Habari ya leo mpendwa wangu, Karibu sana katika
Makala haya ya Uchumba hadi Ndoa yanayoletwa kwako na Mshauri wako kila wiki.
Leo tutazungumzia kipengele muhimu cha Kujihadhari
na matarajio potofu kuhusu Ndoa, au yaliyojengwa kuhusu Ndoa.
Matarajio potofu ni ile hali ya kuamini kwamba kuna
vitu fulani vitatokea au vitakuwa hivi halafu wala havitatokea na wala haviko
hivyo unavyotarajia.
Matarajio potofu kuhusu ndoa yako sana katika jamii
zetu sio za Kiafrika tu hata mabara ya Ulaya, yako katika jamii za dini
mbalimbali, kabila na mila mbalimbali
Najua hata wewe kuna matarajio potofu kuhusu Ndoa
ambayo utakuwa umeyaamini kwasababu ulizaliwa katika jamii ambayo yaligeuka
kuwa sehemu ya hiyo jamii.
Katika jamii zetu na mazingira yanayotuzunguka
matarajio potofu yanaweza kuwa na sehemu kubwa inayofanya Ndoa nyingi ziwe
katika shida ambazo zimekuwa nazo leo.
Kitu kibaya ni kwamba hata sisi Wakristo
tumeyaamini na tunayakiri maratajio hayo matarijio potofu, ndio maana leo
nimekuja kukuambia kwamba hayo ni potofu labda ulikuwa hujui.
Tuangalie Aina Tano za Matarajio Potofu kuhusu Ndoa;
1. Ndoa Ndoano au Ndoa si Lelemama
Mara nyingi kwenye sherehe mbalimbali za Harusi
utakuta pande mbili ya Bibi Harusi na Bwana Harusi wanapewa nafasi ya kutoa
nasaha sasa hapo ndio utasikia haya maneno yakisemwa katika nasaha na tena cha kushangaza utakuta watu ukumbini
wananapiga makofi.
Sasa wewe mzazi au mlezi mwenzangu unaposubiri ile sherehe
pale ndio uje kumwambia mtoto Ndoa si Lelemama au Ndoa ni Ndoano kwanini
umechelewa si ungemkataza au ungekataa mahari jamani, Ili basi kumuepusha na hiyo lelemama unafikiri ipo.
Maana kwa kusema pale ina maana unakiri kabisa kwa
mdomo wako Mwanangu Ndoa Ndoano au si Lelemama kwahiyo ukavumilie, pale unamfanya
huyo mratajiwa awe na hofu kubwa kwahiyo atakaa kimtegomtego ili tu akiona tu
kaugomvi kidogo anakumbukaa anhaa hii ndio ileee lelemama niliambiwa na baba au
mama siku ile pale Kibada Skyline Hall…Ohh mwisho wa siku anaanza tu kuhesabu
makosa siku anakurudia na mizigo ooh Baba na Mama ile Lelemama yangu anhaa
hukuwahi kuiona imekuwa lelemama kwelikweli Nimeshindwa na Nimerudi, Utajibu
nini mzazi mwenzangu au mlezi mwenzangu.
Haimaanishi kwamba kama wewe mzazi au mlezi ulipata shida katika
Ndoa yako na mtoto wako lazima apitie ulichopita, hata kidogo , na jaribu
ulilopitia je umetafuta Kusudi maana nimejifunza kila Jaribu ulilopitia katika
maisha lina kusudi sasa kwasababu tunashikilia sana Uchungu inakuwa Ngumu
kuliona Lile Kusudi ambalo ndilo hasa Mungu anataka tulifanye, Haleluyaaaaaaaaa
Sasa na wewe kijana au binti haya na wewe hata
hujaolewa unaanza kukaa barazani ooh unajua Bwana wanaume siku hizi wasanii tuu
Ndoa hamna, hakuna zote Ndoa Ndoano, unajua kinachotokea katika Ulimwengu wa
Roho, tusome pamoja Mithali 18: 21 “Mauti
na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”
Haya kijana na Binti yangu umeona Maneno ya Mungu
yanavyosema,kuwa makini unaongea nini wewe ni mtoto wa Mfalme wa Wafalme
usiishi kama watu wa mataifa ambao hawana Tumaini,badili Maneno ya Kinywa chako
leo, Sema mimi ndoa yangu itakuwa nzuri itabariki watu, itasimama kama Ushuhuda
na utapata hicho unachokisema.Aminaaaaaa
2. Ndoa ni 50/50
Hapa wanamaanisha usijitoe mzima mzima kwenye Ndoa,
mwenzako asije akakujua sanaa. Hayo ni maneno tena hata wazazi wanafundisha watoto wao hivyo.
Unajua Mungu anataka moyo safi,Ndoa ili iwe Ndoa
nakwambia ni kujitoa 100/100 asilimia katika maeneo ya kifikira, kimwili na
kiakili nakadhalika.
Ukikaa nusu nusu na ndoa yetu ya Kikriso ni ya milele
yaani kifo tu ndio kinatenganisha si utaumia sana mpendwa wangu maana utaishi
maisha fake maisha yako yote.
