Bwana Asifiwe wapendwa karibu
tena katika Masomo yenu ya Uchumba hadi Ndoa yanatoletwa kwenu na Mshauri wako.
Leo tutazungumzia jambo
muhimu sana ambalo limesumbua mahusiano mengi ya uchumba na Ndoa pia, jambo
lenyewe ni Mahusiano ya nyuma ambayo mtu alikuwa nayo. Mahusiano hayo ni kama
mkaka au mdada alishakuwa na mchumba mwingine huko nyuma lakini ikashindikana
kuendeleza mahusiano ikabidi wavunje uhusiano. Hayo ndio mahusiano hasa
nitakayozungumzia leo.
Mahusiano ya nyuma mara nyingi
huvunjika pale mnaposhindwana tabia, mitazamo, maamuzi na kadhalika na
kadhalika.
Mpendwa wangu yamkini huko
nyuma kabla ya kukutana na huyo mtarajiwa wako ulishakuwa na Mahusiano, ni muhimu
sana kuhakikisha unachukua maamuzi thabiti kuhakikisha kwamba hayo mahusiano ya
nyuma yanaisha na hakuna kingine kinaendelea kati yenu zaidi ya salamu tena tu
ikitokea tu mmekutana uso kwa uso sio unaanza kumpigia simu enhee unaendeleaje
hiyo ni hatari na dhambi ya kutokuwa muaminifu.
Siku hizi ndoa zina shida
kubwa ya Cheating kwasababu watu hawakuachilia mahusiano ya nyuma. Au unakuta
mtu anampigia Simu yule mwenzi wa zamani na kumuelezea jinsi anavyopata matatizo
labda na uhusiano wa sasa wenyewe wanaita a sholder
to cry.
Nasikitika sana maana hayo
mambo yako makanisani pia siku hizi ni jambo la hatari sanaaa. Sasa wengine wataendeleza huo uhusiano kwa
siri mpaka wanafunga Ndoa unaendelea hivyo hivyo kwahiyo utashangaa Ndoa mwezi
imevunjika kumbe shida ni Mahusiano ya Zamani jamani hiyo Roho ishindwe
naikemea kwa Jina la Yesu.
Nilisoma mahali kuna dada
alikuwa anakwenda kuolewa ile siku moja kabla ya ndoa eti akaenda kuagana na
mtu wake wa zamani basi yaliyomkuta huko ikawa ni mauti na dunia nzima kujua
siri na uchafu huo alikuwa anaufanya.
Unaweza kuona labda leo
hujakamatwa lakini unatakiwa ujue mpendwa wangu Mungu hapendi vuguvugu kama
umeamua mimi ni wa Yesu mfuate umeamua kurudi nyuma kaa nyuma lakini usijifishe
kanisani ukajifanya kondoo kumbe wewe ni mbwa mwitu unamfanyia mwenzako ubaya
anakuamini sana anafikiri amepata mwenzi mwaminifu kumbe wewe unafanya
uasherati ndugu kuna malipo, Jihadhari ndugu yangu.
Mahusiano ya zamani ndio
chanzo cha nyumba ndogo tunachoona katika jamii watu wamegeuza fashion.. Siku
hizi mtu haogopi kama huyo mtu ameoa au ameolewa ni Hatari mpendwa Jihadhariii.
Madhara
ya Mahusiano ya Zamani:











