Friday, June 20, 2014

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili na Mama Mchungaji Deborah Said amefariki Dunia

 
Deborah Said wakati wa uhai wake
 
Mama Mchungaji na mwimbaji wa Nyimbo za Injili Debora Said amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 20/06/ 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Deborah Said ni mke wa Mchungaji John Said wa Kanisa la Victorious Living lililopo Mabibo External

Marehemu ameacha watoto wanne na Mgane Mchungaji John Said

Katika Uhai wake Deborah Said alikuwa ameimba nyimbo mbalimbali za Kumsifu na Kumwinua Mungu, utumishi wake uliwagusa wengi hata Tanzania, siku si nyingi alikuwa amezindua albamu yake ya Mti wenye Matuda

Deborah Said akizindua Albamu yake ya Mti wenye Matunda kabla hajatangulia kwa Baba
 
Blog imefanikiwa kuongea na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa Chama  cha Muziki wa Injili Tanzania  MC Joshua Makondeko ambaye amesikitishwa sana na msiba huu na Mara nyingi tuliona akituomba sana katika facebook wall yake tumuombee Deborah na hata Deborah aliporuhusiwa hospitali  aliendelea kumshukuru Mungu kwa Uponyaji wa mwimbaji huyo wa nyimbo za Injili, kwasasa MC Joshua Makondeko yuko safarini  Rukwa ameomba kila waimbaji wa Injili wote wafike kuifariji familia pia wafike na mchango wa elfu 10 wamuone Cosmas Chidumule

Msiba uko nyumbani kwao nyuma ya Mabibo Hostel karibu na Pepsi Bar uliza kwenye Msiba wa mama Mchungaji

Programu ya mazishi itakuwa kuanzia hawajaamua mpaka sasa ila itakuwa kuanzia wiki ijayo, Blog itaendelea kuwapata taharifa ya Ratiba ya Mazishi


POLENI WOTE KWA MSIBA HUU,Roho Mtakatifu Awafariji yeye ndiye Mfafiji wa Kweli
 

No comments:

Post a Comment