Mungu ndio alianzisha Ndoa na kama Mungu ndio
mwanzilishi alijua tu kwamba itakuwa nzuri ila tufuate kanuni zake, kila siku
kujikana na kuhakikisha uko katika mstari Mungu anaotaka
3. Ndoa ni sehemu ya kupunguzia matatizo
Wengine
wameoa au wameolewa ili kupunguza matatizo waliokuwa nayo kabla, labda
mmoja ana kipato kidogo sasa anajua akiolewa na mwenye kipato kikubwa atakuwa
amepata suluhisho,
Nakwambia ni kosa kubwa kuolewa na mtazamo huo,
kwasababu kama ni hivyo matatizo yako yatazidi mara mia maana sasa unaweza
kukuta mwenzako labda ana vitu vingine anavipa kipaumbele na sio kutapanya hela
kama ulivyofikiri, maana mwingine anaolewa au kuoa anafikiri kila wiki atakuwa
anapelekwa Sychells au Dubai kumbe mwenzako ana malengo mengine ya maendeleo,
sasa hapo unajikuta unakuwa frustrated ooh hanipendi , kumbe wewe ndio
unatakiwa kujua ndoa si sehemu ya kusolve matatizo yako ila inabidi ubadilike
ili uweze kuishi vizuri na mwenzako, Halleluyaaa, Bado mnanipenda kweli jamani……..
4. Mwanamke aliyesoma sana hafai kuwa mke
Nimekutana na hili swali mara nyingi jamani mama
mimi nina Masters au PHD nitaolewa kweli, ni kutokana na jamii ambavyo
imetufanya tuone kwamba sio sahihi.
Wengine wanasema ukitaka kuoa Bwana nenda zako
kijijini wakutafutie mchumba mwenye elimu ya chini sana au hana kabisa ili
niweze kumtawala hawa wasomi wana maswali sana sitawaweza,nani kakuambia Ndugu
yangu wewe unafuata kanuni gani ya Ndoa ya Dunia inavyosema au Mungu. Je hujui
kama unaweza kumchukua wa kijijini akitakata tuu anakuwa tatizo mpaka unajuta,
achana na hilo tarajio potofu kama Mungu amekukutanisha na mdada ana PHD au
Masters yeye Mungu huyohuyo atampa huyo dada hekima ya kuishi na wewe na wewe
hivyohivyo.
Ukimuamini Mungu kwamba yeye ndio anakupa wa
kufanana nae na ukaamini kabisa kwamba huyu amefanana nami chochote alicho
nacho hakimkoseshi sifa za kuwa mke, huo mtazamo utafanya uwe na Ndoa yenye
Amani sana.
5. Kuishi pamoja, kinyumba kwanza ili kuona kama tunaendana
Eti kuna mtu ameniambia kwamba siku hizi kuna
mtindo umeibuka Bwana, watu kwasababu wanajua Ndoa ni Lelemama ni Ndoano basi
wamevumbua njia zao wenyewe kwamba sasa ili kumsoma mwenzangu kama anafaa
kunioa au kumuoa nitest kuishi naye, yaani hiyo ni ajabu na kweli.
Hiyo si sawa kabisa maana nikipekua Biblia yangu
sioni popote kinyumba kimeruhusiwa na Mungu, lazima tufuate manual ya
aliyetuumba ili tuwe salama.
Ndoa ni mpango Kamili wa Mungu ukiingia ujue uko
katika mpango wake uache hofu na Mashaka, uwe na Imani kwasababu maisha yetu ya
Ukiristo ni maisha ya Imani.
Amini kwamba ukiingia katika Ndoa utashinda
majaribu yooote maana kwakweli lazima yaje, wala siko mahali hapa kukuambia
kwamba Majaribu hayatakuja yatakuja mpendwa wangu ila kama Neno linavyosema
katika Warumi 8 : 37 ”Lakini katika mambo
yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye
aliyetu penda.” TUJUE UTASHINDA NA UTAKUWA NA NDOA YENYE USHUHUDA, Aminaaaaaaa
Haya Mpendwa karibu tena Wiki ijayo Masomo yanaendelea , tuendelee
kuombeane Mungu ashushe vile anataka tule watoto wake maana na mimi nafundishwa
hapa, Amen
Barikiwa mpendwa wangu , weka maoni yako hapo chini ili kutiana moyo
basi mnakaa kimya sana jamani ili nijue siongea peke yangu, Ameen
Asante kwa kutuelewesha jinsi ya kuanza uchumba mpaka kufikia ndoa maana mawazo ya wengi tunaamini ukisha oa au kuolewa matatizo yameisha kabisa kumbe unatakiwa kupambanua mambo yaja. Barikiwa sana mtumishi wa Mungu kwa mafundisho mazuri Mungu akupe maona mazuri zaidi ili uzi kutufumbua macho ktk hili.
ReplyDeleteThis sounds great mummy I like it. Iam a long time married lady but it has just revive my marriage life.. very useful teachings
ReplyDeletebarikiwa sana mtumishi huduma yako inatujenga sana vijana.
ReplyDeleteEnter your comment...Ahsante
ReplyDeleteUbarikiwe mtumishi wa Mungu kwa maundisho yenye baraka. Ni mara yangu ya kwanza kuisoma blog yako. Ni kweli tuishi kwa kulifuata neno la Mungu siyo ulimwengu. Tusiache kuombeana ili shetan asifanikiwe ktk ndoa za wana wa MUNGU.
ReplyDelete