Tuesday, November 27, 2012

Hoja Yangu Leo: Majina tunayowapa watoto Je yana Faida au Hasara Yoyote?


Majina tunayowapa watoto wetu yana madhara au faida yoyote katika maisha yao ya sasa na baadae?

Je unamshauri nini mtu ambaye anategemea kumpatia mtoto wake Jina Je ampe tu la Babu au Bibi Yake au lolote tu au ampe kutokana mambo na hali alizopitia katika kipindi  cha kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa mtoto huyo?

Tunaomba Mawazo na Ushauri wako umsaidie mtu anayejiandaa kumpa mtoto Jina..

 

 

Karibu Bonyeza Comment,Andika Maoni Yako,Halafu kibox kidogo hapo chini chagua Name uandike Jina au chagua anonymous,Halafu chagua Send.

 

 

Karibu Sana

5 comments:

 1. Jina linamuwakisha mtu ni muhimu kuangalia kwa makini jina unalompa mtoto

  ReplyDelete
 2. It real depends na mzazi mwenyewe. To me ni vizuri kumpa mtoto jina lenye maana nzuri na ambalo halitakuwa na Madhara. Maana kuna watu wanaita watoto "Shida" au Masumbuko au Tabu jamani kweli si unamtakia mtoto apate Shida maisha yake yote ?

  Iwapo ni mambo ya family that you have name your kid after your dad or mom ni vizuri kuombea lile jina na kulikomboa kabla ya kumpa mtoto.

  ReplyDelete
 3. Majina yote yana maana. Wengi wetu wana majina ya Waingereza na Wayahudi ambayo pia maana yao ni ya hivi hivi tu - akina Williamson, Johnston, etc.

  Kama si neema ya Mungu, watu wa kule kwetu wanaoitwa MASAMAKI, MASATU, MAFURU au akina Mwita (muuwaji), Marwa (pombe), Chacha (mwanaume) au akina Otieno ( Usiku), Onyango (Asubuhi etc)wangekuwa wana behave ki-ajabu sana.

  Andrew Mushi aliwahi kuniambia kuwa tuwaache watoto wachague majina yao wao wenyewe wakifikisha umri wa miaka 18. Kabla ya hapo waite kwa identity yoyote kama namba, etc

  ReplyDelete
 4. Luphurise the BloggerNovember 28, 2012 at 8:37 AM

  Jina sometimes lina-affect sana sana tabia ya mtoto nimeona watu kama shida na tabu kama alivyosema Philipina wanaishi katika shida kubwa.Au Masumbuko anakuwa anaishi katika masumbuko makubwa.
  Jina ni muhimu sana mpe mtoto jina ambalo litampa mustakabali mzuri hapa duniani usimpe jina ambalo litamfanye awe katika vifungo maisha yake yote

  ReplyDelete
 5. Majina yana maana lakini tumekua na mazoea ya kuwapatia manina watoto kutokana na majina ya wazee au kutoka ktk biblia kutokana na majira yakuzaliwa au matukio ya raha au shida ya kupatikana kwa mtoto huyo lakini ni vyema kufuata manina ya bible kwa sababu kila jina la biblia lina historia yake!

  ReplyDelete