Thursday, June 19, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Jiepushe na Mahusiano ya Zamani


 
Bwana Asifiwe wapendwa karibu tena katika Masomo yenu ya Uchumba hadi Ndoa yanatoletwa kwenu na Mshauri wako.

Leo tutazungumzia jambo muhimu sana ambalo limesumbua mahusiano mengi ya uchumba na Ndoa pia, jambo lenyewe ni Mahusiano ya nyuma ambayo mtu alikuwa nayo. Mahusiano hayo ni kama mkaka au mdada alishakuwa na mchumba mwingine huko nyuma lakini ikashindikana kuendeleza mahusiano ikabidi wavunje uhusiano. Hayo ndio mahusiano hasa nitakayozungumzia leo.

Mahusiano ya nyuma mara nyingi huvunjika pale mnaposhindwana tabia, mitazamo, maamuzi na kadhalika na kadhalika.

Mpendwa wangu yamkini huko nyuma kabla ya kukutana na huyo mtarajiwa wako ulishakuwa na Mahusiano, ni muhimu sana kuhakikisha unachukua maamuzi thabiti kuhakikisha kwamba hayo mahusiano ya nyuma yanaisha na hakuna kingine kinaendelea kati yenu zaidi ya salamu tena tu ikitokea tu mmekutana uso kwa uso sio unaanza kumpigia simu enhee unaendeleaje hiyo ni hatari na dhambi ya kutokuwa muaminifu. 

Siku hizi ndoa zina shida kubwa ya Cheating kwasababu watu hawakuachilia mahusiano ya nyuma. Au unakuta mtu anampigia Simu yule mwenzi wa zamani na kumuelezea jinsi anavyopata matatizo labda na uhusiano wa sasa wenyewe wanaita a sholder to cry.

Nasikitika sana maana hayo mambo yako makanisani pia siku hizi ni jambo la hatari sanaaa.     Sasa wengine wataendeleza huo uhusiano kwa siri mpaka wanafunga Ndoa unaendelea hivyo hivyo kwahiyo utashangaa Ndoa mwezi imevunjika kumbe shida ni Mahusiano ya Zamani jamani hiyo Roho ishindwe naikemea kwa Jina la Yesu.

Nilisoma mahali kuna dada alikuwa anakwenda kuolewa ile siku moja kabla ya ndoa eti akaenda kuagana na mtu wake wa zamani basi yaliyomkuta huko ikawa ni mauti na dunia nzima kujua siri na uchafu huo alikuwa anaufanya.

Unaweza kuona labda leo hujakamatwa lakini unatakiwa ujue mpendwa wangu Mungu hapendi vuguvugu kama umeamua mimi ni wa Yesu mfuate umeamua kurudi nyuma kaa nyuma lakini usijifishe kanisani ukajifanya kondoo kumbe wewe ni mbwa mwitu unamfanyia mwenzako ubaya anakuamini sana anafikiri amepata mwenzi mwaminifu kumbe wewe unafanya uasherati ndugu kuna malipo, Jihadhari ndugu yangu.

Mahusiano ya zamani ndio chanzo cha nyumba ndogo tunachoona katika jamii watu wamegeuza fashion.. Siku hizi mtu haogopi kama huyo mtu ameoa au ameolewa ni Hatari mpendwa Jihadhariii.

Madhara ya Mahusiano ya Zamani:      
                        

1. Kukosekana Upendo kwa Mwenzi wako

2. Kuharibu Uhusiano wako na Mungu

3. Kuharibu Mustabali wa watoto wako

4. Kulitukanisha Jina la Kristo

5.Kufanya vizazi vijavyo vione Ndoa haina maana

6.Kuharibu Mustabali wenu kama wana ndoa kwa kuwa na Migogoro kwasababu ha hayo mahusiano.

 

Njia zifuatazo zitakusaidia kujihadhari na Mahusiano ya Zamani;

1.Kuchukua Uamuzi Madhubuti kutokuwa na uhusiano au mawasiliano yoyote yatakayopelekea kuendeleza uhusiano huo

2.  Amua kufuta (DELETE) namba za simu, email, Facebook.etc pia wablock wakikutafuta,

3. Muombe Mungu akukomboe na mahusiano hayo, Mungu anaweza ndugu yangu

4. Ongea na Wachungaji au Washauri wa Mahusiano

5. Kaa mbali na watu wanaokukumbusha na kukuvutia katika mahusiano hayo.

Nilishaona kaka mmoja ameoa sasa akigombana na mke wake kidogo anakimbilia kwa mwenzi wa.zamani (ex) na kwenda kumuelezea yoooote na kwamba eti anajuta kuwa na huyo mkewe, hebu niambie mpendwa mwisho wa ndoa kama hii ni wapi si kuvunjika? Kwasababu huyo ex atakuwa amepata pa kulipiza kwasababu yeye hakuolewa, Nimekuja kukuomba leo yamkini ulikuwa hujui madhara yake nakuomba ndugu yangu Jihadhari tena kimbia kimbiaaa kimbia na Mungu atakisaidia.            

Hata kama huyo ex ni Billionaire na wewe umeoa au kuolewa na muuza mchicha , nakutia moyo asubuhi yako inakuja usitishike na mambo yakupita ya duniani ,Mungu atakwenda kukutembelea atakapoona uaminifu wako kwamba umeacha yote ukaamua kuwa na Maamuzi yanayolipa jina lake Utukufu.

Haleluyaaaaaaaaaaaaaaa

 

 

Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Mambo mengii mazuri yanakuja

 

Jina la Bwana Libarikiwe

 


2 comments:

  1. amina mpendwa kwa somo lenye mafunzo mazuri

    ReplyDelete
  2. asanteee nimelipata somo vizuri mtumishi,ubarikiwe sana.

    ReplyDelete