Tuesday, October 16, 2012

Pride au Majivuno




Leo ninapenda tuongelee  swala hili la Majivuno au Pride kama inavyotamkwa na wenzetu wazungu,

Tumesoma katika biblia Mungu hapendi kabisa majivuno na nafikiri ni kwasababu majivuno yanamfanya mtu awe na kiburi,na mtu anapokuwa na Kiburi si rahisi kumheshimu Mungu.

Kabla hatujaendelea naomba kwanza tuangalie neno la Mungu linasemaje kuhusu majivuno Zaburi 10:4 Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Hatapatiliza. Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu.” Hapa tunaona neno Kiburi badala ya Majivuno lakini Majivuno =Kiburi maana yanazaa Kiburi,tuendelee….

Kuna hatari kubwa sana Mtu anapokuwa na Majivuno kuona kwamba Yeye mwenyewe kwa nguvu zake ndio anaweza hadi anaweza kufikia sehemu ya kusema kwamba hakuna Mungu.

Katika maisha ya kila siku katika maofisi,au biashara tunazofanya,mashuleni,vyuoni,au hata makanisani tumekutana na watu wenye majivuno ambao wanaona kwamba wao wako juu sana kuliko wengine yaani wao ndio bora,wengi huwa na tabia hii labda kutokana na familia walizotoka kama kuna kipato zaidi,au ni mfumo tu wa kifamilia,au uwezo katika masomo au uwezo tu wa kuwavuta watu kwa maneno au convicing power. Utakuta mtu anajivuna hadi anasahau kwamba yeye ni kitu kidogo sana aliubwa tu kwa neema na anaishi tu kwa neema na si kwa lolote alilonalo katika maisha yao.

Mara nyingi hata makanisani tumeona watu wenye tabia ya majivuno kwasababu tu labda wako katika kikundi fulani labda ni waombaji,kikundi cha praise and worship,mtoaji sana labda wanafikiri kwamba wao ndio watu wa maana tu mbele za Mungu…

Watu wengine majivuno yamewafanya wasiende hata kanisani anampa tu mke wake sadaka labda au watoto waipeleke,Au wengine kwavile mchungaji anampenda basi ndio majivuno yanaanza anaona kwamba wenzake sio kitu.

Kuna mistari mingi ya Biblia inayozungumzia Majivuno au Pride au Kiburi unaweza ukajisomea na uweze kujipeleleza uko wapi. . Isaya 2:11, Kumbukumbu la Torati 8:14

Mungu atusaidie tuweze kuwa na maisha yanayomuinua yeye tu na wala sio kufikiri liko jambo lolote la kimwili linaweza kutuhesabia haki mbele zake

Kwa leo naona niishie hapa ili nikupe wewe mpendwa wangu nafasi ya kutoa Maoni yako jee wewe unaelewaje majivuno au unaonaje hili swala la Pride linapoingia kanisani au hata katika maisha ya kawaida na umejifunza nini katika hii post?



Karibu Tujadili!


 

 

 

4 comments:

  1. kwa hiyo tunatakiwa kuwa na tunda la roho liitawalo unyenyekevu na kujishusha (humbleness and submission). unyenyekevu sio dalili ya woga au aibu ila tabia ya kuutambua ukuu wa Mungu na kutembea katika mapenzi yake kwa kutambua yeye ni Muumba wa vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. pia yeye ni muweza aweza kumkweza (elevate, promote, higher life kind of) mtu yoyote atakavyo yeye pia aweza kumshusha mtu. tunda hili la roho ni hekima ya Mungu ambayo tunatakiwa tuiishi kila siku. Jina la Bwana libarikiwe

    ReplyDelete
  2. Amen Kabisa,umenena vyema mtumishi ,tunapaswa kumuomba Mungu atupe unyenyekevu

    ReplyDelete
  3. Ahsante sana kwa ujumbe!! Mummy Mlowe!

    ReplyDelete
  4. this site is to non-public doing this client really should attach http://casinogamesonlinee@blogspot.com

    ReplyDelete