NA MCHUNGAJI JOEL HAMULI
Mwanzo 24
1. Kupata
mwenzi miongoni mwa WAAMINI. Mwanzo 24:1-4
-
Abrahimu alimtaka mtumishi wake
kumtwalia Isaka mke kutoka kwa "jamii yake"
-
1Wakorintho 15:15-16 huwezi
kujiunganisha na "makahaba" au kufanyika mwili mmoja na wasioamini
2. Chochote
ukitakacho kwa Bwana unakipata kwa IMANI.
-
Mwanzo 24:6-7 Mungu alimuapia Ibrahimu
kumpa uzao wake nchi hiyo. Hivyo alimwamini Mungu na akamwambia mtumishi wake
kwa imani kwamba Mungu angemtuma malaika wake kumwongoza kupata mke.
-
Filemoni 6:4 msisumbuke kwa neno
lolote bali ktk kila jambo kwa kuomba na kushukuru. Badala ya kujishughulisha
na kujisumbua sana kutafuta mke/mume, mwambie Mungu kasha endelea kuamini.
3. Lazima
kuwe na MAANDALIZI. Mwanzo 24:10-11
-
Maandalizi stahiki kadri ya taratibu
zinazokubalika ni muhimu.
-
Luka 14:28 Kabla ya kujenga, kaa chini
hesabu gharama
-
Jiandae kiroho, kimwili, kisaikolojia,
nk
-
Ikiwa wamtaka kutoka kwa Mungu, timiza
mapenzi yote ya Mungu. Matendo 20:27
4. Fanya
MAOMBI. Mwanzo 24:12-14
-
Ombea jambo hili na ujue mapenzi ya
Mungu kulihusu.
-
Usiwe mgumu kubadilika na kulazimisha
mapenzi yako, unaweza kuwa na vigezo vyako, lakini si lazima Mungu ajibu hivyo.
Ila waweza kuomba ili kupata uthibitisho wa ki-Mungu
5. Chukua
HATUA
-
Kwa tamaduni nyingi mwanaume ndiye
huanzisha mchakato kwa kwenda kuomba uchumba. Mwanamke anaweza pia Biblia
haijakataza, lakini zingatia matokeo yake. Kwa kuwa upendo unaoshikilia ndoa ni
wa mwanaume, inabidi yeye ndio ashawishike zaidi juu ya msichana. Ndiyo maana
yeye anaagizwa kupenda na mwanamke kutii.
6. Kuhusisha
watu WENGINE. Mwanzo 24:28-31, 50
-
Yafaa kueleza familia. Zamani familia
zilibeba jukumu la kijamii na kiroho
-
Kwa sasa majukumu ya kiroho yapo kwa
kanisa, kwa hiyo waambie viongozi wako wa kiroho wakuongoze, hata kabla ya
kwenda kwa wazazi
7. Msichana
KUKUBALI. Mwanzo 24:57-58
-
Msichana inabidi kwa utashi wake
mwenyewe aamue kumkubali na kuolewa na mwanamume husika.
1Wakorinthi 7:39 inaongelea
juu ya mwanamke kuolewa na mwanamme “amtakaye”. Kuingia kwenye ndoa kwa
kulazimishwa si mapenzi ya Mungu.
Makala hii ni sehemu ya semina ya Mahusiano na Ndoa iliyofundishwa kanisani City Harvest na ni sehemu ya kitabu kilicho njiani.
No comments:
Post a Comment