City Harvest, Bahari Beach
Sehemu ya mbele ya jengo jipya la City Harvest |
Disemba 25,
2016 ilikuwa siku ambayo itabakia kuwa ushuhuda kwa kanisa la TAG City Harvest baada
ya kufanya ibada ya kwanza katika jengo lake jipya lililopo Bahari Beach wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Uhalisia wa
kusanyiko wa ibada ya kwanza ambayo ilikuwa siku ya Krismas unaonyesha kuwa Ukuu
wa Mungu na saburi ya watu wa City Harvest katika kuuongoja hatimaye kuupokea
muujiza huo.
City Harvest imeweza
kuhamia kwenye jengo la kisasa la kufurahisha lilojengwa na wataaaluma
waliyobobea katika ufanisi na uhandisi wa majengo.
Kanisa hili
limeweza kwa nguvu za Mungu kujenga nyumba ya ibada ikiwa bado ni changa ndani
ya kipindi cha miaka minne tangu lianzishwe, kitu ambacho ni ushuhuda mkuu
kanisani hapo wa yale Bwana ametenda.
Mchungaji
kiongozi wa City Harvest, Architect Yared Dondo alielezea kwa furaha na
ushuhuda kwa safari ndefu ya changamoto ilipelekea kupata makazi ya kudumu
kwenye uwanja mkubwa wa ekari tano.
“Tunamshukuru
Mungu kwa kutuwezesha kuhamia katika eneo la letu ambapo ni makazi yetu ya
kudumu,” alisema.
City Harvest
ilianza kufanya ibada zake miaka michache iliyopita katika ukumbi wa sinema uliyopo
Mlimani City ambapo Mungu alikuwa anawezesha kulipa kodi ya Sh.900,000 kila
ibada kwa kipindi cha mwaka moja na nusu kabla kuhamia Mabibo gereji.
Jengo la Bahari
Beach lina uwezo wa kubeba watu 1,000 walioketi na ujenzi unaendelea mpaka hapo utakapokamilika
kwa ajili ya ufunguzi rasmi mapema mwaka 2017.
Kanisa jipya la
City Harvest lina ukumbi wa sinema ambayo unachukua watu takribani 200, ukumbi
wa watoto, sehemu ya wakina mama ambazo zimejengwa kwa kiwango cha kimataifa.
Kwa upande
mwingine eneo hilo lina maegesho ya magari zaidi ya 100, vifaa vya kuchezea
watoto, viwanja vya michezo, na shughuli za kijamii kama shule ambayo itajengwa
hapo.
City Harvest kama kanisa linalokua wanafurahia
namna Mungu amefungua milango kwa njia
ya kipeke, hatua itakayotoa
nafasi kukamilisha maono ya kumtumia
Mungu.
Nguzo za chuma
zilizoshikilia jengo hilo ziliagizwa kutoka nchini marekani na kufanya kanisa
hilo kupata jengo kabla hata ya kupata kiwanja cha kujenga.
Mfumo wa kisasa
wa kuunda majengo kwa nguzo za chuma unaofahamika kama “pre-fabrication” ndiyo
uliwezesha City Harvest kuweza kumiliki jengo huko muujiza wa kiwanja
ukifuatia.
Ibada ya kwanza
Siku ya
Krismasi mwaka huu ndiyo ilikuwa ibada ya kwanza ya City Harvest katika jengo
hilo jipya, na wageni kutoka maeneo mbalimbali walifanikiwa kufika ikiwemo
mhubiri na Mtumishi wa siku nyingi, Askofu Titus Mkama
Mchungaji huyo
ndiye aliyealikwa kutoa ujumbe wa Neno la Mungu ambapo alihubiri kuhusu Kuishindania
Imani akiongozwa na andiko kutoka kitabu cha Yuda 1:3 na kusisitiza kuwa yeye
atakayeshindana na kushinda, ndiye atapewa taji stahili
Historia fupi
Umisheni
City Harvest kama ilivyo na moyo wa kuhudumia na kuwafikia watu hasa vijana
wanataaluma na maeneo mbalimbali yasiofikiwa, katika jingo hilo jipya kutakuwepo
ofisi maalumu za umisheni na uinjilisti, ikiwemo vyumba kwajili ya maombi na
kambi za vijana ambazo zitakuwa wazi kwa saa 24 kila siku.
Kanisa
hili limejikita zaidi kwenye huduma za kiinjilisti na kila mwaka hushirikiana
na vyama vya wanafunzi wakristo vilivyopo vyuo vikuu kwenye kupeleka injili
sehemu mbalimbali nchini.
Kwa
mwaka huu unaoisha; City Harvest limeweza kufanya kazi ya umisheni sehemu
mbalimbali ikiwemo Mpwapwa mkoa wa Dodoma, Lindi, Bagamoyo, Kibaha na Mkuranga
kutoka Mkoa wa Pwani.
Mpaka
sasa Kanisa limeshirikiana na wanafunzi na wamishenari wa hapo kanisani na nje
ya nchi kupeleka Injili ya uwokovu zaidi ya wilaya 20 nchini na nchi za
Sudani
Kusini na Msumbiji, na mipango ikiwepo kufika nchi nyingine zaidi.
Watoto
CityHarvest huthamini sana watoto na kuwalea katika misingi ya mafundisho Mungu kwa
ajili ya kukua kiroho na kimwili.
Watoto
wa City Harvest hupewa nafasi za kuhuduma ndani ya kanisa pia katika shughuli
za kijamii nje kanisa ikiwa kufikia watoto wenzao. Katika jengo hilo jipya,
watoto wana sehemu maalum kwajili kuendesha ibada zao pamoja na sehemu za michezo
ya watoto.
Vijana
Kanisa
la City Harvest ambalo limelenga kuinua vijana wana taaluma ambao wamejizatiti
kwenye ubora na maono yao, limelenga kuboresha na kutumia taaluma zao kwa ajili
ya majukumu ya Ufalme kwa mafanikio kupitia
uadilifu,
ubunifu na ubora kama mabalozi waaminifu wa Kristo.
Waefeso 2:21-22
Katika
yeye, jengo loye linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu
katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu
katika Roho
No comments:
Post a Comment