Leo napenda kuzungumza juu ya Uchungu na jinsi tunavyoweza
kujiondoa katika hii hali ya uchungu……..
“Mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na
kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”
Mara nyingi katika maisha tunakunatana na
vitu vingi ambavyo kwa njia moja au nyingine vinaumiza sana mioyo yetu. Unaweza
kukutana na mtu akakuambia yaani moyo wangu unauma sana kutokana na jinsi
Fulani alivyonifanyia. Kuna mambo mengi sana ambayo yamepelekea watu kupatwa na
uchungu mioyoni mwao,vitu hivyo vyaweza
kuwa kama;
· Kijana alikuwa amechumbiwa au amechumbia halafu ghafla mwenzake
anavunja uhusiano tena mwingine anamwacha mwenzake bila taarifa anasikia tu leo
harusi ya aliyekuwa mchumba wako
· Wanandoa wameoana muda mrefu lakini bado hawajabahatika kuwa na
mtoto
· Mume au Mke kumuacha mwenzake
· Kuondokewa na mpedwa wako kama vile baba,mama ,mtoto ,mume,mke au
mtu yoyote wa karibu.(Nakumbuka
nilivyoondokewa na baba yangu ghafla nilipatwa na uchungu sana)
· Kupatwa na ugonjwa ambao hautibiki au jambo lingine lolote ambalo linampata mtu
na kumpa uchungu moyoni mwake.
· Wewe ni kijana au dada una umri mkubwa tu hujapata mwenzi wa maisha
Kila mtu ana njia yake ya kuonyesha
uchungu, wengine ndio wale utasikia wamepigana kama njia ya kulipizana
kisasi,lakini sisi kwakuwa ni viumbe vipya tunatakiwa kuwa tofauti maana neno
la Mungu linasema katika Warumi 12:19 “Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali
mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kulipiza
kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana."
Mtu mwingine
akiwa na uchungu anajifungia kabisa hataki kuonana na mtu yoyote na hataki hata
mawasiliano na mtu yoyote,anakuwa anajifungia tu na kulia. Lakini hii njia
haitamsaidia kabisa kumaliza uchungu bali anajizidishia uchungu tena anaweza
kupata matatizo mengine zaidi.
Wengine wakiwa
na uchungu wanaharibu vitu eti kuvunja vunja vitu kama vile TVs,Vyombo basi
hapo ndio uchungu utaachia ,jamani hayo sio mapepo kweli? Maana shetani ni
muhuni sana anaweza kuja kwa njia ambayo watu wakachukulia tu ndivyo
anavyokuwaga hivyo huyo,kumbe kipepo kimejificha ndani.
Mtu mwingine
akiwa na uchungu anakuwa anapungua uzito sana au kunenepa kwasababu inategemea
na kila mmoja anavyochulia jambo,mwingine anaweza hakawa hapendi kabisa hata
kula na mwingine hata kama atakula basi mawazo yanamfanya apungue tu uzito.
Sasa wapendwa
wangu hebu tutafakari kwa pamoja,sawa ni kweli kabisa jamani yule kaka au dada
amekuacha mataa tena masikini sijui na nguo mlishashona au kununua,ni kweli
kabisa mmekaa katika ndoa kwa miaka 10 au zaidi na bado hamjapata mtoto,ni
kweli kabisa mmeondokewa na wapendwa wenu mliowapenda na kuwazoea,ni kweli
kabisa umefukuzwa kazi au kuna mtu anakufanyia hila kazini ili ufukuzwe kazi au
ukose haki zako fulani fulani kazini,ni kweli kabisa jamani una ugonjwa ambao
umemaliza hospitali zote lakini wamekuambia hakuna tiba,ni kweli kabisa unajiona
kwamba una roho ya kukataliwa hakuna mtu anayekupenda kila unachokifanya hakuna
mtu anaona kinafaa au yawezekana wewe ni kijana wa umri mkubwa lakini haujapata
mwenzi wa maisha,LAKINI Tuangalie
neno la Mungu linasemaje basi kama umeshaumizwa na umekataa tama kabisa na
kukosa tumaini napenda kukuambia ndugu yangu liko tumaini hebu tusome wote neno
la Mungu kutoka Warumi 12:12 “Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha;
muwe na saburi katika shida na kusali daima”.
Tukimtumaini
Mungu tutakuwa wenye furaha daima na itatufanya tuwe na saburi katika yale
tunayopitia haijalishi ukubwa wa tatizo. Unapomtumaini Mungu unapata nafasi ya
kusali kama neno la Mungu lilivyosema hapo juu,ila ukikata tamaa na kutumia
akili zako mwenyewe mpendwa wangu hutaweza hata kusali kabisa.
Katika kitabu cha 1Korintho 10:13 neno la Mungu linasema “Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida
kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu,
ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya
kutoka humo salama.”
Kwahiyo
unapopita katika majaribu jipe moyo maana hata neno linasema kwamba majaribu ni
ya kawaida kwa binadamu ila Mungu ni mwaminifu hataruhusu jaribu lililo kuzidi
na atatupatia nguvu za kushinda na kutoka salama,Sema AMEN mtu wa Mungu!
Ninampenda
sana Mungu na Neno lake maana kila changamoto tunazopitia katika dunia hii yeye
alishatuwekea majibu yake. Jipe moyo songa mbele maana neno linasema katika
kitabu cha Waebrania13:6 “Ndiyo maana tunathubutu kusema: "Bwana
ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?"
Usikate tamaa,usiogope
mruhusu Mungu leo awe msaada wako na uamini kwamba hakuna
binadamu,ugonjwa,changamoto inayozidi ukuu wa Mungu,AMINA MPENDWA!
Ni maombi yangu, Mungu akuwezeshe
kusimama na kusonga mbele na kumtegemea yeye peke yake.
Kutoka katika meza ya Rejoice and
Rejoice by Luphurise
DADA LUPHURISE hongera sana kwa huduma hii nzuri ambayo Mungu amekupa. kweli kwa ujumbe huu utakuwa umewafikia wengi na hope pia wengi watapata uponyaji kwani katika ulimwengu huu kuna changamoto kibao kuanzia kukataliwa, kuondokewa na uliyempenda sana, kuachwa/kuachika, kutofikia malengo yako ya kimaisha kama kazi, kuoa/kuolewa, masomo, biashara n.k (list inaweza kuwa ndefu. Nashukuru sana mwandishi wa somo hili. umenisaidia sana, utasaidia wengine pia. songa mbele
ReplyDelete