndio yanakuwa yameishia hapo. Hii ni very premature, lakini ni common practice kwa vijana wengi hasa walio kwenye umri wa kati, yaani 22 mpaka 26. Bahati mbaya sasa kwa upande wa wadada, akiachwa hapa ana-panic, na anaweza akachukua maamuzi ya kumkomoa huyo mwenzake kwa kuingia kwenye mahusiano mengine ya ghafla. Huwa na yenyewe haina mwisho mzuri.

2. Kukaa kwenye mahusiano muda mrefu. Ukimchunguza sana bata humli. Baadhi yetu tunafikiri kukaa kwenye mahusiano muda mrefu ndio kuchunguzana vizuri. Watu wanakaa kwenye mahusiano miaka 5, na hawana sababu za msingi. Yaani uwezo wa kuoana wanao, lakini wanakaa tu kwenye mahusiano, hoja yao wafahamiane. Ni jambo zuri kufahamiana kabla ya kufunga ndoa, lakini kwa kweli kufahamiana hakuji kwa kukaa muda mrefu kupita kiasi.

Kuna sababu za kukaa muda mrefu, ikiwa haziepukiki, lakini mimi nashauri tu kuwa sio afya, ina risks nyingi. Kama mna mahusiano yenye dira, basi chukueni hatua msonge mbele badala ya kuendelea kuchunguzana.

3. Kuingia kwenye mahusiano mkiwa hamna uwezo wa kuoana. Hii inarejea kule kule kwa jana, lakini hoja yangu ya msingi hapa ni hii, unaingia kwenye mahusiano na mdada ilhali hauko tayari kuoa leo. Mfano, wewe ni mwanafunzi au “graduate”, huna kipato na unaishi kwenu au kwa mshkaji, halafu unaongezea na mahusiano juu. Unakaa muda wa kutosha tu na huyo dadajusi, ukimpa ahadi kedekede juu ya kesho yenu. Muda haugandi, time inasogea. Baada ya miaka 4 unapata kazi, lakini unagundua huyo dadajusi sio type yako, unaanza kufanya maombi ya kuachana kwa amani. My brother hakunaga kuachana kwa amani katika hiyo situation, utamjeruhi tu huyo mdada. Upande wa pili nao unahusika.

Hapa naomba nikazie, ingia kwenye mahusiano pale unapokuwa na uhakika wa kuoa kesho, na mdada ingia kwenye mahusiano na mkaka ambaye yuko tayari kuoa leo/kesho. “I don’t mean you become materialistic, I mean be realistic. Don’t misquote me by leaving your man with a vision for a man with television, you will end-up seeing the man with vision in your husband's television.”

I mean, go into relationship when you both ready for it, usiingie kwenye mahusiano kwa sababu wakaka wataisha.

Hapa nakumbuka wakati natoka chuo nikaambiwa kama huna relationship utapata tabu sana kupata mtu mtaani kwani ni wachache, eti kule chuo ni wengi

Nijuavyo mimi, sioi kwa sababu ni wengi, nimeoa kwa sababu wangu yupo.

Mdada mmoja, was my college young-sister, alimaliza chuo pale UDOM akiwa single. Nakumbuka akiwa mwaka wa tatu nilimuuliza kama yuko na mahusiano, akaniambia hana. Nikamuuliza kwa nini, akaniambia sentensi ambayo kamwe siisahau, "Mama ameniambia nisome, nijiweke vizuri, niwe wife material. Wakati ukifika nikitaka kuolewa mtu anaye-derseve kunioa atakuja." This was so powerful to me, na huyu dada hakuwa mpendwa.

Changamoto ya kuwa kwenye mahusiano na Serengeti Boy ni kwamba, unakuwa occupied na kwa hiyo unakuwa busy na mtu ambaye sio muoaji. Huchukui muda wa kutosha kujiandaa kuwa wife material kwasababu tayari "unaye" (ambaye siye). Na waoaji wanakosa nafasi kwa sababu kila wakija uko occupied. Umri unaenda, na huyo uliyenaye analiona hilo. Ikifika wakati yuko tayari kuoa, anagundua wewe sio wife material, anakuacha. Hii ni mbaya sana, lakini sasa inatokea na watu wanaumia, very bad.

4. Kuonja pembeni. Hili nimelizungumza kule kwa wadada. Zinaa huleta uharibifu, dawa yake ni toba tu. Mkiingia kwenye mahusiano halafu mkajihusisha na ngono, ni sababu kubwa ya mahusiano kuvunjika. Jambo la kwanza, hii inaondoa kabisa uwepo wa Mungu, mnaenda wenyewe. Lakini pili, maziwa yale yanayokufanya ufuge ng'ombe sasa unayapata dukani, why keep a cow! Ni muhimu kujizuia, ili iwape nafasi ya kumsogelea Mungu kwa sala na maombi, lakini pia iwape sababu ya kwenda huko kwa shauku. Nilisema sana katika hili, nisirudie. Jambo la msingi ni kwamba, mkishirikiana ngono inawapunguzia credit, value, na hivyo kuonana wa kawaida. Kuna tofauti ya ngono na tendo la ndoa; ngono huleta aibu, tendo la ndoa huleta utukufu.

