Thursday, November 8, 2012

Kanisa Zuri ni lipi? What is a good church to go?

Kanisa Zuri ni lipi? What is the good Church to go?Leo nina  hili swali ambalo limewasumbua wengi sana,najua nimekutana na watu wengi wanauliza hili swali hivi ukitaka kujua Kanisa fulani uangalie nini ? NAWAKARIBISHA mtoe maoni yenu in any language English or Kiswahili.

Kwa kushiriki utakuwa umewasaidia watu ambao wako njia panda na hawajui cha kufanya ni nini juu ya Kanisa,wengine wameamua hata kukaa nyumbani tu.


Jinsi ya Kushiriki; Click kwenye Comment,halafu andika maoni yako,halafu katika kiboksi hapo chini chagua Anonymous au Name URL andika jina,halafu click Send

Karibuni Wote

8 comments:

 1. Hii hoja ina changamoto zake. Lakini niseme hivi, kama umeokoka, kanisa zuri ni lile ambalo Roho wa Bwana atakuongoza kuwa mshirika kwa wakati huo. Haimanishi kwamba itakuwa hivyo kwa wakati wote, kwani ushirika wako utaweza kubadilika kutokana na sababu mbalimbali na jinsi Bwana anavyokuandaa katika maisha yako ya kumtumikia yeye. Ni safari unayoanza pindi unapookoka mpaka unapotwaliwa hapa duniani.

  Ubarikiwe.

  ReplyDelete
 2. well said brother Cleopa,
  in addition, kanisa zuri ni lile linalozaa matunda ya wokovu.

  ReplyDelete
 3. Kwanza Mimi naamini Yesu kristo Ni kanisa, hivyo watu Katika kuchagua kanisa tufwate neno ambalo Ni chakula cha roho waliyowengi wanafwata makanisa kwa ajili ya miuujiza na uponyaji na Hilo shetani amelijua ndiyo maana makanisa mengi ya uwokovu watu wanatumia juju zaidi. Nadhani ukaribu na Mungu kwa usomaji wa Biblia utakuwa na Imani na utajazwa roho mtakatifu aliye tuachia kristu mwokozi wetu nae atakupa muongozo mzuri wa wapi pakusali.

  ReplyDelete
 4. Kanisa Zuri kwakweli ni lile ambalo linahubiri utakatifu,ukuu wa Jina la Yesu na neno la Mungu linazingatiwa sana.Miujiza Yesu anatenda makanisani ndioa lakini sio criteria ya kuwa kanisa zuri kwa miujiza tu. Tusije tukageuza makanisa ni waganga wa kienyeji,maana siku hizi watu wanapenda miracles churches,so unakuta watu wanabaki katika uchanga wa ukiristo

  ReplyDelete
 5. Nacahangia kwa
  Kanisa kwa maana ya Jengo ni mahali ambapo ambapo upo Ufalme Mungu aliye hai
  Kanisa Zuri Halipo kwa namna ya kulitafuta kibinadamu labda kwa kuishia sebuleni wewe unatakiwa kulifanya zuri.
  Kibiblia kanisa zuri ni lile ambalo limeoshwa na Damu Ya Mwanakondoo

  ReplyDelete
 6. Kanisa kwa ninavyojua mimi siyo jengo bali ni popote wanapokusanyika wawili au watatu kwa kusali.Na uzuri wa kanisa upo pale tu ambapo wanasali kwa kuzingatia mambo yafuatayo:kutazama wagonjwa,kusaidia yatima,wajane N.k hilo ndo kanisa zuri kwa uelewa wangu.asante!!!!!!

  ReplyDelete
 7. Kanisa zuri ni jengo pale wakusanyikapo wawili au zaidi kumuabudu MUNGU na roho wa kweli pia naktukuza bwana wetu Yesu kristo japo kuna makanisa mengi siku za leo lakini twatakiwa kuwa waangalifu kuna majengo yanayo itwa makanisa kama jina tuu yanayo tendeka nikinyume na mpango wa MUNGU !

  ReplyDelete