Wednesday, April 23, 2014

DAMU ICHORAYO MIPAKA na Pastor Sayuni Mngodo


Tusome kwa pamoja Yohana 5: 5-9

“5 Basi, hapo palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane. 6 Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo, akatambua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, "Je, wataka kupona?" 7 Naye akajibu, "Mheshimiwa, mimi sina mtu wa kunipeleka majini wakati yanapotibuliwa. Kila nikijaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia." 8 Yesu akamwambia, "Inuka, chukua mkeka wako utembee." 9 Mara huyo mtu akapona, akachukua mkeka wake, akatembea. Jambo hili lilifanyika siku ya Sabato.”

Yesu alipita katika birika lililokuwa likitibuliwa watu wa kwanza kudumbukia wanapata unafuu.

Akamkuta mtu amekuwa mgonjwa kwa miaka 38 amekaa pale eneo la birika akiwa amelala na kwenye ya godoro.

Yesu alipofika pale akamuuliza unataka nikufanyie nini, akasema hakuna mtu wa kunipeleka katika birika.

Jibu lake linafanya tujiulize hivi kweli hakuwahi kuona mtu wa kumsaidia.

Dunia haitafuti mtu wa kumpa msaada wa chakula au malazi bali inatafuta mtu atakayewanganisha na MUUJIZA wao.

Warumi 8: 19

“Viumbe vyote vinatazamia kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake”

Watu wana nia, shauku na njaa ya kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Ina maana kuna kitu hakiko sawa mahali fulani, kinasubiri udhihirisho wa wana wa Mungu.

Kutumika kama daraja kati ya dunia na utatuzi wa matatizo yao.

Najua utaniuliza nani ni mwana wa Mungu, hebu tusome mistari ya Biblia hapo juu

Yohana 1:11-12

“Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. 12 Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu”

 

Warumi 8: 14

“Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni watoto wa Mungu”

 

Kama umempokea Yesu wewe ni mwana wa Mungu

Katika Ofisi yako, biashara yako na majirani wajue wewe ni mwana wa Mungu.

Sasa hiyo ilikuwa msingi, tuingie katika somo la PASAKA sasa..

Fungua na mimi Kutoka 12: 1-13

“BWANA akamwambia Mose na Aroni katika nchi ya Misri, 2“Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani, mwezi wa kwanza wa mwaka wenu. 3Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana kondoo mmoja kwa ajili ya familia yake, mmoja kwa kila nyumba. 4Ikiwa nyumba yo yote ina watu wachache wasioweza kumaliza huyo mwana kondoo mzima, nyumba hiyo itabidi ishirikiane na nyumba ya jirani wa karibu, baada ya kuzingatia idadi ya watu waliomo. Mtaangalia ni kiasi gani cha nyama kitahitajika kulingana na mahitaji ya kila mtu. 5Wanyama mtakaowachagua, lazima wawe wa kiume wa umri wa mwaka mmoja wasio kuwa na dosari, mwaweza kuwachukua kati ya kondoo au mbuzi. 6Tunzeni wanyama hao mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi, ambapo lazima watu wa jumuiya yote ya Israeli wachinje wanyama hao wakati wa jioni. 7Ndipo watakapochukua baadhi ya hiyo damu na kuipaka kwenye vizingiti na miimo ya milango ya nyumba ambamo watakula wanakondoo hao. 8Usiku huo huo watakula nyama iliyookwa kwenye moto, pamoja na mboga chungu za majani na mikate isiyotiwa chachu. 9Msile nyama mbichi wala iliyochemshwa, lakini iwe imeokwa kwenye moto, kichwa, miguu na nyama zake za ndani. 10Msibakize nyama yo yote mpaka asubuhi, nazo kama zitabakia mpaka asubuhi, lazima mziteketeze kwa moto. 11Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka, hii ni Pasaka ya BWANA.

12“Usiku uo huo nitapita katika nchi yote ya Misri na kumwua kila mzaliwa wa kwanza, wa wanadamu na wa wanyama, nami nitaihukumu miungu yote ya Misri

Mimi ndimi BWANA. 13Damu itakuwa ishara kwa ajili yenu ya kuonyesha nyumba ambazo mtakuwamo, nami nitakapoiona damu, nitapita juu yenu. Hakuna pigo la uharibifu litakalowagusa ninyi nitakapoipiga Misri.”

Inawezekana kuna maeneo ambayo bado unapambana na Farao, ambaye ni Shetani. Kama vile wana wa Israel walivyoshikiliwa na Farao akikataa kuwaachia.

Mungu alikuwaameufanya moyo wa Farao mgumu ili ajue Yeye ni nani.

Mungu anasema nitawahukumu ili wajue Mungu ni nani

Kipindi cha Pasaka ni kipindi cha Mungu kuwahukumu maadui zako

Mungu anashuka kuagiza hukumu juu ya mingu inayopambana na wewe

Ili ijulikane kama wewe ni mwana wa Mungu

Yule malaika wa hukumu alishuka kuja kuharibu alikuwa anatafuta damu, mipaka ya damu. Na wote waliokuwa ndani ya mipaka ya damu walipona.

Mungu anaposhuka kukusaidia hatafuti sadaka japo sadaka ni muhimu, hatafuti waimbaji japo kuimba ni muhimu, anakuja kutafuta tu kama kuna Damu ya Yesu

Damu ya Yesu peke yake ndio inaweza kukutengenezea mipaka

Yesu alikuja kama Mfalme

Leo hii unaweza kuanza upya maana Musa aliambiwa leo ni Mwezi wa Kwanza

 

Efeso 6: 17

Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.

 

Chepeo ya Wokovu inakulinda.

Kama wewe ni Mkristo mzuri, unaimba, unatoa sanaa, Mungu hataangalia hayo siku ya hukumu Mungu bali atakuwa anatafuta wokovu ndani yako

Haijalishi Shetani au maadui zako wamejipanga kiasi gani, wakija wakakutana na Damu ya Yesu ni MIPAKA inayomzuia na UTAMSHINDA,

 

Amen

 

 

No comments:

Post a Comment