5. Tabia zisizo za adili. Hii nimeiweka hivi kwa sababu kuna tabia ambazo mimi naziita si nzuri kuzi-practice kwenye mahusiano.

↘Tabia ya kuomba hela. Ni kweli huyu ni mchumba wako, lakini kwa kweli sio tiketi ya yeye kutatua shida zako zote. Hii ni kwa pande zote. Dada mmoja alimuacha kakajusi wake kwa sababu tu huyo kakajusi alikwenda kuchukua gari ya dadajusi na kukaa nayo, kupigia misele. Dadajusi akaona huyu ni “Mario” akaachana naye. Si jambo baya mkaka kutumia gari ya dadajusi wake, lakini pale inapolazimu, sio kupigia misele.

↘Kueleza matatizo ya kwenu. Yaani kabla sijaingia kwenye ndoa na wewe najua kuwa kwenye familia yenu uchawi umeweka makao. Ni advantage ya kakajusi kujua anakoingia, lakini sasa wewe usimtangazie. Sasa kama umemwambia kwenu wachawi, akikukimbia utamlaumu? Ni kazi yake kuchunguza kwenu kukoje, akijua atachagua kusuka au kunyoa, akikuuliza mwambie ndio kuna hiyo shida, ila mimi nimetengwa nayo na damu ya Yesu. Let your problems not to be problems.

↘Kuelezea changamoto za mahusiano yako ya nyuma. Wengi hapa watasema, kuwa muwazi, usiifiche historia yako. Mimi nasema burry the past, live your today. Kama atataka kujua huko nyuma mahusiano yako yalikuwaje, mwache achimbe, akijua akikuuliza mwambie ndio yalitokea, lakini hiyo ni historia. Simaanishi umfiche kuwa hujawahi kuwa na mahusiano, akikuuliza mwambie, asipokuuliza usimwambie. Hivi kwani ukimwambia inaongeza nini katika mahusiano yenu? Sasa wewe unaingia kwenye mahusiano leo, kesho unaitisha outing ya kumwambia changamoto za mahusiano yako yaliyopita, in the name of transparency. My dear, you are digging ur own grave, achana na hiyo kitu. Yazungumzie pale tu kunapokuwa na strings ambazo unaona zinaweza kuhatarisha mahusiano yenu ya sasa, otherwise don’t talk about. I know I swim up-stream in this, lakini sijawahi kuona manufaa ya jambo hili.

↘Kuigiza. Unaishi maisha yasiyo halisi. Unaazima gari la mshkaji utoke out na mchumba wako. Kila anachoomba mpaka unakopa umtimizie. Be you, because the day she/he realise the real you, she/he will dump you definitely. Unavaa sketi ndefu ilhali unajua kabisa huwa sketi zako ni za magotini. Vaa sketi zako, akupende nazo hizo. Siku mojamoja onana naye ukiwa hujapaka poda, auone uso wako halisi. Usihofie kuachwa, ila afadhali akuache mapema kuliko akikuacha mwezi mmoja kabla ya ndoa baada ya kukutembelea ukiwa unaamka by surprise. Be you.

↘Kujipendekeza kwa ndugu wa kakajusi/dadajusi. Ni jambo zuri kufahamika ukweni, ila usijipeleke. Ni jambo la staha mkaka kwenda ukweni, ila ni jambo la aibu mdada kujipendekeza ukweni. Acha akupeleke, na kama unataka kwenda mwambie akupeleke. Sio unachukua namba ya dada yake na kuanza kujitambulisha, this is bad.

↘Kukagua simu ya kakajusi/dadajusi wako. Another up-stream swimming. Una uhuru na haki ya kuperuzi simu ya mchumba wako, lakini sio tabia nzuri. Huwa ina connotation mbaya, humuamini. Leave his/her phone alone, mind yours. Simu ni private property, kupekenyua humo ni kujivusha mipaka ya umiliki. Mkiingia kwenye ndoa mtayaamua, lakini katika mahusiano sio tabia nzuri.

↘Kutokuwa nadhifu. Pamoja na kwamba umeshampata na ni wako, lakini sio tiketi ya kuwa rafu. Kila mtu anapenda kilichopendeza, pendeza my friend. Unaenda kuonana na kakajusi/dadajusi wako, vunja sanduku lako japo kidogo. Usiende kuvunja la rafiki, vunja lako. Be real, and be smart.

Kwa hayo machache niwatakie siku njema.

No comments:

Post a Comment